Wednesday, May 8, 2013

Ya Lwakatare na "kesi ya ugaidi"....kuna la kujifunza

Leo tumepata habari za kufutwa mashitaka ya uGAIDI yaliyokuwa yakimkabili kiongozi mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Bwn Wilfred Lwakatare.

Lakini hili (la kushutumiwa kwa kesi kubwa kisha ikaishia "hewani" bila maelezo kamili ya kwanini ilianza na / ama imeishia ilivyoisha) halijaanza kwenye kesi hii ya Bwn Lwakatare pekee.
Tulishaiona kwenyebaadhi ya kesi zilizovuma nchini Tanzania
Kesi kama ya Babu Seya, ya Zombe, ya Balozi Mahalu nk
TATIZO ninaloliona ni kuwa, hakuna anayewajibiswa kwa MAKOSA YA KESI HIZI.
Kinachotokea ni kuwa KESI INAJENGWA KWA (kile nilichofafanuliwa kama) PROBABLE CAUSES kisha inashindiliwa kwa mmoja na huyo AKICHOMOKA basi kesi imekwisha (at least machoni mwa waTanzania waliofanywa kuifuatilia).
Ama kinyume chake huwa sahihi..
Kwamba KESI INAJENGWA KWA (hichohicho nilichotambulishwa kama) PROBABLE CAUSES kisha inashindiliwa kwa mmoja ambaye "hachomoki".
Kama kuna mamilioni yaliibiwa ubalozini kwenye kesi ya Balozi Mahalu, kama kuna uuaji ulifanyika kwenye kesi ya kina Zombe, kama kuna UGAIDI kama ulioelezwa na M'bunge aliyeonyesha karatasi ya ushahidi mahakamani (0:59)

NA BADO WASHUTUMIWA WAKASHINDWA KUTIWA HATIANI......HII INA MAANA WALIOTENDA MAKOSA HAYA WAKINGALI WANAPETA
Lakini pia.....
Vipi kuhusu wale ambao wanasota jela wakiomba DNA itumike na haitumiki ili TUWAHUKUMU KUKAA HUKO ama TUWAPOKEE MTAANI na kila upande uridhike?
Maswali haya si mapya kwangu hapa kibarazani...
Januari 2, 2010 niliandika...
"...Lakini ni kwanini tusifanye kitu kwa usahii kwa mara ya kwanza? Na kama kuna ambao ni watu huru huko magerezani (na kwa habari nilizokuwa nasikia kuhusu kubambikiziana keshi nina hakika wapo), ni kwa muda gani tutaendelea kuwashikilia? Na siku wakija kugundulika kuwa walifungwa kimakosa ni nania wa kubeba gharama za kuwafidia? James Bain sasa atalipwa $50,000 kwa kila mwaka aliokaa gerezani. Ina maana Jimbo la Florida litamlipa takribani dola milioni 1.75 muda mfupi ujao. Na hiyo ni kwa kuwa waendesha mashtaka walifanya makosa. Kama ulimwengu wetu wa Tanzania utabadilika (na naamini umeanza) na kupata watu watakaotetea haki za walio gerezani bila hatia, ni nani wa kulaumiwa? Ni vipi tupate mabilioni ya kukarabati nyumba za watendakazi wa serikali na tukose vifaa kama hivyo kuamua kesi muhimu kama hizo? Ni maisha mangapi yanawekwa pasipostahili kwa kuwa tu wenye dhamana hawajali HAKI NA USAWA wa wananchi wao?...."
REJEA HAPA KWA ARTICLE KAMILI
Bado tatizo la uwajibishaji linakuja hapa ambapo tunashindwa kujua kuwa IWAPO KOSA LIMETENDEKA, KWANINI ASIPATIKANE WA KUWAJIBIKA NALO?
KUNA LA KUJIFUNZA

No comments: