Tuesday, May 14, 2013

Hongera na Karibu Balozi Mulamula

Photo Credits: Sunday Shomari blog
Katika taarifa yake ya leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kujaza nafasi za mabalozi wa Tanzania katika nchi za Marekani na Falme za kiarabu.
Mmoja wao
Rais Jakaya Kikwete ameteua mabalozi ili kujaza nafasi zilizo wazi nchini Marekani na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule, Rais Kikwete amemteua Balozi Bi. Liberata Rutageruka Mulamula (pichani juu) kuwa balozi wa Tanzania nchini Marekani (Washington D.C.) kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe Balozi Mwanaidi Maajar aliyemaliza muda wake.
Balozi Mulamula, ambaye anakuwa Balozi wa pili wa kike nchini Marekani ni Msaidizi wa Rais Mwandamizi katika masuala ya kidiplomasia na aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa kwanza kuiongoza Sekretarieti ya Nchi za Maziwa Makuu kwa kipindi cha miaka minne kuanzia Januari, 2007 hadi Desemba, 2010.
Pia, Rais Kikwete amemteua Balozi Bw. Mbarouk Nassor Mbarouk kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu. Hadi uteuzi huu unafanyika, Bw. Mbarouk alikuwa Afisa Mwandamizi katika ubalozi wa Tanzania nchini Urusi (Moscow).


No comments: