Tuesday, July 23, 2013

VIDEO: Ukaribisho rasmi wa Balozi Liberata Mulamula Washington DC

Alhamis iliyopita (July 18, 2013), Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula alikabidhi nyaraka zake za utambulisho kwa rais wa Marekani Barack Obama.
Baada ya tendo hilo, Mhe. Balozi Mulamula aliandaliwa sherehe fupi ya kumkaribisha rasmi katika kituo chake cha kazi.
Sherehe hii iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa Ubalozini, pia ilihudhuriwa na mabalozi toka nchi za maziwa makuu, viongozi wa Jumuiya mbalimbali hapa jijini na pia waandishi wa habari.
Karibu utazame video hii hapa chini juu ya siku hii


Baada ya sherehe hii fupi, wenzetu wa SWAHILI TV walipata nafasi ya kufanya mahojiano mafupi ya "papo kwa hapo" na Mhe. Balozi

1 comment:

Ali Taufik said...

i like it conten for you blog amzing and radio station . thanks