Thursday, October 18, 2012

Miaka 5 baadae. Phillips Lucky Dube.....Aliwa(ga) nini?

Ikiwa ni miaka mitano tangu kuuawa kwake, nimeona ni vema kurejea bandiko langu hili kumhusu. Kuhusu sanaa yake na namna alivyounganisha maudhui ya nyimbo zake.
Najiuliza....ALIWAZA(GA) NINI? 
KARIBU.

LUCKY is What We Are! (click here) Ndivyo alivyoweza kueleza kwa ufupi mchambuzi Larry Leiber wa ReggaeMovement.com NAMI NAKUBALIANA NAYE.
Nimeshaandika mara kadhaa kuhusu msanii huyu Philips Lucky Dube. Nimekuwa nikimfuatilia kwa ukaribu kwa miaka 9 sasa tangu nilipopewa CD yake na Kaka Philbert Kiyenjeo (nuff respect Kaka) ambayo ilikuwa ni The Best of House of Exile, Slave & Prisoner. Nikirejea kwa ufupi kuhusu nipendacho kumhusu ni kuwa alikuwa akiandika na kuimba nyimbo ambazo ni HADITHI KAMILI na alitumia lugha nyepesi na pia midundo iendanayo na uhalisia wa tukio. Ni kati ya wasanii wachache ambao wamefanikiwa KUNIWEKA katika fikra za tukio kwa uhalisia wake. Pia Lucky Dube anafahamika kwa kueleza visa viiingi vya kweli ambavyo ama amekumbana navyo au vimetokea kwenye jamii yake. Mfano wa nyimbo ambazo zinaniweka kwenye UHALISIA WA TUKIO ni ule aliouimba akizumzungumzia Askari ambaye alikuwa amereja toka vitani ambako yaonekana alikwenda bila hiari (kama ilivyo kwa askari wengi) na kurejea akwa na MSONGO WA MAWAZO na MAJUTO juu ya mauaji aliyoyafanya huko vitani na hasa ya watoto. Na sasa alikuwa amechoshwa na NDOTO NA SAUTI za aliowaua na alikuwa tayari kujiua.
Tangu nimeanza kuusikiliza wimbo huu 2003, sijachoka na bado nausikiliza. Tulishaujadili hapa na waweza kuurejea kuusikiliza na kusoma lyrics zake HAPA. Lakini jambo ambalo bado nawaza kuhusu Lucky Dube ni uwezo wake wa kuwaza kitu ambacho kipo, na ambacho kingeweza kutendeka kwa namna fulani lakini hakikutendeka hivyo japo kinaleta maana halisi ya fikra ya kutendeka kwake. Yaani alikuwa na uwezo mkubwa saana wa KUSADIKI habari ama tukio ama maisha halisi kwa namna ambavyo yanaweza KUSADIKIKA. Alieleza, kuuliza ama kufafanua utata ama fumbo ama mwenendo fulani wa maisha kwa namna ya kipekee.
Tunaweza kuangalia baadhi ya nyimbo kuwaza kwa pamoja kuwa ALIWAZA NINI??
Kwanza tuanze kutafakari nyimbo DIVORCE PARTY na COOL DOWN ambazo ni kutoka katika albamu yake ya The Other Side.
DIVORCE PARTY unaeleza familia ambayo ilikuwa ikijifurahisha kwa sherehe mbalimbali na sasa wameamua kuwaalika watu wakisherehekea kutengana kwao. Sikiliza mwenyewe hapa chini na lyrics zake waweza kuzipata HAPA
 

Na wimbo huu wa COOL DOWN ni kuhusu wapenzi ambao wameoana kwa miaka 17 lakini wameonekana kufumaniana. Lakini kila mmoja anampooza mwenzie kuwa "Pooza munkari Mpenzi, hakuna la kukufanya uwe na shaka kwani kila kitu kiko kama kinavyotakiwa kuwa. Haijalishi ni wapo "ntapata hamu", nitakula nyumbani"
Labda ukiusikiliza hapa chini utaweza kutafakari alichokuwa akiwaza kuandika nyimbo hizi
Waweza fuatilia lyrics zake HAPA
 

