Thursday, March 14, 2013

Ya Lwakatare na VIDEO YAKE........MSHINDI AWE MTANZANIA

Hivi karibuni kumetolewa VIDEO HII HAPA (na chini) ambayo kwa hakika imezua tafrani kwa jamii nzima.
Katika mijadala mingi iliyoibuka kuhusiana na video hiyo, yaonekana watu wamesahau kuhusu TANZANIA na mjadala umehamia kwenye mchuano kati ya wafuasi waaminiyo SERIKALI YA CCM NA UPINZANI.
Lakini watu hawa wamesahau kuwa haijalishi kilichotokea mpaka sisi kuiona video hiyo,VIDEO HIYO NI HATARI KWA USALAMA WA TAIFA (katika hali iwayo yote)

Iwe imeghushiwa ama ni halisi, video hii INADHIHIRISHA TISHIO KATIKA USALAMA WA TAIFA
1: Kama imeghushiwa, ina maana taifa letu liko kwenye "ncha" ya machafuko toka kwa watu wenye vipaji vya kutengeneza video zilizo karibu na ukweli.
2: Kama ni ya kweli, basi taifa letu liko kwenye "ncha" ya kuingia katika IMANI ISIYO SAHIHI kuhusu yanayotokea na yanavyotokea.
Kinachonishangaza ni kuwa, badala ya kuweka MASLAHI YA TAIFA NA WANATAIFA MBELE, na kupambanua CHANZO CHA VIDEO HII ili kutumika kutoa ushahidi wa moja kati ya mambo mawili niliyozungumza, naona ITIKADI INATAWALA mijadala hii jambo ambalo si la manufaa hata kidogo.
Jamani...
Tuwe waTanzania kwanza.
Tujadili namna ya kupata suluhisho la TISHIO HILI LINALOTUKABILI.
Natumai tutaanza kuona ITIKADI ZIKIWEKWA KANDO NA KUANZA KUJADILI HATARI INAYOAMBATANA NA VIDEO HII.
Na kwa kufanya hivyo, MSHINDI ATAKUWA MTANZANIA na sio itikadi kwani tutakuwa tumepata CHANZO NA NIA YA VIDEO HII, NA HILO LITAEPUSHA HATARI INAYOLIKABILI TAIFA

Na huu ni MTAZAMO WANGU kwa namna nionavyo tatizo.
Labda namna nionavyo tatizo ndio tatizo.


"POLITICS FIX" ni kipengele kinachozungumzia mambo ambayo blogu hii inaamini yanastahili kuwekwa vema katika siasa za nyumbani Tanzania, ama zinazoathiri Tanzania. Kusoma matoleo yaliyopita katika kipengele hiki BOFYA HAPA

No comments: