Thursday, October 22, 2009

Happy Birthdate "Uncle" Charles Hillary

Mafanikio kama changamoto na thamani kwa jamii......... Picha kwa hisani ya Da Candy 1. Soma mahojiano yake na BC HAPA
Mubelwa
wa leo anaandika hapa kwenye blog kwa sababu ya watu wengi na kwa namna tofauti saana na mmoja wao ni huyu niliyemtaja hapa. Mr Charles Hillary.
Kifupi ni kuwa kabla sijaandika nilitangaza na kabla sijatangaza nilipenda kazi ya utangazaji na kati ya walionifanya niipende kazi hii na kuona UMUHIMU WAKE KWA JAMII ni Bwn Charles Hillary. Ukweli ni kuwa Mkongwe huyu sijawahi kuzungumza naye ana kwa ana lakini namna alivyoweza kufanikiwa na kufanikisha kazi yake, kulinifanya kujifunza meengi katika kazi hiyo iliyoniweka katika nafasi ya kuiandikia na kuitangazia jamii yale niaminiyo ni ya manufaa kwa jamii.

Nikitakiwa kuwa muwazi kwa nafsi yangu, basi jina lake litakuwa miongoni mwa majibu ya SWALI HILI.
Lakini kuna umuhimu gani wa kusherehekea siku kama hii kwa mtu ambaye hata hanijui??? Ukweli ni kuwa, katika kukua kwangu NIMEJIFUNZA KUSHEREHEKEA MAISHA YA MTU KULIKO SHEREHE ZA MAISHA YAKE na kwa siku muhimu kama ya leo naungana naye na familia yake kusherehekea mwanzo wa maisha yaliyogusa, kuelimisha, kubainisha, kutafakarisha, kufurahisha na pia kuhabarisha mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Maisha yaliyosaidia kunyanyua vipaji vingi na kuangalia mitazamo mingi ya kimaisha. Maisha yaliyosaidia maisha mengine kuwa mema.
Naungana na kila mwenye kuthamini UWEZO, KIPAJI NA JUHUDI za wenzetu kujifunza kuenzi kila ambaye anatumia vema nafasi aliyonayo katika kuielimisha jamii imzungukayo. Pengine hiyo ndio KAZI halisi unayokuwa nayo kama "mtu maarufu" ambapo unajikuta ukiwa kioo cha wengi na kulingana na maisha uishiyo, unaweza kuijenga ama kuipoteza jamii. Leo hii naandika kwa kuwa najua nimuandikaye amekuwa sehemu iliyojenga jamii / ameanza kazi hiyo ambayo nasi tunaiendeleza.

Ni wajibu na CHANGAMOTO YETU sote kuthamini wale ambao kwa namna moja ama nyingine wametuwezesha kuwa tulipo. Kwa kila tuwezaye kumshukuru basi ni vema tukafanya hivyo wakingalipo (kama nilivyowahi kuandika HAPA) na kwa wale ambao wametusaidia bila sisi kujua ama wametusaidia na hatuwezi kuwakumbuka ama hatuwezi kuonana nao na kuwashukuru, basi ni vema kuwaombea tu (kama nilivyowahi shauri HAPA).
Basi uanzapo mwaka mwingine kamili katika maisha yako, nakutakia kila lililo jema, uendelee kufanya vema katika yale mema ufanyayo na utaendelea kuyagusa maisha ya wengi katika wema huo na panapo majaaliwa wengi watadhihirisha umuhimu wa kazi njema uifanyayo.
BARAKA KWAKO NA KWA FAMILIA YAKO
Happy Birthdate future Hall of Famer

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Happy Birthdate "Uncle" Charles!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Charlz Hillary (nasikia huwa hapendi kuitwa Charles!) ni mmoja kati ya watangazaji BORA KABISA kutoka Tanzania na katika ulimwengu wote kunakosemwa Kiswahili. Anaweza akakupa macharanga safi dakika hii, akakimbia uwanjani na kutangaza football kwa utaalamu wa hali ya juu, akarudi tena kukusomea taarifa ya habari mpaka mwenyewe ukasuuzika, akaondoka na kwenda kufanya mahojiano ya kina na rais wa nchi, akarudi kupeperusha kipindi cha salamu za wasomaji na...Ni watangazaji wachache wanaoweza kufanya vitu vyote hivi na yeye na Julius Nyaisanga ndiyo waliipa hadhi Redio One enzi zile. Na mpaka leo sauti yake yenye mvumo bado inaunguruma sawia pale BBC. Happy Birthday!

Faith S Hilary said...

Mmh..eti nimechelewa huku...hehe, anyway Happy Birthday dad!! xx...na Mzee wa Changamoto...biggest fan...he says thanks :-)