Maneno yote yenye rangii hii ni viunganishi kwa blogu zilizotajwa.
Ni kweli kuwa siku kama ya leo miezi 12 iliyopita, niliamua kufuata ushauri wa Kaka MICHUZI wa kuanzisha BARAZA langu ambalo lingeniwezesha niJIACHIE kimawazo hapa na kuwakilisha mengi kwa jamii. Nilifuata ushauri huo kwani karibu kila NUKTA ya MAISHA yangu nimekuwa nikizama MAWAZONI nikiwaza namna ninavyoweza kurejesha uelimishaji kwa jamii. Miezi 12 iliyopita blogu zilikuwa nyingi lakini si kama sasa. Sasa hivi unaweza kujihakikisha kuwa kama watembelea blogu mbalimbali, UTAONA NA KUSOMA UNACHOKIPENDA tena toka kwenye COLLECTIONS ya wanablog wazalendo. Na hata MWANANCHI MIMI nilipoamua kujikita katika ukumbi huu, nilijua kuwa kuna mengi tunayostahili kuyasema ili jamii yetu iJIELEWE kwa namna mbalimbali lakini kuu ikiwa ni kuwafanya wapate UTAMBUZI NA KUJITAMBUA. Hilo si jambo rahisi, kwani kuna waonao UPANDE WA PILI wa mambo kama wenye manufaa zaidi (hata kama si wa manufaa kwa jamii) na hilo hutusababishia kazi ya ziada katika UDADISI wa kile tuandikacho na hasa katika UCHAMBUZI wa habari mbalimbali. Uchambuzi huu hubainisha ukweli na uozo unaoendelea na si ajabu sasa kushuhudia VIONGOZI NA HOFU YA KALAMU zinazoanisha mapungu, uongo na udhaifu wa utekelezaji wa ahadi zao na haki za wananchi.
Kwa mwaka mmoja niliokuwa karibu saana katika kufuatilia majamvi yetu haya, nimejifunza meengi sana ndani mwake. Blogu zetu zimekuwa na zitaendelea kuwa sehemu muhimu kwa jamii yetu, na zaidi kwa kuwa sasa twawafikia wengi tangu tulipoamua kuwa ni SWAHILI TIME kwa teknolojia hii. Tuna mada tofauti zenye hadhira tofauti kwa nia tofauti na kupafanya kuwe na majina tofauti na hata wale wapaonapo kama KIJIWENI, bado tunajivunia kuwa ni kijiwe chema chenye mengi mema. Tujuao faida hatuwezi kuacha kukaa kijiwe hiki cha blog. Habari ni mseto kwani tunao wanajamvi wanaoANGALIA BONGO wakituletea habari za habari za MTAA KWA MTAA ambao kila kukicha wanakuja na habari za namna ya kutuwezesha kupigana na magumu ya maisha na kutambua kuwa INAWEZEKANA kuikomboa jamii yetu. HAPA KWETU (bloguni) pamekuwa chachu ya suluhisho la mengi na kuifanya jamii iVUKANI (Ooops!! nimeongea ki-ukweni nikimaanisha iamke) katika usingizi iliyopo. Blogu hizi zimeifunza jamii kuwa UHURU HAUNA KIKOMO na kuifunza mengi yasiyojulikana kwayo huku ikiwasisitiza kutojiona wajinga kwani ukweli uko kwetu sote kuwa UTAKAPOJUA HUJUI NDIPO UTAKAPOJUA. Nililojifunza katika mwaka huu wa kuperuzi kwenye blogu zetu ni kuwa tunagusa kote na yote. Tunatumia HADUBINI zetu kuchungulia na kujulisha KULIKONI UGHAIBUNI na kwa wale wasomi hawaachwi nyuma kwani kuna wanaowapasha yatokeayo huko kwa kuangalia PILIKA VYUO VIKUU. Walio na mpango wa kuingia huko pilikani wanaendelea kuwa ndoto hizo wanapoweza kuona namna ya kupata SCHOLARSHIPS kwa wenye uhitaji na waliomaliza na kuanza kazi na maisha, wanasoma mchakato mzima wa UCHUMI NA FEDHA.
Lakini si hayo tu. Tunawezeshwa kuANGALIA BONGO na hata nje katika SPOTI NA STAHERE na kujua mengi katika ujumla wa ANGA LA MICHEZO. Tunapata TASWIRA katika BONGO PICHA na hata habari kuhusu BONGO MOVIES zinazorekodiwa kila uchao bila kusahau kizazi kinachoonekana kuwa na PASSION 4 FASHION ambacho chaja juu kwenye mambo ya FASHION na pia katika fani ya UMODO. Tumeanza kutumia blog zetu kuenzi kazi za kila BONGO CELEBRITY ambao kwa namna moja ama nyingine wanaonekana kusahauliwa na wenye mamlaka na hii ni kuonesha kuthamini mchango wa waliotutangulia. Iwe ni katika muziki wa asili ama ile tuijumuishayo katika AFRICA BAMBATAA ama aina yoyote ile ya muziki. Kwa ufupi, kwenye blogu zetu twaweza kupata kila KALI NA MPYA TOKA BONGO. Niseme kuwa blogu zetu zatupa FULL SHANGWE. Uzuri wa mseto wa logu zetu, ni kama nilivyosema awali kuwa unatupa yote. Humu twapata NYIMBO ZA DINI na pia mijadala mbalimbali ihusuyo imani kutoka katika zile zilizojikita katika injili pekee (kwa lugha nyingine twasema STRICTLY GOSPEL)
Lazima tukubali kuwa blogu zetu ni MWANGAZA na kiunganishi muhimu kwa jamii yetu. TWATAKIWA KULITAMBUA HILO na kulienzi. Tusiwe kama wale wapishi :"wababaishaji" watumiao sura za walaji kupima ubora wa vyakula vyao wakisahau kuwa CHAKULA KITAMU NA KICHUNGU VYOTE VYAWEZA KUMFANYA MLAJI AKAKUNJA USO. Humu ni mahala unapoweza kuelimika vema, tuna hazina ya busara na mafunzo humu. Tuna ABSOLUTELY AWESOME THINGS katika blogs zetu ambazo takribani kila moja imejidhihirisha kuwa THE HILL OF WEALTH katika yale izungumziayo.
Labda mwisho niwashukuru kinadada wanaoendeleza fani hii wa nguvu zote. Ma-DIVA hawa wamekuwa WANAWAKE WA SHOKA katika kueleza, kutetea na kuelimisha mambo mbalimbali ambayo kinakaka / kinababa wasingeweza kuyajengea hoja kikamilifu.
Kwangu mimi blogu ni kama nyumbani na sina budi kuwakaribisheni katika awamu ya pili na blogu hii. Nasema KARIBUNI NYUMBANI. Nyumba ambayo inajumuisha yooote toka ulimwenguni. Ni ulimwengu wangu mdogo (ama niiseme kimsisitizo kuwa MY LITTLE WORLD) tunakojuvyana na kueleweshana mambo mbalimbali. Tukitafuta maisha bora kwa kila mTanzania. Na nina hakika tukiwa na umoja na nia TUTAFIKA TUUU!!!.
Kwangu mimi, nyote ni mashujaa.
SIKU NJEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
18 comments:
Hongera sana kaka kwa kutimiza mwaka mmoja. Ni mafanikio makubwa sana. Miezi 12 yote umefanya kazi nzuri sana. Umetuelimisha, umetuburudisha, umetukumbusha na kutushirikisha.
Umetupa changamoto kubwa katika mambo mbalimbali ya maendeleo ya maisha ya mwanadamu. Hakika tunajivunia kuwa na wanablog kama wewe.
Ni wajibu wetu kupashana habari na kuelimishana kwa ajili ya ukombozi wa fikra zetu. Blog zetu zinafanya kazi kubwa kuliko chombo kingine cha habari. Tunayo nafasi ya kuwafikia watu wengi tukijivunia kuwa na habari zisizo haririwa kwa manufaa ya watu fulani.
Nirudie tena kukupongeza kwa mwaka mmoja kwenye harakati. Nitumie fursa hii kuwapongeza pia wanablog wote. Kazi yao ni ya kujivunia.
Sambamba na hayo, nakupongeza kwa umaridadi wa maarifa ya kuandika post hii ya leo. Inavutia kuitazama, kuisoma na kuifikiria.
Nilikuahidi zawadi, nipo kiguu na njia kuelekea barazani kwangu kukuwekea.
Mungu akubariki sana wewe na familia yako, na wanablog wote.
Pamoja daima.
Hongera sana kaka kwa kutimiza mwaka mmoja. Ni mafanikio makubwa sana. Miezi 12 yote umefanya kazi nzuri sana. Umetuelimisha, umetuburudisha, umetukumbusha na kutushirikisha.
Umetupa changamoto kubwa katika mambo mbalimbali ya maendeleo ya maisha ya mwanadamu. Hakika tunajivunia kuwa na wanablog kama wewe.
Ni wajibu wetu kupashana habari na kuelimishana kwa ajili ya ukombozi wa fikra zetu. Blog zetu zinafanya kazi kubwa kuliko chombo kingine cha habari. Tunayo nafasi ya kuwafikia watu wengi tukijivunia kuwa na habari zisizo haririwa kwa manufaa ya watu fulani.
