Wednesday, November 4, 2009

Mwaka mmoja baada ya HISTORIA

Tarehe kama ya leo mwaka mmoja uliopita ulimwengu ulitambua kuwa HISTORIA ilikuwa ikiandikwa nchini Marekani. Ambacho hakikujulikana ni kuwa NI HISTORIA GANI ambayo ingeandikwa.
Je!! Ni ya kwa na Rais mwenye umri mkubwa zaidi aingiapo madaakani?
Je!! Ni ya kuwa na Rasi wa kwanza mwenye asili ya Africa?
Ama ni ya kuwa na Rais toka chama kidogo cha siasa? (kumbuka walikuwepo wagombea 5 wa Urais nchini Marekani)
Na ndio maana siku ya uchaguzi (Nov 4, 2008) nikaandika kuwa Kushinda si kazi, Akishinda sasa!!!!!(Bofya hapa kuirejea) na kama ilivyotakiwa akapatikana MSHINDI ambaye ni rais wa sasa Mhe Barack Obama. Ilikuwa ni historia ambayo wengi hawakujua ilikoanzia na kwa waliokosa, basi mwaweza kusoma nililoandika nikisema A NEW DAY: Toka Frederick Douglas mpaka Barack Obama (Bofya hapa)Tazama hotuba ya kukubali Urais aliyoitoa Grant Park, Chicago. November 4th, 2008 ama maandishi yake HAPA
Labda safari ilikuwa ndefu ndio maana watu waliamua "kupumzika" mara baada ya uchaguzi, lakini kwa uongozi huu uliopo madarakani, nahisi kuna wanaojilaumu kwa madaraka waliyonayo. Uchumi unazidi kuporomoka (japo wao si waanzilishi wa hali hii), vita vya Irak na Afghanistan navyo vinazidi kuwa tatizo na wameshaanza kuviita Vita Vya Obama wakimaanisha kuwa maamuzi yake yatatathmini uwezo wake kuongoza nchi, wameanza uangalia ahadi alizokuwa akisema na utekelezaji wake, na kwa hakika ulimwengu umekuwa kwenye hali mbovu kiuchumi kuliko wengi tulio hai tunavyoweza kusimulia.
Mwaka wa kwanza umepita na haujawa na pumziko.
Ni vipi hali ya tathmini ya mwaka wa u-Rais wa Obama itaathiri imani za waMarekani? Ni kweli wengi wanajua ni zipi lawama zake na zipi si stahili yake? Ni kweli watu watatambua kuwa uchumi na maisha ya sasa ni tofauti ukilinganisha na wengi tujuavyo???
Na ni kweli kuwa ataweza kuwaeleza waMarekani ni kwanini hajawa TUMAINI kama ambavyo walitegemea?
Mwaka mmoja katika HISTORIA ya uongozi unamalizika leo.
NINI KITAFUATA???

Kwa upande wa Tanzania kumbuka mwaka jana tuliwaza nini ningejibiwa kama NINGEPATA NAFASI YA KUONGEA NA RAIS WANGU SIKU YA UHURU (Bofya hapa)

2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

binafsi sishanga na sikuona ajabu kwa Obama kuwa rais kwani sitambui rangi bali natambua utu au ubinadamu.

kwa hiyo basi hilo si noma na mambo ya uchumi bwana siasa za dunia zina mambo yake kwani kuna wanaozipanga na hawa wanasiasa huwa makasuku wa kurudia na kutete walichoelekezwa na ndio maana wanasiasa waliokataa amri na kujifanya kuleta amana kama akina Kennedy, Lumumba, Nkurumah nk walipata ajali na kufariki haraka

kwa hiyo Obama na ajifanye anayake ya kuleta usawa kiukweli ukweli sio kigeresha harafu uone.

amina

malkiory said...

Mkuu, umefanya vizuri kutunza na kutukumbusha hili tukio la kihistoria.Inaonesha ni jinsi gani ulivyomakini kuweka kumbukumbu.