Tuesday, August 18, 2009

Ni lini tutawaenzi WATU hawa?

Kama kuna ambalo hatujaweza kupiga hatua nchini Tanzania basi ni suala la KUVUMBUA, KUENDELEZA KUTHAMINI NA KUENZI VIPAJI MBALIMBALI ambavyo kwa namna moja ama nyingine vingeweza kuwa endelevu saana nchini mwetu.
Inasikitisha saana kuona wale ambao wanatumia muda na hekima zao nyingi kuwekeza katika taifa letu "hupotea" na kutosikika na pengine "kutokumbukwa" mpaka pale wanapoonwa na wasio na mamlaka na pengine wajibu wa kufanya hivyo. Na hapa nawazungumzia watu kama walimu, wauguzi, wanamuziki, watangazaji na wafanyakazi wengine wengi ambao kazi zao zaongozwa na wito kuliko malipo.
Na katika kuwathamini na kuwaenzi, nazungumzia kwa namna tofauti kulingana na kazi na mahitaji yao.
Kwa walimu na wauguzi sina hakika kama kuna asiyejua ama kusikia kilio chao. Hao wanalia kila iitwayo leo. Wanapata malipo yao kwa nyakati zisizo sahihi, wana mazingira magumu ya kazi na pengine kuwa kama "wamesahaulika" huku SERIKALI ikiendeleza danadana ya kufuatilia mawazo yao. Wanapostaafu UTUMISHI ULIOTUKUKA, wengine inawachukua zaidi ya nusu mwaka kufuatilia mafao yao tena toka mikoani na wengine wakiishi kwa gharama zao jijini. Naamini hata kwa kuwalipa kwa wakati HAKI ZAO ni sehemu kuu ya kuwaenzi.

Mmoja wa wale niwaheshimuo sana fanini na future Hall of Famer ktk utangazaji Bwn Charles Hillary akiwa kazini Picha toka Bongo Celebrity
Kwenye fani niipendayo ya Utangazaji nako ni shughuli. Wapo wachache ambao unaweza kuwasikiliza katika kipindi chochote na usikate tamaa. Watangazaji wanaoweza kubadilika na kufaa katika kusoma taarifa ya habari, kisha akasoma matangazo ya vifo akafanya kipindi cha muziki, akatangaza michezo na lililo kuu akafanya mahojiano ya moja kwa moja. Sasa hivi kuwa "watangazaji" wengi ambao wanavuma katika kipindi kimoja ama viwili na baada ya hapo ni kinyaa. Wapo wanaovuma wanaposoma habari na taarifa mbalimbali lakini unaposikia mahojiano yao unaweza kujiuliza kama walijiandaa. Sasa kuna mstari gani unaowatenganisha na wale ambao wana UWEZO halisi na waliotumikia kwa miaka nenda rudi kwa uadilifu na kutunza maadili ya kazi yao na KUTUVUTIA WENGI katika kazi hiyo? Ni lini TUTAWAWEKA katika kundi la HALL OF FAMERS kwa utangazaji nchini mwetu ili na wanaochipukia wapate kuangalia wanakoelekea? KAMA HAKUNA SIFA ZA KUTOFAUTISHA MCHELE NA CHUYA, BASI MCHELE NA CHUYA HAVINA TOFAUTI YA THAMANI NA UBORA. Kuna haja ya kuwaenzi walio bora.

Mkongwe Said Mabera. Picha toka Inawezekana Blog
Kwa upande wa wasanii (zaidi niseme wanamuziki) tumekuwa tukishuhudia namna ambavyo wamekuwa KAMA CHOMBO CHA STAREHE CHA SERIKALI (Bofya hapa kusoma) na wanapomaliza kazi zao hapa duniani na kutoweka, basi na mchango wao hubaki kukumbukwa na wachache. Serikali yenyewe kupitia "matawi" husika havijihusishi na kuweka kumbukumbu zao na matokeo yake HATUWATHAMINI KWA KUWA HATUWAJUI (Soma hapa). Ni matawi haya ya serikali (kama CHAMUDATA na BASATA) ambayo yangestahili kusimamia thamani ya wanamuziki hawa kwa kuwatengenezea kumbukumbu maalum na hata tuzo za heshima kama HALL OF FAME kwa fani mbalimbali.
Kutofanya haya, ndiko kunakoweka DHARAU katika fani. Tunaona namna ambavyo watu wanathaminisha waimbaji wa sasa na WANAMUZIKI ambao wamefanya mengi ya maana kwa jamii na hakuna KIPIMO chochote cha kuwalinganisha. Leo hii waimbaji "chipukizi" wanawekwa kwenye kundi moja na watu kama Mzee Said Mabera ambaye licha ya heshima katika utunzi na utumiaji ala za muziki lakini amekuwa mfano wa kuigwa kwa kutohamahama bendi (yuko na Msondo kwa zaidi ya miaka 35), kutoropoka hovyo kwenye vyombo vya habari (kama wafanyavyo wengi sasa hivi katika kujitafutia majina) na pia kuheshimu maadili ya kazi. Wapo wengine wachache kama hawa. lakini hawana KINACHOWATHAMINISHA toka kwa walezi wao (Baraza la Sanaa ama Chama cha muziki wa Dansi). Kuna haja ya kuwaenzi kwa kuwaweka katika kumbukumbu na kuwapa TUZO ZA HESHIMA kulingana na kazi yao nzito.
Binafsi ntaendelea kuwaenzi na kuwakumbusha wasiokumbuka namna ambavyo mmekuwa mstari wa mbele kuielimisha jamii licha ya kutoonekana kuenziwa kisahihi. Ni kama Beres Hammond anavyokumbuka enzi na kuwakumbuka wale waliomfanya atinge katika muziki alipowaimba katika wimbo wake makini ROCKAWAY.
PamoJAH Daima. PROFESA MATONDO ALIWAHI ANDIKA JUU YA HAYA HAPA. Bofya ujikumbushe

