Thursday, August 12, 2010

Ni mimi, sisi, wao ama mazingira?

Haya sasa. Nyakati zaenda na pengine wapo ambao kama mimi wanaendelea kukubaliana na ile dhana ya ZA KALE NI DHAHABU.
Lakini bado nawaza kama ni kweli kuwa vingi ya vya kale ni bora kuliko vya sasa.
Na hili laweza kupingwa kwa kuangalia tafsiri ya UBORA wa kitu ama vitu.
Binafsi nimekuwa nikiamini kuwa utendaji wa kazi wa kizamani ulikuwa ukihusisha akili za kibinadamu zaidi ya ilivyo sasa ambapo karibu kila kitu ni automated.
Nirejee kwenye MUZIKI. Nimekuwa mpenzi mkubwa wa Marehemu "TX" MOSHI WILLIAM na kitu kikubwa kilichokuwa kikinifanya kupenda tungo zake ni namna alivyoleta uhalisia wa maisha katika tungo hata zilizokuwa zilizokuwa zina mafumbo.
Ninapozungumzia muziki wa zamani kugusa maisha simaanishi kuwa muziki wa sasa hauna ujumbe na kugusa maisha ya sasa.
Lakini naendelea kujiuliza kama Ni mimi, sisi kama mashabiki ama mazingira ya maisha ya sasa? Nakumbuka kati ya nyimbo zilizokuwa zikinipa taswira ya kinachoimbwa ni huu wa Tuma (japo hii ni remix)

Lakini kuna TUNDA SPECIAL yao

Na hata MASIMANGO yao TOT-Plus

Nihamie kwenye MICHEZO YA KUIGIZA. Michezo hii ilikuwepo tangu awali na labda tofauti ni kuwa "enzi" hizo tulikubali kuwa hii ilikuwa michezo ya kuigiza, tuliikubali na kuendelea kuiboresha kwa namna hiyo. Ninaloona sasa ni MAIGIZO YA MAIGIZO na "kurushwa daraja" na kuitwa MUVI.
Hayati Mzee Pwagu ambaye maishani mwake alikuwa zaidi ya muigizaji. Waliokuwa waelimishaji wakubwa waliofanya kazi kwa ufanisi na kuleta taswira halisi ya wazungumzacho licha ya kuwa walikuwa wakisikika tu redioni na si kuonekana. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
Photo credit:
Bongocelebrity.com
Ninalowaza ni kama kweli kuwa vya kale vilikuwa na ubora ama ni mtazamo wangu ama ni mtazamo wetu sisi wasikilizaji wa sasa?
Ama ni mazingira ya maisha ya sasa ambayo yanatufanya kuthamini kile kilichopita? Labda sikiliza maigizo ya enzi hizo

4 comments:

Maisara Wastara said...

RIP mzee Pwagu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kutamani ya jana ni sawa kabisa na kuyahofia, au kwa maneno mengine ni kuisha jana badala ya leo.

ila ya kale ni dhahabu, labda kwa kuwa sielewi dhahabu ninini isjekuwa komeo la kufungia choo, kama ningejua ubora wa dhahabu ningekubaliana nawe, ila dhahabu ilivyo mbaya kwa kuleta vita kwa waigombaniao, kuleta umasikini na hata kusababisha watu kujipodoa nayo, ukisema ya kale ni dhahabu labda ni kweli,

sema past ni muhimu kwa evaluation ya present, amini usiamini!

lakini mimi nafurahia nililonalo sasa. wengi huipenda past kwa sababu inawaweka mbali na future ambayo ni kifo!

najiuliza tu hapa mimie ehe

Simon Kitururu said...

Tukumbuke tu WAKALE nao walikuwa na KALE zao. Msemo `` Old is gold ´´labda kunamaeneo imezidishiwa sifa zisizostahili.:-(

Yasinta Ngonyani said...

ustarehe kwa amani mzee Pwagu.