Katika vipindi vya Matukio ya wiki na Michezo nilivyobahatika kuongoza pale Times Fm, DiJaro aliweza kushiriki mara kadhaa na kwa hakika alionesha alichokuwa akiamini. Lakini si kwa waliokuwa wakiamini vingine kwani kwao, DiJaro hakuwa na uwezo.
Baadae "alipotea" ambako sikujua nami "nikapotelea" huku nilipo ambako sina hakika kama anajua niliko. Lakini nikasikia namna ambavyo aliendelea "kukua" na kuwa alipata nafasi ya kazi PRT na nikaanza kumsaka na naendelea kumsaka. Hiyo ilikuwa zaidi ya faraja kwangu kwani aliweza KUDHIHIRISHA alichokuwa akijariu kuonesha kwa muda mrefu bila mafanikio.
Mimi na yeye TULIAMINI KUWA ANA UWEZO MKUBWA KULIKO ALIVYOKUWA AKIONEKANA AMA KUDHANIWA na kwa wale waliompinga na kumkatisha tamaa walidhani hakuwa na uwezo bali ALIBISHA UKWELI KUWA HANA UWEZO.
Ni wapi ulipo mstari mwembamba utenganishao UBISHI kama alioonekana nao DiJaro (ambao kwa hakika hana) na IMANI aliyokuwa nayo kuwa yeye ni bora kuliko wanavyomdhania?
Na habari ya rafiki yangu huyu yaniacha nikijiuliza kuwa ni wangapi wanaoishia njiani wakikatishwa tamaa na wasiojua uwezo wao halisi? Ni wapi ambapo tunaweza kuona ulipo mstari mwembamba wa wale wasiokutakia mema na wale wakuoneshao njia sahihi?
Nawaza tu
Hongera Kaka DiJaro na huko uliko, KAZA BUTI
Blessings
4 comments:
Inawezekana hakuna mstari! Kuna wakati unajifunza kitu kingine wakati unabisha kwa kutumia hoja nyingine!
Cha muhimu, wanasema iwapo unajiamini katika jambo, kamwe usikate tamaa.
kusimama imara katika kile uaminicho ndio njia sahihi ya kulinda na kuboresha ulichonacho.
If u have the motivation,
nothing can stop u, from achieving what u want.
Bravo kaka!
Post a Comment