Friday, August 9, 2013

Balozi Mulamula na Balozi Nyang'anyi washiriki sherehe za Idd na waTanzana wa DCAliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mustafa Nyang'anyi (kulia) akiwasili kwenye park ya Wheaton, Maryland kwenye sherehe ya Eid El Fitr iliyoadhimishwa Alhamisi Aug 8, 2013 baada ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani kuisha. Sherehe hii iliyoandaliwa na jumuiya ya Waislam waishio DMV, TAMCO pia ilihudhuriwa na Balozi wa sasa wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

Balozi mpya wa Tanzani nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akilakiwa na  Afisa Ubalozi Suleiman Saleh wakati anawasili kwenye sherehe za Idd El Fitr.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Mustafa Nyang'anyi, viongozi wa TAMCO na wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
Picha zote kwa hisani ya VIJIMAMBO BLOG

KWA PICHA ZAIDI, BOFYA READ MORE

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika Wheaton, Maryland, kulia ni Afisa Ubalozi Abbas Missana.

Balozi Liberata Mulamula akiongea Jambo na Balozi Mustafa Nyang'anyi.

Ustaadh akielezea maana ya mfungo wa Ramadhani wakati alipofungua rasmi sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika DMV iliyowajumuisha Watanzania wote waishio DMV na marafiki zao.
Mmoja ya viongozi wa TAMCO, Asha Nyang'anyi akiongea machache kwenye sherehe hiyo.

Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Mustafa Nyang'anyi akiongea machache kwenye sherehe hiyo ya Eid El Fitr iliyofanyika DMV huku akisisitiza umoja wa Watanzania ni kitu muhimu sana bila kujali itikadi zao, alisema amefurahi kukuta TAMCO aliyoianzisha wakati ule yeye akiwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani bado inaendelea kwa nguvu zote pia  Balozi Nyang;anyi alisisitiza Watanzania Waache majungu huku akisema kama mtu una jambo linakukera ni bora uliweke wazi kwani majungu hayajengi, pia aliendelea kwa kusema uwazi wa mapato na matumizi ni jambo kubwa kwenye jumuiya zetu lisipokuwa wazi Wanajumuiya hukosa imani na viongozi wao na hatima yake hufanya Jumuiya kulegalega na baadae kufa.
Mhe.Balozi Liberata Mulamula naye alisisitiza umoja wa Watanzania na kuimwagia sifa Jumuiya ya Waislamu DMV (TAMCO) kwa mshikamano walionao na jitihada zao za kuwaunganisha Watanzania wa DMV bila kujali itikadi za dini zao na kusema kwamba kuanzia jana yeye amejiunga rasmi na atakuwa mwanachama wa kudumu wa TAMCO pia aliwakumbusha enzi ya kidongo chekundu na Zanzibar sikukuu ya Eid ilivyokuwa ikisherehekewa pia alikabidhi Eid yake kwa Afisa Ubalozi Abbas Missana kwa ajili ya  watoto waliokuwepo kwenye sherehe hiyo.

Balozi Mulamula akichukua chakula kilichoandaliwa na Farida Catering.

Balozi Mustafa Nyang'anyi akijumuika na Watanzania wa DMV kwenye chakula cha Eid.

Baadhi ya Watanzania waliohudhuria sherehe ya Eid El Fitr.
Aunty Jasmine akimshukuru Balozi Mulamula kwa kukubali wito wa kujumuika nao japo ndio kwanza amekuja 
nchini Marekani pia alimshukuru Balozi Nyang'anyi na watu wote waliofika kwenye sherehe hiyo.

Juu na chini ni watoto wakicheza kwenye Moon Bounce


Mhe. Balozi katika picha ya pamoja na Viongozi wa TAMCO

No comments: