Wednesday, September 15, 2010

Blogu shule... wafunza na kufunzwa

Photo Credit: Living Big. Watoto wa Baraka
Swali pekee si NAWEZA, bali pia NAWEZAJE?

Ijumaa ya tarehe 3 mwezi huu niliweka bandiko kuhusu hotuba ya Eric Shigongo aliyoitoa Minnesota kwenye mkutano wa Diaspora ambapo nilisema NIMEJIFUNZA KITU KUTOKANA NA HOTUBA YAKE.
Lakini akaja ANON ambaye aliweka "mtazamo wa ndani" zaidi kuhusu Shigongo ambapo tulijadili na kufunzana KWA HESHIMA kuhusu "mafanikio" ndugu huyo ambapo suala kuu nililojifunza ni kuwa "swali pekee si NAWEZA, bali pia NAWEZAJE?"
BOFYA HAPA kuisoma na kurejea maoni yetu.
BARAKA KWAKO

3 comments:

Simon Kitururu said...

Bogu shule ukitaka kujifunza.

Tukumbuke tu pia na katika wote waliowahikwenda shule hata angalau ya MSINGI na yenye walimu wazuri tu, SIO WOTE walioweza kufanikiwa kujifunza.

Na kwa kuwa kuna mitihani ambayo unaweza kuifaulu kwa KUKARIRI tu USICHOKIELEWA, labda hata wajulikanao kwa kupasi mtihani labda sio kweli wamejifunza.:-(

NAWAZA TU hapa MKUU!

emu-three said...

Blog shule kwa wenye kutafakari, kama ulivyo mtandao(internet).
Vijana wengi wanapotea kwa njia na wale wenye kutafakari wananeemeka, kwani kama jamaa mmoja alivyosema, mtandao ni kila kitu, chema na kibaya, mwenye hulka ya ubaya atayapata mabaya yake na wema wataneemeka.

SN said...

Nilikuwa nimebanwa Mubelwa.. Lakini ile siku wakati mnabadilishana mawazo na yule Anon, nilikuwa nawafuatilia. Nikaamua nisiingilie kati; mi kazi yangu ikawa ku-refresh tu!