Nirudie tena kukupongeza kwa mwaka mmoja kwenye harakati. Nitumie fursa hii kuwapongeza pia wanablog wote. Kazi zao ni za kujivunia.
Sambamba na hayo, nakupongeza kwa umaridadi wa maarifa ya kuandika post hii ya leo. Inavutia kuitazama, kuisoma na kuifikiria.
Nilikuahidi zawadi, nipo kiguu na njia kuelekea barazani kwangu kukuwekea.
Mungu akubariki sana wewe na familia yako, na wanablog wote.
Pamoja daima.
Kwnza kabisa napenda kusema HONGERA sana. Binasi nilishatimiza mwaka mwei wa pili lakini siku hiyo nilikuwa mgonjwa. HONGERA Mubelwa. Pia nimefurahi sana kwa jinsi ulivyoiandika mada hii inavutia na inapendeza nakusifu kwa mpangilio huu kazi nzuri sana. Na ni kweli Binafsi nimejifunza mengi sana kupitia blog hii kuna viburudisho, yaliyopita na bila kusahau CHANGAMOTO. Ni kweli tunapaswa kujivuna. Uwe na wakati mzuri Mubelwa.TUPO PAMOJA DAIMA!!!
pamoja na mwaka huo, post hii imetulia. ni ya kushea kijiweni. ni mwaka mwingine wa kujibaini sisi wenyewe.
kweli tumejifunza mengi, tumefahamiana, nk
changamoto ni changamoto tu.
hakuna kulala
nilijua umerudia ile ya mwaka mpya. knimezoma kumbe hazifanani hata kidogo.
kweli tena ni nzuri
Vipaji Tanzania vipo sana ila tu hatuvijali. Hebu kaa ujaribu kuandika post kama hii uone kama utaweza (mimi siwezi).
Hongera Mulangira. Wewe ni mchambuzi makini na mada unazoshughulika nazo katika blogu hii ni zile za muhimu zinazoigusa jamii moja kwa moja. Endelea kuielimisha jamii. Polepole tu tutafika!
Hongera Mubelwa kwa kutimiza mwaka mmoja wa ku-blogu, kazi nzuri na iendelee.
1. Hongera sana sana sana yaani sana, kijiji chako kutimiza mwaka mmoja...angekuwa mtoto tayari anatembea lol.
2. I think ni my favourite post katika zote ulizowahi kuweka maana ni talent ya kipekee kuweka majina ya blogs mbali mbali na ikaleta maana (I cnt do that).
3. Bado kijiji kinazidi kukua sio...na sie ambao ndio kwanza tunacheua, bado tupo na wewe sambamba lol.
Bless ya bro!! xx
Mzee wa Changamoto,
Kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikichota ujuzi na maarifa hapa bila kusahau burudani kabambe za miziki ya kifalsafa,nashindwa kuamini kwamba umekuwepo hewani katika mwaka mmoja tu uliopita.Naona kama umekuwepo kwa muda mrefu zaidi.
Hoja zako,busara zako na jinsi ambavyo umeruhusu blog yako kuwa sio tu kitambulisho chako pekee bali kitambulisho cha kile unachokiamini na kukisimamia,ni miongoni mwa sababu ambazo zinatufanya sote tupende kusoma na hata kuchangia unachokiandika.
Waraka huu wa kutimiza mwaka ni mfano wa ninachokiongelea.Umeperuzi na kuweka,kwa umaridadi,viungo vya blogs mbalimbali.Nimeipenda sana hii.
Nakutakia kazi njema.Tafadhali endelea kublog.
Mzee wa Changamoto,
Hongera sana kwa blogu yako kufikisha mwaka mmoja. Kwa mabloga wengi, tatizo si kuanzisha blogu, bali ni kuhakikisha kuwa kuna habari mipya zenye kuvutia wasomaji.Umefanikiwa katika muda mfupi kuwa na blogu yenye mvuto.
Nimekuwa nikifuatilia uchambuzi na maoni yako kuhusu mada mbai mbali, napenda kusema nimefurahishwa na kina cha uchambuzi wako.
Keep it up.
Mdau
Faustine
Kwetu UHAYANI kuna msemo usemao "usijishukuru kama mwendawazimu"
Na mimi niliweka POST hii kuwashukuru wadau ninyi kwa kuwa nanyi kila iitwayo leo. Tumetembeleana kimawazo na kuelimishana saaana pia kujenga umoja wa kuielimisha jamii yetu. Ninyi kunipongeza mimi naamini si sahihi. Pongezi zije kwenu nyote. Kuna wanaonifanya niendelee kuandika kwani hata nibanawapo na vi-shughuli vya maisha napata email kuulizwa "mbona kimya?" Hivyo najua wapo walio na muda hata wa kunijulia hali nikipotea. Kuna wale ambao wamekuwa ma-fundi mitambo wa blog hii. Yaani kila uchao najifunza toka kwao, nawauliza hili na lile na hata "kudesa" (kama asemavyo Da'Mdogo Koero) busara na hekima zao kila uchao.