Chorus:
Oh Yeah
Oh I Miss Those Days Yes
I Miss Those Days Yeah
Remember The Songs
Used To Make You Rock Away
Those Were The Days
When Love Used To Reign , Hey
We Danced All Night To The Songs They Played
Weekend Come Again Do It Just The Same, Hey

Verse 1:

Now I Feel it To My Heart
Being Such A Golden Time Had to Part Yeas
Now There 's Hardly Any Safe Place Left To Go
Someone's Bound To Come Any Try To Spoil The Show, Oh Oh

Chorus:
Remember The Songs
Used To Make You Rock Away
Those Were The Days
When Love Used To Reign, Hey
We Danced All Night To The Songs They Played
Weekend Come Again Do It Just The Same, Hey


Verse 2:
Hail John Holt, Alton Ellis, Derloy Wilson, Dennis Brown, Hey Hey
Big Youth, Josey Wailes, Daddy Roy
Would Wake The Town Yeah
And You Had To Hold Your Woman Real Close
When Smokey Starts To Sing
Temptations, Marvin Gaye, Spinnners All The Way
Aretha Franklin, Patti Labelle Used To Make Me
Drift Away Play Stevie Play Sam Cooke Any Day Yeah
We Dance All Night To The Song They Play
Weekend Come Again Do It Just The Same Yeah
Right Now We Need A Brand New Start
People Everywhere Need More Music From The Heart
And If There Remain Such A Place That I Can go
Will Someone Tell Me Tell Me I love To Know

Chorus:
Remember The Songs
Used To Make You Rock Away
Those Were The Days
When Love Used To Reign, Hey
We Danced All Night To The Songs They Played
Weekend Come Again Do It Just The Same

Remember The Songs
Those Were The Days
When Love Used To Reign, Hey
We Danced All Night To The Songs They Played
Weekend Come Again Do It Just The Same

Remember The Nights
Remember The Songs
Used To Make You Rock Away
Those Were The Days
When Love Used To Reign, Hey
We Danced All Night To The Songs They Played
Weekend Come Again Do It Just The Same Hey
Remember The Songs

6 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hata kama ungekuwa na kipaji cha namna gani hakuna anayejali tena usije ukashangaa ndiyo ukaanza kutazamwa kama adui anayestahili kupigwa vita. Ndiyo sababu wengi wanakata tamaa na kutimkia nje ambako vipaji vyao vinathaminiwa na kutuzwa. Niliwahi pia kulalamika kidogo kuhusu suala hili hapa: http://matondo.blogspot.com/2009/04/vijana-wetu-watundu-tunawasaidiaje.html

Si vibaya tukianzisha "Holywood Walk of Fame" yetu pale Mnazi Mmoja. Ndhani tunao "ma-celebrity" wa kutosha

Fadhy Mtanga said...

Tena tunao wa kutosha sana.

Yasinta Ngonyani said...

Naoma waliotangaulia wamesema yote. Ila kweli inasikitisha sana tena sana. Ni wazo zuri Prof. Masangu kwanini tusifanye hivyo? Tupo pamoja na tutafanikiwa tu.

Nicky Mwangoka said...

Yaani hatujali kabisa, cheki wenzetu wanavyomkumbuka Bob Marley, halafu nasi tunawaiga inapofika siku ya kumkumbuka na sisi tumo

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tatizo ni kwa sisi wenye vipaji wenyewe, hatujiamini na tunatarajiwa kusaidiwa na wasiojua vipaji vyetu vikoje.

kuna wakati unashindwa kujua kipaji fulani kikoje isipokuwa mwenye nacho ndiye ajuaye kwa hiyo yatubidi kuwa wabunifu sisi wenyewe jinsi ya kuvifanyia kazi.

kama zecomedy, walipiga hatua, wakahangahika na sasa wanafurahia vipaji hivyo

BC said...

Nimeipenda "changamoto" hii.Kimsingi hili ndilo lililonisukuma kuanzisha Bongo Celebrity.Niliona ipo haja ya kuenzi wakongwe na watu wengine maarufu ambao,kwa njia moja au nyingine,wamechangia kutufanya tuwe jamii kama tulivyo.Niliona ipo haja ya kuhifadhi habari zao.Mahali pa pekee nilipoona pana uwezo wa kusaidia katika hili ni mtandaoni.

Masangu,wazo la Tanzania Walk of Fame ni zuri mno.Naliunga mkono.