Pia aliimba wimbo uitwao SOLDIERS FOR RIGHTOUSNESS ambao ulizungumzia "ASKARI" wa haki wanavyotakiwa kuwa na walivyo tishio kwa wanyonyaji na wanyanyasaji katika jamii. Ameueleza ki-utani na kwa kufurahisha lakini unaweza kupata ujumbe halisi.
Sikiliza wimbo huo hapa chini kisha waza uzito wa ujumbe, midundo, UKWELI uliopo ndani mwake. Lyrics zake zapatikana HAPA
 

Lucky pia aliwahi "kuingia akilini" mwa watoto na kueleza raha ya utoto kwa namna ya pekee. Lakini pia alieleza KARAHA iwapatao wale matajiri tunaoweza amini kuwa wana kila sababu ya kufurahi. Alifanya hivyo katika wimbo wake MY WORLD ambao waweza usikiliza hapa chini kutambua utundu aliokuwa nao katika kueleza utoto, utajiri, chanzo cha furaha na kufuta dhana potofu kuwa pesa ni chanzo cha furaha. Lyrics za wimbo huu zapatikana HAPA
 

Dube aliwahi pia kuweka CHEMSHA BONGO kuubwa akiuliza ni kipi ama nafasi gani ungependa kuwepo? Ya Mfungwa / Mtumwa alishwaye akasaza ama Mtu huru afaye njaa?
Wimbo wake WELL FED SLAVE OR HUNGRY FREE MAN unadhihirisha haya. Usikilize hapa chini
 

Na mwisho labda nigusie ile "dhana" ambayo nimeisikia mara kadhaa ya "kubusu chura akageuka mwana mfalme". Ni dhana kama ilivyo dhana nyingine. Lakini katika wimbo wake wa KISS NO FROG, Lucky Dube anaelezea namna ambavyo binti alijitahidi kumuiga mamake kila kitu, akawa na karibu kila kitu kasoro bwana amfaaye. Akasikia kuhusu hiyo "fairytale" kuwa ukim'busu chura atageuka mwana mfalme avutiaye. Lakini kajaribu tena na tena na tena bila mafanikio na ndiopo "alipojipata mwenyewe" na kutambua kuwa hastahili hilo. Na ndipo alipoweka dhamiri kuwa HATABUSU CHURA TENA.
Chura aweza kuwa chochote maishani. Anaweza kuwa kazi yako ama mambo mengi unayojitahidi kuyafanya bila mafanikio na ambayo unaamini ni chanzo cha furaha kwako (kama binti huyu alivyoamin) lakini akaja kugundua kuwa "better be alone and be happy than be with someone and be unhappy" WAZAMsikilize hapa chini akisema KISS NO FROG. Aliwaza nini kutunga hivi??
 

Lyrics zake waweza zifuatilia HAPA
Ninalowaza na kupongeza ni namna anavyoweza kutumia matani, mizaha na akili za kusadiki katika kueleza UJUMBE HALISI alionao.
Binafsi ntamkumbuka saana kwa kazi alizofanya na wengi watanufaika na hazina kuubwa ya MAFUNZO NA UELEKEZI ndani ya nyimbo zake.
Na ndio maana GRAMPS wa Morgan Heritage aliamua (katika albamu yake ya kwanza kama msanii wa kujitegemea) kumuenzi Lucky Dube kwa kibao mwanana ALWAYS & FOREVER.
Kisikilize hapa chini
 

Shukrani za pekee kwa Da' Mkubwa Subi kwa kufanikisha kupatikana kwa wimbo Always and Forever

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

1 comment:

Halil Mnzava said...

Safi sana,walau nimejikumbusha Luck Dube.