Saturday, October 13, 2012

Miaka mitatu, siku tatu.......na hawa watatu

Ni miaka mitatu sasa tangu niwe Baba kwa mara ya kwanza. Well! Tang tuwe wazazi kwa mara ya kwanza
Yaani ni siku ya kwanza tangu tulipomtwaa mwanetu wa kwanza Paulina siku kama ya leo mwaka 2009.
Na pia ni siku ya tatu tangu tulipobarikiwa kupata binti wa pili Annalisa aliyezaliwa Oktoba 10,2012.

Mpaka sasa "Da'Mkubwa" anaonekana kufurahia ujio wa mchukua "attention" yake (japo sina hakika hii itakuwa kwa muda gani).
Lakini furaha na baraka zote za kuwa na hawa wapendwa katika familia zinaambatana na SHUKRANI kwa wengi.
Zaidi kwa Mwenyezi Mungu aliye muweza wa kila nikiaminicho.
Safari zote hizi hazikuwa nyororo na wala sikutegemea ziwe hivyo, lakini kuna mengi mema niliyookoteza njiani. Na la kwanza (ambalo si siri) ni UJASIRI WA MAMA YAO. Kwangu.......NAMSHUKURU MUNGU KWA UWEPO WAKE.
Shukrani pia kwa Wazazi wetu, walezi, ndugu jamaa na marafiki ambao wamekuwa nasi kila uchao katika safari hii wakitupa moyo na kutuimarisha pale ambapo imani ilianza kuyumba kidogo.
Hakuna lolote ninaloweza kusema likaweza kuwa sawa na namna ninavyothamini uwepo wa wote waliounga mkono na kuamini ukamilifu wetu katika hili, na hata wale ambao walitupa changamoto kwa kuamini kuwa tusingeweza.
Photo Credits: SFAppeal
Hawa walitulazimisha kujifunza zaidi, kujizatiti zaidi na kuhakikisha kuwa tunaondoa hofu zao.
NA KWA KUFANYA HIVYO, TUMEKUA ZAIDI.
Yote juu ya yote, uwepo wa HAWA WATATU umekuwa chanzo cha furaha kwangu. Kuwaona nirejeapo nyumbani toka kazini ni sababu tosha kurejesha tabasamu ambalo wakati mwingine hupotezwa na watu wenye fikra "kandamizi" kazini.
Ni furaha hii ya MWISHO WA SIKU inayofuta fikra za mahangaiko na mateso yaliyokuwepo katika miaka yote mitatu, siku tatu na yaliyohusisha HAWA WATATU.
Lakini mara zote nilifarijika kwa kumsikiliza mwanamuziki Darius Rucker alipoimba "It won't be like this for long. One day we'll look back laughing at the week we brought her home. This phase is gonna fly by, so baby, just hold on. It won't be like this for long"
Happy EARTHDAY Paulina. Karibu Annalisa. Asante Mama watoto wangu.
NIUSIKIAPO WIMBO HUU, NAFARIJIKA

5 comments:

Albert Kissima said...

Hongereni sana. baraka tele kwenu, nawatakia maisha mema yenye amani, upendo, furaha na mafanikio tele.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana tena sana na mwenyezi mungu awazidishie upendo na amani siku zote. kama sikosei pia leo ni siku yake Paulina..Hongera Pau..na karibu sana Analisa..Mungu uzidi kuwapa nguvu wazazi hawa wawili.

Subi Nukta said...

Pongezi kwa ujio mpya kwenye familia. Mungu aendelee kuwa baraka yenu.
Heri kwa sikukuu ya kuzaliwa, Paulina.
Namtakia Mama watoto afya njema ya kipindi hiki cha kujifungua na uzazi, naitakia familia nzima afya njema pia!

Jestina George said...

Wow what a good news, kweli Mungu ni mkubwa na wakushukuriwa daima. many congrats to you my brother, my wifi and my lili beautiful princess Pau on the arrival of baby sister Annalisa. God bless.

Mija Shija Sayi said...

Japo nimechelewa lakini hongereni saaaaaaana...

Mungu awazidishie kila lililo la baraka katika kuwalea watoto hawa..