Friday, August 9, 2013

Ni siku mpya kwangu. Mwaka mpya kwangu. Ni siku yangu. Asante kwako

Siku zinasonga na kwa hakika licha ya ugumu tupitiao, tukiangalia nyuma twaona kama jana tuu tulipokuwa tukicheza kama watoto.

Nami sasa nimetulia kuangalia maisha yangu yaliyopita katika siku hii ninayokumbuka kuzaliwa kwangu. Na ninajifunza mengi kwa kukumbuka mengi. Najua maisha yangu yasingekuwa yalivyo kama nisingezungukwa na watu niliozungukwa nao. Labda ningekuwa na watu tofauti ingekuwa zaidi ya hapa ama pungufu yake, lakini kwa sasa sina la kulaumu bali NASHUKURU KUWA NILIVYO.
Kwa hakika kuna wengi waliogusa maisha yangu ambao kwa namna moja ama nyingine wamebadili maisha yangu. Huwa nawafikiria saaana na mara kwa mara nimekuwa nikijaribu kuandika chini watu hao ili niweze kuwashukuru kwa pamoja lakini nimeshindwa. Tarehe 7 Aprili nilijaribu kwa mara ya mwisho kuwashukuru wote lakini nikashindwa na ndio chanzo cha kuandika kuwa HUWEZI KUWAHUKURU WOTE, WAOMBEE TUUU (Bofya hapa kusoma).
Kila mmoja ana nafasi ya pekee kwangu.
Kwa wanafamilia yangu sina la kusema. Wakubwa mmekuwa mkinionesha njia kwa upendo na unyenyekevu na mara zote kunisaidia pale niangukapo na wale wadogo kwangu mmekuwa mkinitia moyo pale nilipoonekana kukosa wa kuwa upande wangu.
Shukrani kwenu.
Kwa wale tuliocheza wote, furaha tuliyokuwa nayo wakati huo ndio chanzo cha fikra za sasa. Tuliosoma wote, bila ninyi nisingeweza songa mbele kwani mlisaidia kwa namna kubwa saaana.
Wale niliofanya nao kazi na hawa tunaoendelea kufanya kazi ya kuielimisha jamii na zaidi wale wasomao hapa kusaidia kunielewa, NAWAPENDA SAAAANA.
Wale MARAFIKI ZANGU ambao tumekutana kwa namna mbalimbali na bado tunajaliana na kusaidiana....NAWATHAMINI SANA
Labda nitoe upendeleo kwa watu wanne.
Mmoja ambaye licha ya kuthamini mchango wake kwangu na kumuombea kila leo, bado nahitaji msaaada wa kuwasilaiana naye. Si mwingine bali ni Dada mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye niliandika habari ya kumtafuta HAPA (bofya kuisoma) na bado naendelea kusubiri mawasiliano naye.
Nirejee wa wanangu wapenzi....Paulina na Annalisa. Hawa wamekuwa stress busters kwangu.
Wamekuwa zaidi ya faraja pale nichokapo na pengine ni TASWIRA ya nini kinatakiwa kuendelea.
Mara kadhaa nilipofanya / kufanya UPUUZI, nawakumbuka ama kukumbushwa kuhusu hawa na hilo hurejesha fikra kuwa SIKO DUNIANI KWA AJILI YANGU TU.
Wazazi na walezi (wema) mwalielewa hili.
MWISHO NI SALAMU ZA UPENDO KWA WANGU Esther.
NAKUPENDA SAAANA, NAKUHESHIMU, NAKUTHAMINI NA NAPENDA UTAMBUE KUWA UWEPO NA USHIRIKIANO WAKO MAISHANI NI KATI YA VITU VYEMA NINAVYOJIVUNIA KATIKA MAISHA.
SINA LA ZIADA NINALOWEZA KUMUOMBA MUUMBA
Ni mwaka mpya Kwangu, Ni siku yangu na ASANTE KWAKO
THANK YOU LORD

No comments: