Sunday, October 13, 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA. Kutekwa kwa Waziri Mkuu wa Libya na kukamatwa kwa Al-Libi


Kutoka Tripoli nchini Libya....Watu wenye silaha mapema Alhamis walimteka na baadae kumuachia huru Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Zeidan juu ya kile ambacho waasi wamesema ni kuonyeshwa kukerwa na matatizo ya RUSHWA NA USALAMA katika nchi hiyo.
Hili linaonekana kutekelezwa kufuatia kukamatwa kwa mshukiwa wa kundi la kigaidi la AlQaeda Nazih Abdul-Hamed al-Ruqai, ambaye pia anafahamika kama Abu Anas al-Libi aliyekamatwa jumamosi iliyopita nchini Libya na makomandoo wa Marekani
Huu ni muendelezo wa taarifa tofauti na za kuchanganya tangu kukamatwa kwa Al-Libi
Ifuatayo ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 12, 2013

No comments: