Nimesema saana juu ya Nasio. Mmoja kati ya "darubini" kali za maisha ya wengi kupitia muziki halisi wa Reggae. Na japo nilimzungumzia wiki iliyopita, basi hapa ninaye tena katika kibao hiki TRUTH WILL REVEAL kutoka albamu yake ya Revolution.
Umati mkubwa nyakati za kampeni. Ukitaka kujua wawazalo juu ya mgombea, angalia matokeo. Kama unabisha muulize Mrema (1995)Kwa hapa Marekani tumeona namna ambavyo uchaguzi wa mwaka huu umegeuka kuwa funzo kwa wengi.
Kuwaonesha kuwa MABADILIKO yajapo hayazuiwi kwa vitisho wala mtazamo wa mtu. Watu walipiga kura za maoni kwa namna ya kuweka uwiano na wengine hata kutopiga kabisa ilhali wakijua walichonacho mioyoni mwao.
Hilo liliwapa watu mtazamo kuwa uchaguzi ungekuwa mgumu kiasi na wengine kubashiri mambo kugeuka siku ya mwisho kulingana na "enthusiasm" waliyokuwa wakiiona kwenye kampeni zao. Walilosahau ni hilo lililoimbwa na Nasio ambalo pia nimeliandika hapo juu.
Wanadanganywa na sura bila kujua mawazo, na kuangalia matendo bila kujua madhara yake na wakati unapofika kila mtu akafanya kilichokuwa mioyoni na UKWELI UTADHIHIRIKA kiasi hata cha kuwashangaza walioshindwa.
NASIO ALIKUWA NA BADO YUKO SAHIHI.
Tusubiri usiku wa leo kujua, ni umati gani ulioshangilia na kisha kwenda kupiga kura?
1 comment:
Inanipa faraja sana na kusema `kwanini sisi hatuwezi hili' ni pale wanaposimama pamoja kwenye midahalo.
Post a Comment