Wapo ambao kwa CHANGAMOTO ZAO naweza kujua zaidi kuhusu kazi na maisha na naweza kusema hiki kiwekwacho hapa ni MCHANGANYIKO (COMBO)ya takribani kila mmoja wenu (sijui kama itaonekana ni wizi wa style na mawazo na mitindo) na wenye kuhitaji shukrani ni ninyi.
Lakini LILILO KUBWA ni kuwahakikishia kuwa UMOJA UNAOJENGWA BAINA YETU ndio hasa NGUVU ya KUIKOMBOA JAMII YETU na tukiimarisha blogu zetu tutaweza kusonga mpaka kwenye kuweka maandishi yetu kwenye mifumo mingine itakayowafikia wanaoihitaji zaidi. Hatuwezi sasa lakini haimaanishi tusifanye lolote. Wenyewe wanasema DON'T DO NOTHING BECAUSE YOU CANT DO EVERYTHING.
Ni wakati wetu kuanza na HABA NA HABA na panapo majaaliwa na TUKIIMARISHA NA KUKUZA UMOJA WETU basi TUTAJAZA KIBABA
Blessingsssssss
Mzee wa changamoto nimeikubali hii post. NAWEZA KUSEMA NI KIPAJI CHA HALI YA JUU. nimeisoma mara mbili mbili, NIMEPENDA ULIVYOCHEZA NA LUGHA. kuanzia leo sipo kwenye kundi linalosema kuwa lugha ya kiswahili haijitoshelezi. Ina misamihati ya kutosha. MIMI INGEWEZA KUNICHUKUA ZAIDI YA MWAKA NA NISIWEZE KUTOKA NA KAMA POST YAKO.
hongera kwa kufikisha mwaka mmoja. Naamini tutaendelea kusoma na kujifunza mengi mbeleni toka kibarazani. HONGERA SANA MKUU
Kaka Mubelwa Bandio,
ebwana ndio.
Nakupongeza kwa blog yako kutimiza mwaka mmoja.
Kwa kweli ktk baraza hili nimekuwa nikijifunza mengi sana kuanzia ya kisiasa, kijamii na hata ya kiuchumi.
Nimwambie kaka Mubelwa kuwa kwa hivi sasa mimi ni mpenzi sana wa miziki ya Rege.Huwa nazipitia song lyrics na huwa navutiwa sana na yanayozungumzwa kwani yanailenga jamii kwa kuelezea matatizo,furaha na nini kifanyike ili kuinasua jamii ktk matatizo.Kwa ujumla kaka anatuonyesha nafasi ya Music ktk jamii kwani mbali na rege pia hutumia aina nyingine za miziki ktk kuielimisha na kuiburudisha jamii.
Umakini wake ktk kuandaa posts na pia umakini ktk utoaji wa maoni ni kati ya vitu ambavyo vyanilazimisha kusema kuwa kaka huyu ni lulu sana, tena sana ktk ulimwengu huu wa blog.
Posti hii ni "CHANGAMOTO YETU" sote kwani inatufundisha na kutuambia wanablog wote kuwa twatakiwa kuwa wabunifu,wenye nia ktk utendaji wa mambo(ndio maana post hii imekuwa na mvuto wa kipekee kabisa.) bila kusahau umuhimu wa wale wote watuzungukao.Hakika post hii imenifurahisha kupita maelezo na amedhihirisha uwezo wake.
Kaka,
Ninakutakia kila la heri ktk maisha yako na nakukaribisha kwa moyo mmoja ktk awamu hii ya pili ya kuielimisha jamii.
Hongera Papaa Mubelwa!
Blogu kibonge hii we acha tu!
Kublog si kazi ndogo hata kidogo..nakutakia kila jema katika kuendeleza libeneke la kublog..
kila jema
Tutafika tu
Wewe ni kiboko na Hongera sana kwa jinsi ulivyo creative.
Keep it up
Hongera sana!
Siku zinakwenda kwa kasi kweli. Hatimaye ni miaka mitano. Ninayerejee maoni yangu ya miaka minne nyuma. Naomba uzipokee pongezi zangu za dhati.
Unafanya kazi nzuri sana. Ninajivunia kufahamiana nawe kwa kupitia kublog.
Salamu zangu kwa familia nao wote wakuzungukao.
Post a Comment