Sunday, October 13, 2013

Kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production......FAMILIA ZA KAMBO

Photo Credits: Amy Urbach @ Runhers.com 
Pale familia zinapoamua kusonga mbele na maisha yanayohusisha watu zaidi ya waliokuwepo awali, mambo mengi hutokea. Kuna wakati ambao watoto huonekana kutokuwa tayari kupokea ujio wa watu wengine kwa kudhani watapoteza sehemu ya hadhi yao ndani ya nyumba (ama unaweza kusema wanakuwa na namna fulani ya wivu)
Lakini pia, hata wazazi wanaoingia katika maisha ya familia nyingine hushindwa kurekebisha mwenendo wao kuweza kuwafaa watoto wanaowakuta na matokeo yake kuleta namna ya kutoelewana baina yao.
Tunaweza kuangalia sababu mbalimbali zinazosababisha haya, na kunaweza kuwa na sababu nyingi zaidi ya tunazoweza kufikiria juu ya hili, lakini tunaamini kuwa yapo mambo ambayo kama tutayazingatia, yanaweza kutupa mwanga wa kuepuka hili.
Karibu katika kipindi hiki cha FAMILIA kutoka Jamii Production kinachokujia kila Jumatatu, ambapo katika kipindi hiki, tumeanza na sehemu ya kwanza ya mfululizo wa vipindi vyetu vitakavyozungumzia changamoto za FAMILIA ZA KUFIKIA.
Yaani, kuwa mzazi wa kufikia, ama wengine wanasema MZAZI WA KAMBO.
Je! Ilikuwaje zamani? Ikoje sasa na kubwa zaidi tutajaribu kuangalia...Je! ilistahili kuwaje?
Katika kujadili hili, tumeungana na wazazi kujadili mada hii, na pia kusoma makala za uchunguzi juu ya hili.
KARIBU
Mtayarishaji na Mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA, Georgina Lema akiwa na mgeni wake Mayor Mlima ndani ya studio wakati wa kipindi

Georgina Lema akiendesha kipindi. Pembeni ni "fundi mitambo" wake Mubelwa Bandio
 Georgina Lema akijadiliana jambo na msimamizi wa kipindi chake Abou Shatry kuhakikisha kila kitu kiko sawa kabla ya kipindi
 
Georgina Lema baada ya kipindi
Twawapenda...Tukutane juma lijalo katika muendelezo wa kipindi hiki kuhusu FAMILIA ZA KUFIKIA / FAMILIA ZA KAMBO

No comments: