Wednesday, May 15, 2013

Thaminisha.......Mr & Mrs Abdallah Kitwara

Photo Credits:  Vijimambo blog
Nawasikia(ga) tu wakisema "nyuma ya mafanikio ya mwanaume, kuna juhudi za mwanamke"
Labda ni kweli..
Lakini pia, kuna UKWELI kuwa huyo MWANAMUME yuko na huyo amuwezeshaye kwa kuwa naye amejitolea mengi kuweza kuwa naye.
Kwa hiyo, nyuma ya mafanikio ya kila mwanaume, kuna juhudi za mwanamke ambaye alichaguliwa, kukubaliwa na / ama kuendelea kuwa na mwanaume aliyenaye.
Labda....NYUMA YA MAFANIKIO YA KILA MTU, YUKO MTU.
Kwanini nimeanza na nukuu hiyo?
Ni kwa kuwa nataka ku THAMINIsha Kaka yangu Abdallah Kitwara na mkewe.
Hawa wamekuwa chachu ya maendeleo ambayo binbafsi NIMESHUHUDIA na pia NINAYAISHI.
Kabla sijatambulishwa kwake na mwenzangu katika kazi (Abou Shatry), nilipata kujua USHIRIKI wake kwenye jamii kwa kuona UDHAMINI wake kwenye timu ya Tanzania DMV
Jezi za timu zilizodhaminiwa na kampuni ya Vizion One Inc inayomilikiwa na Mr & Mrs Kitwara.
Baada ya kumuona katika hili, tuliwasiliana nao kuangalia namna ambavyo wangeweza kuwa na ushirika katika harakati zetu za kukuza mkakati wetu wa kuanza kufanya uzalishaji wa AUDIO na VIDEO kwa matukio yanayotukia hapa Washington DC na vitongoji vyake.
Tulipowasiliana nao, walikuwa wakarimu sana kutualika kwao na kisha WALITUWEZESHA KUPATA VIFAA VYA KISASA NA VYA KUTOSHA KUFANYA KAZI ZETU.
Huu ulikuwa ni zaidi ya msaada.
Hii ilikuwa zaidi ya baraka
Hili ni zaidi ya DENI LA KUSONGA MBELE
Hili walilotenda wapendwa hawa ni zaidi ya ambalo tulitegemea na baada ya kukamilisha manunuzi, tukapata (pamoja na mambo mengine) kamera ya kisasa saana
Mpiga picha mkuu wa Jamii Production Abou Shatry
Ni kwa uwezeshwaji wa wapendwa hawa, tukaweza kuanzisha JAMII PRODUCTION ambayo imejikita katika kuhakikisha inaELIMISHA, BURUDISHA na KUKOMBOA JAMII kwa mahojiano, mijadala na mambo mbalimbali
  
Ukweli ni kuwa, hapa tulipo tusingefika kwa wakati huu bila kuwezeshwa na ndugu hawa wawili.
Na si sisi pekee ambao tunajivunia nafasi yao katika jamii. Bado tumeona udhamini wao katika matukio mbalimbali ya jamii.
Mkurugenzi wa Vizion One, Abdallah Kitwara akimkabidhi Dj Luke cheki ya kusaidia matayarisho ya sherehe ya Blog ya Vijimambo itakayofanyika July 6, 2013 maeneo ya Capitol Heights, Maryland.
 Photo Credits: Vijimambo blog
Nikirejea kwenye mwanzo wa post hii, labda ni kweli kuwa mafanikio ya kila mmoja yametokana na ushirikiano wa kila mmoja wao, na kwa hakika napenda kuwaTHAMINISHA Mr & Mrs Abdallah Kitwara kwa nafasi yao katika jamii.
June 7, 2010 niliandika post hii isemayo UTAKUMBUKWA KWA DESHI YA MAISHA YAKO ambapo kati ya niliyosema ni kuwa "Maisha yana hatua tatu muhimu na mbili kati ya hizo (KUZALIWA na KUFA) hazina mjadala, na moja ambayo ndiyo tusiyoijua, ndiyo muhimu kwetu. Ndio hiyo niitayo "deshi". Na kwa kuwa kila mtu anazipitia mbili nilizozitaja, basi hakuna anayezijali wala kumkumbuka mtu kwazo. Ina maana maisha yetu yamebaki kwenye hiyo hatua iliyo kati ambayo ndiyo tunayoihangaikia..... 
......Leo hii kila aitwaye shujaa ama fisadi ama mshkiliza rekodi, ama mtakatifu ama mkatili ama mwenye cheo chochote ulimwenguni anakumbukwa kwa kile alichofanya kwa muda wake wa "deshi" ambao ni wa katikati ya kuzaliwa na kufa. 
Basi tuchuje vema maisha yetu na kuangalia na kutambua kuwa kwa kila utendalo sasa ndilo lenye kuweka historia yako mbeleni."
UKWELI NI KUWA...
Najivunia namna ambavyo Ndugu zangu hawa wamewezesha maisha ya wengi
Nami nawatakia baraka katika maisha haya ambayo punde mmesherehekea miaka kumi ya ndoa pamoja
Video hii iliyo muhtasari wa sherehe yao kuadhimisha miaka kumi ya ndoa ni kwa hisani ya IskaJoJoPhotography 


Kwangu na kwa jamii ijuayo mema, nyinyi ni HEROs
Na wimbo huu hapa chini, ni maalum kwa ajili yenu

**THAMINISHA ni kipengele kinachounganisha makala ama matoleo mbalimbali ya watu mbalimbali wanaojitolea kuboresha maisha ya wengine na hata wale wanaoona vema kuthaminisha yale waliyotendewa na wengine. Kwa matoleo zaidi BOFYA HAPA**

1 comment:

emuthree said...

Mkuu, sina cha kuongeza, maana naweza kupaka matope, kwenye nguo safi, cha zaidi tu nikuwapa hongera walengwa kwenye hoja hii, na kukuambia weye kuwa tupo pamoja