Tuesday, April 30, 2013

Ana kwa Ana na msanii Bi Salma Moshi



Karibu katika mahojiano haya na mmoja wa wasanii wakongwe nchini Tanzania, ambaye pia ndiye msanii wa kwanza wa kike kucheza na nyoka Bi Salma Moshi.
Katika mahojiano haya, Bi Salma anaeleza mambo mbalimbali yakiwemo..
1: Historia yake katika sanaa?
2: Uhusiano na ushindani uliokuwepo kati ya kundi lake na makundi mengine?
3: Alijiingiza vipi kwenye kucheza na nyoka?
4: Ni nini unachotakiwa kufahamu kabla hujaanza kucheza na nyoka?
5: Ni kweli kuwa sanaa ya kucheza na nyoka huushisha ushirikina?
6: Ni kweli kuwa alikuwa akiishi na wale chatu nyumbani kwake?
7: Ni kwanini sanaa za jukwaani hvutia zaidi watu toka nje ya nchi?
8: Kama ni kweli kuwa soko kubwa la muziki wa asili liko nje ya nchi, kwanini wasanii wake hawapato shows nje ya nchi?
9: Ni kipi kinasababisha maisha duni kwa wasanii mambali nchini?
Na mengine mengi
KARIBU UUNGANE NASI

Tuesday, April 23, 2013

Kijiwe cha Ughaibuni.....VIJIMAMBO

Hi ni sehemu ya 19 ya kipindi hiki kiletwacho na blog ya VIJIMAMBO.
 Sikiliza. Uburudike, uelimike na kuhabarika.

Sunday, April 21, 2013

Wana-Diaspora....Tuwafunze watoto wetu Kiswahili

Hivi karibuni, Jumuiya ya waTanzania hapa DMV imeanzisha madarasa ya kiSwahili kwa watoto.
Mkakati huo ni muenedelezo wa kusaidia kukuza lugha kwa watoto waliozaliwa ama kukulia huku.

Katika hili, mwanaharakati Abou Shatry wa SWAHILIVILLA BLOG alianza kuandaa madarasa kwa njia ya video ili kuwezesha kuelewa kwa urahisi.
Hapa, ameanza kwa kutengeneza video ya majaribio inayoonyesha baadhi ya Wanyama na Ndege na anakaribisha maoni ya namna ya kuboresha mkakati huu.

Ni jambo jema na la kujivunia kuona idadi kubwa ya watoto wakihudhuria madarasa haya, jambo linaloonyesha mwamko wa wazazi kuwafunza watoto lugha yao ya asili Madarasa haya yamegawanywa katika makundi kulingana na mahitaji ya watoto na yanaendelea kila Jumamosi

Baadhi ya watoto waliohudhuria darasa hili la watoto la kiswahili kama walivyonaswa na kamera ya Blogu ya Vijimambo

Saturday, April 20, 2013

Ana kwa Ana na Mhe. Leticia Nyerere


Karibu katika mahojiano kati ya Jamii Production na Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Leticia Nyerere.
Yeye ni Mjumbe wa kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Katika mahojiano haya yaliyofanyika Machi 15, 2013, Mhe. Nyerere amezungumzia mambo mengi ikiwemo
1: Historia ya maisha yake
2: Wajibu wa mbunge wa viti maalum
3: Ushirikiano wa wabunge wanawake katika kumkomboa mwanamke
4: Utata wa uraia wa nchi mbili
Pia mtazamo wake katika Mchakato wa katiba mpya, uongozi wa majimbo Tanzania, kutenganisha chaguzi za Rais na Wabunge, kuwa na mabunge mawili nchini, mchakato wa kuwapata wabunge wa viti maalum, na mengine mengi
Karibu uungane nasi

Friday, April 19, 2013

Ana kwa Ana na Nape Nnauye....Mwaka mmoja baadae


Mwishoni mwa mwaka 2011, nilibahatika kupata fursa fupi ya kuketi na kuhojiana na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Nape Nnauye. Alikuwa nchini kwa ziara fupi ya kikazi na pia alikutana na wanachama wa matawi ya CCM hapa nchiniTulijadili mambo machache tofauti kuhusu chama anachoongoza na migogoro iliyomo ndani mwake.
MWAKA MMOJA TANGU TUHOJIANE...UNAONA MABADILIKO?
Karibu kusikiliza mahojiano yetu hapa chini

Friday, April 12, 2013

Ana kwa Ana ya SwahiliTv na Bwn. Rahim Kangezi


Hivi karibuni, Swahilili TV ya hapa DMV ilipata fursa ya kufanya mahojiano na mmiliki wa timu ya African Lyon Tanzania Bwn. Rahim Kangezi
Katika mahojiano haya, Bwn. Kangezi ameeleza mengi kuhusu harakati zake kufikia hapa na hata kutoa ushauri kwa waTanzania wengi (hasa walio nje ya nchi) kuhusu WAJIBU wetu katika kuendelezana na kuiendeleza nchi.
UNGANA NAO

Monday, April 8, 2013

CHINA IS MORALLY BANKRUPT!!.... ALL THEY NEED IS OIL AND MINERALS

By Liberatus Mwangombe “Libe”
 To my fellow Africans and Tanzanians who praise and give China credit for building a coalition with African nations.  The Chinese government doesn’t care about you – their intentions are not transparent, they do not care about human rights, and corruption is as natural to them as breathing.  Even if no one else will tell you what China’s true motivation is, I will.  They need our natural resources such as oil and minerals.

            I wonder if President, Jakaya Mrisho kikwete, considers the ultimate impact on Tanzania from forming trade alliances with China.  Through my personal research I have found historical facts that reveal significant growth in the volume of trading between Tanzania and China.  In 1997 Tanzania’s total export of goods and services to China was Tsh 10 billion.  In the same year, China’s export of goods and services to Tanzania was Tsh 37 billion.  In 2005, a mere 8 years later, these two countries exchanged goods and services worth Tsh 347 billion! Tanzania’s exports represented Sh 101 billion of the total and China’s exports represented Sh 245 billon, more than twice that of Tanzania! (The Citizen, March 2013)

            The numbers in 2005 already suggest a Tanzanian dependence on China’s goods and services.  In addition, in 2009 the divide widened even further when Chinese President, Hu Jintao, met with Tanzanian President, Jakaya Mrisho Kikwete and trading was at Tsh 1.37 trillion between the two countries, again, disproportionately!  History demonstrates that China has never been a genuine trading partner since they have slowly widened the gap to form a reliable source of income for themselves by providing largely low quality goods and services at inflated prices.  As of 2011 the export value between the two countries was at Tsh 2.28 trillion!!  I don’t have to tell you which country has the lion’s share of that Tsh 2.28 trillion.

Wito kwa Vijana Wote Watanzania- Zamu Yetu Kuliongoza Taifa Imefika


The Kilian Kamota’s Call to All Tanzanian Youth: Our Turn to Lead the Nation is Now.
By Kilian Muya Kamota


The task is ours, the Tanzanian youth, to decide the future and the fate of our Nation. Our fathers, the first generation of leaders, have done their part; they fought political colonialism and afforded us the political independence. The time has come for them to pass on the torch to us, so we can fight for socio-economic independence. We must show up, accept the torch and lead our Nation into new horizons. The future of Tanzania is in our hands – the Tanzanian youth. This is the task we cannot ignore; this is the task we cannot pass to someone else. It is our task, it is our duty. The question is what are we going to do about it? Are we going to show up for this noble task? Are we going to report for duty? Or are we going to let our Nation stray into wilderness and chaos without leadership? Are we going to decide the fate of our own future or are we going to let few politicians decide our fate and our future?

Our fathers – the first generation of leaders – have grown old. Their actions and leadership can attest to that. The time has come for them to pass on the torch and for us to take the realm. Let us help them retire in peace as we take over the noble task of leading our nation.

Letter to the First Generation of Leaders – Good Bye and Good Luck
On behalf of all Tanzanian youths’, i wish to express sincere gratitude to our fathers – the first generation of leaders – for all the hard work and dedication to our Nation. Your hard work and efforts is truly appreciated, it will not be forgotten and will not perish in vain. We will always cherish all that you were able [and not able] to achieve. And to that end, we want to wish you good health and good luck as you retire in peace. Please take on your new task of advising the new generation and

To Read more click here


Monday, April 1, 2013

Umemshukuru ama kumuombea ADUI yako?


Ndioooo!!!
Nauliza kama umeshamshukuru adui yako. Lakini kwanza adui yako ni nani?
Na anakufanya wewe uweje? Jasiri? Ujitegemee? Utambue upande wa pili wa binadamu wengine? Uwe na maamuzi ya haraka na yenye kukulinda wewe? Kufikiria namna ya kutoanguka aamuapo kufanya jambo kwako? Ama afanyaye lipi?
Lakini yote haya si yana umuhimu kwako? Yaani ukishajiandaa hivyo halafu akafa leo, akianza kutokea mwingine hudhani kuwa utaweza kumkabili kabla hajafikia kiwago cha uharibifu? Wewe waonaje?
Na kumbuka si lazima uone nionavyo mimi maana NAMNA UONAVYO TATIZO NDILO TATIZO.
Lakini niliandika kwa Kaka Bwaya kuwa kila mtu ana nafasi na wakati mwimngine wahitaji mawazo ya kweli ya wale wakuchukiao kuweza kujengeka zaidi. Bwaya tena alishauliza juu ya akusifiaye na akukosoaye na pale pia tukasema kuwa kusifiwa na kukosolewa vyote vyaweza kukujenga ama kukubomoa kulingana na mtazamo wako.
Rudisha fikra nyuma kisha utazame ni wangapi walisema huwezi kufanya hiki na ukasema unaweza na kwa kuwadhihirishia kuwa unaweza ukajifunza meeengi sana ambayo pengine usingeyajua kama si kutumia njia uliyotumia kutaka kuwaonesha kuwa uko sahihi? Ni wangapi wametambua msimamo wako na ushujaa wako kwa kuwa tu umeweza kukabiliana na vikwazo fulani? Unajua kuwa ushujaa wa kweli hutokana na vikwazo?
Na unadhani vikwazo huletwa na nani? Si adui?
Basi adui ana nafasi gani katika maisha yako? Pengine vikwazo ndiyo "shehena" kubwa ya furaha unayoweza kuwa nayo mara uvipitapo.
Hebu sikiliza SHUHUDA mbalimbali zitolewazo na watu. Jinsi ulivyopita maisha magumu zaidi, ndivyo ushuhuda wako unavyokuwa na nguvu zaidi na ndivyo unavyowagusa wengi na kubadili mitazamo ya wengi wenye shida kama wewe. Nelson Mandela alinukuliwa akisema "The greatest glory in living lies not in never falling, but in rising everytime we fall" Hakuna ubishi katika hili. Lakini pia ni nani anayependa kuanguka? HAKUNA. Anayependa kusimama imara baada ya maanguko? KILA MTU.
Mmmmmhhhh!!
Na maanguko yapo na hatuwezi kuyakwepa, sasa kwanini tusiwe na mtazamo chanya wa kukabiliana na kuyapita haya? Kwanini tukae tukiwaza "kwanini limetokea" badala ya vipi ntajinasua na kuhakikisha sianguki tena? Tutakiwa kukubali changamoto kuwa kama twataka na twajua kuwa kuna maanguko na makwazo, basi lazima tuwe tayari kupita njia hizo kuyashinda na kuibuka washindi. TWATAKA MEDALI BILA KUSHINDANA? Nasio Fontaine alisema "harder the battle, tougher the fight, sweeter the victory" Nadhani yuko sahihi.
Peter Tosh alisema "everyone wants to go to heaven but nobody wants to die" aliposema mengi watu wapendayo lakini bila kutaka ama kujua njia sahihi za kupita kutapata katika wimbo wake Equal Rights.
SIWAPENDI MAADUI LAKINI SI KWELI KUWA HAWANA NAFASI KATIKA UKUAJI WETU. Na huu ni mtazamo wangu, na yawezekana Namna Nionavyo Tatizo Ndio Tatizo
Lucky Dube katika wimbo wake wa Celebrate Life alisema tunaishi na wendawazimu wengi wenye nia tofauti. Kwenye The One akasema usiwape nafasi ya kukwambia "hili haliwezekani" maana "neno hilo halipo kichwani mwa jasiri" Msikilize hapa katika Celebrate Life nawe uwe Jasiri


BLESSINGS
NB: Marejeo ya Dec 29, 2008