Tuesday, August 27, 2013

Mdogo mdogo......Tunakaribia. Asante kwenu

Ndio mwendo tuaminio watufaa...Mwendo usio na kasi.
Lengo ni kuhakikisha kuwa kila TUKANYAGAPO, haturejei kukanyaga (labda iwe nje ya uwezo wetu)
 Lakini pia...
Katika mwendo huu mdogomdogo, tunajifunza mambo mengi makubwa.
Nayo ni NGUVU NDOGO YA WENGI ambayo ina NGUVU kuliko NGUVU KUBWA YA WACHACHE.
Kuweza kufika hapa tulipo, imekuwa ni ushirikiano na wengi ambao wametuwezesha katika kile walichoamini kuwa ni KIDOGO kwao.
Walioona NIA na FAIDA ya kuWEKEZA katika wale waliowekeza kwa muda KATIKA JAMII.
Tumegundua kuwa kwa pamoja tunaweza kufika mbali iwapo kila mmoja atashikilia wajibu na talanta na uwezo wake katika kulileta pamoja WAZO MOJA....JAMII
Nasi sasa tunakaribia kukamilisha lengo hilo.
Tunakaribia kuwekeza zaidi katika kile tuaminicho kuwa ni muhimu zaidi kwetu...
KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KUKOMBOA FIKRA
Karibu
KARIBU KATIKA "JIKO" LA JAMII PRODUCTION.

JAMII PRODUCTION 
"USAHIHI WA FIKRA NDIO FIKRA SAHIHI"

1 comment:

MswahiliFlani said...

Asante kaka kwa kwakuliendeleza gurudumu la kuenzi fikra za waliopita na kumbukumbu kwa vizazi vijavyo sasa nimeamini ya kwamba Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi