Sunday, March 10, 2013

KENYA: Kwanini nafurahia kushindwa kushinda kwa walioshindwa?

Photo credit: GVLN Rao blog
JIRANI, RAFIKI NA NDUGU ZETU WA KENYA WAMEMALIZA UCHAGUZI WAO MKUU.
Ukweli ni kuwa, katika uchaguzi huu, MSHINDI WA KWELI NI MWANANCHI WA KENYA.
Nani asiyekumbuka msuguano uliotokea katika uchaguzi uliopita?
Nani asiyekumbuka kampeni zilizofuatiliwa kwa kila kauli?
Nani asiyekumbuka VIJEMBE vilivyotawala kampeni?
Nani asiyekumbuka USHINDANI MKUBWA uliokuwepo katika uchaguzi?
YOTE YAMEPITA NA WOTE WAMESHINDA. WALIOSHINDA KUSHINDA NA WALIOSHINDA KUSHINDWA.
Lakini pia tulijua tangu awali kuwa kati ya wagombea 8 waliokuwa wakigombea urais, kulilazimika kuwa na mshindi mmoja. Hii lingetokea hata kama uchaguzi ungerudiwa mara kumi.
 
SASA TUYAGEUKIE MATOKEO
FALSAFA YA MATOKEO (ALIYESHINDA NA ALIYESHINDWA) NI SAWA NA ILE YA MLIMA NA BONDE
Nani asiyejua kuwa "mwanzo halisi wa mlima ni mwisho halisi wa bonde"?
Ama ni nani anayesahau kuwa furaha ya sasa ni akiba ya huzuni ijayo?
Na kuna aliyesahau kuwa huzuni ya sasa ni akiba ya furaha ijayo?
Basi kwa "MANTIKI" hiyo hiyo.... kuna mengi ya kufurahia kwa wale walioshindwa kushinda nchini Kenya.
Kuna mengi ya kujifunza na kuna mengi ya kusahihisha.
Wale wachache walioweza kuweka hisia zao wazi, wamesema kuwa kuna mengi mema na mabaya waliyojifunza.
Wamejifunza kuhusu KUTOAMINI MFUMO na wengine kujua UNAFIKI WA WANANCHI.
Wapo waliojifunza kuhusu namna ambavyo mwananchi anaweka DEMOKRASIA yao kando na kuridhisha matumbo na haja zao za wakati huu.
Ina maana, kuna walilojifunza
Kwa maana nyingine, ni kwamba ili walioshindwa sasa wahakikishe kuwa wanafanikiwa baadae, kuna ulazima wa waliofanikiwa sasa kushindwa baadae.
Na pengine, namna pekee ya wale walioshinda kwa njia zisizo halali kukosa nafasi hizi kihalali, basi kuna haja ya kuhakikisha MFUMO UNAREKEBISHWA NA JAMII INAELIMISHWA.
Ina maana, naamini kuwa KAMA WALIOSHINDA KUSHINDWA AMA KUSHINDWA KUSHINDA WANA UCHUNGU NA KENYA KAMA WALIVYOSEMA, BASI KAMPENI YA KUIELIMISHA RAIA ITAENDELEA MPAKA UCHAGUZI UJAO.
Sasa ni kwanini NIMEFURAHIA "kushindwa kushinda kwa walioshindwa"?
1: Kuna mengi waliyojifunza kuhusu uchaguzi.
2: Kuna mambo mema yatakayoongezeka ifikapo uchaguzi ujao.
3:  Kuna DHIHIRISHO KUWA AMANI YAWEZEKANA na tunasonga mbele.
Baada ya vurugu za uchaguzi uliopita, Umoja wa Mataifa ulimuomba Winston Rodney almaarufu Burning Spear kwenda kufanya ONYESHO LA AMANI nchini Kenya.
Burning, ambaye amechukua jina hilo kwa heshima ya rais wa kwanza wa Kenya huru Mzee Jomo Kenyatta, alifanya moja ya maonyesho makubwa yaliyoshirikisha watu wa makabila yote yaliyohasimiana na hakukuwa na tukio la vurugu.
Aliporejea toka Kenya, akatunga wimbo ONE AFRICA ambamo anasisitiza kuwa "ONLY IF YOU COME TOGETHER IS WHEN YOU CAN GET MORE THAN WAHAT YOU'VE LOST"
Naamini, iwapo wale wote walioshindwa katika uchaguzi huu wataungana kuimarisha KUREKEBISHA KWA NJIA ZA HALI yale yaliyowasababishia kushindwa, naamini uchaguzi ujao utakuwa wa MAFANIKIO ZAIDI
PamoJAH

JICHO LA NDANI ni kipengele kinachozungumzia mambo mepesi na yaliyo ndani mwetu, ambayo yakiangaliwa vema na kwa tafsiri ama tafakari njema yanaweza ama ndio suluhisho kwa matatizo yetu. Kwa matoleo yaliyopita katika kipengele hiki, BOFYA HAPA

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

mmmhhh!!

emuthree said...

Mkuu niwaza sana hilo, ndipo nikaja na wazo hili kuwa mwenzako akinyolewa na weye tia maji kichwa chako!