Friday, February 24, 2012

MUALIKO WA MAULIDI YA MFUNGO SITA DMV

Mualiko wa Maulidi ya DMV Jumuiya ya Tanzanian Muslim Community Washington DC (TAMCO) inapenda kutoa mualiko huu kwa Watanzania wote wa DMV kwenye maulidi ya mfungo sita yatakayosomwa siku ya Jumamosi Feb 25, 2012 mida ya saa 5:PM Jioni, Adress

Park: 10615 New Hampshire Avenue, Silver Spring, MD 20903
Tarehe na siku ile ile Jumamosi Feb 25, 2012 mida ya saa 5:PM Shkran ..

Tuesday, February 21, 2012

Pale "KIBAYA" kinapokuwa NGUVU pekee ya kutangaza "UZURI"

MARUDIO YA April 27, 2010
Septemba 14, 2009 niliandika kuhusu suala la kile kiitwacho UBAYA na UZURI na nililonena ni kuwa Hakuna kibaya kisicho na uzuri...... Yategemea umeachia wapi kuoanisha na tukio (jikumbushe hapa) na bado naamini hivyo.
Ukweli wa mambo ni kuwa kile kiitwacho KIZURI chatokana na kutoonekana kuenenda sawa na kile kiitwacho kibaya japo si kila kizuri na kibaya vina tafsiri moja katika jamii husika.
Lakini tuachane na tofauti za kijamii.
Lolote liitwalo baya lina funzo zuri ndani mwake hata kama funzo hilo ni kutukumbusha kuwa WABAYA WANGALIPO.
Takribani majuma mawili yaliyopita nilikuwa nasikiliza kipindi cha mahojiano cha FRESH AIR kirushwacho na Redio ya Taifa ya Jamii (NPR) kinachoongozwa na Terry Gross ambaye amekuwa akifanya mahojiano mbalimbali katika kipindi hicho tangu 1987. Katika kipindi hicho ambacho siku hiyo Terry hakuwepo, yalifanyika mahojiano na Frank Meeink (aonekanaye kwenye jalada la kitabu chake) ambaye akiwa na miaka 13 alianza kujitmbua kama SKINHEAD; kundi la watu wawachukiao watu weusi na wayahudi na (wale wawajumuishao kama) watu wa rangi. Alipofikisha miaka 18, akawa "sauti ya kundi hilo" huku akizunguka nchini akitafuta wanachama wapya wa kundi hilo na pia kuendesha kipindi cha Televisheni huko jimbo la Illinois kwa dhamira hiyo hiyo. Baadae alikamatwa na kufungwa kwa kosa la kuteka na kumpiga saana mwanachama wa kundi jingine la Skinhead.
Kwa mujibu wa tovuti yake, "While in prison he befriended men he used to think he hated, men of different races. After being released from prison, Meeink tried to rejoin his old SkinHead pals but couldn't bring himself to hate those whom he now knew to be his friends." (Anzia Dk 19:10 - 24:42)

AUDIO HII NI MALI YA NPR NA IMECHUKULIWA HAPA
Ukisikiliza kwa makini utagundua kuwa Frank aliamini kuwa alikuwa na marafiki waliokuwa wanawaza mamoja. Na aliamini kuwa watu wa rangi nyingine hawakuwa watu na hakukuwa na namna wala haja ya kuwajali. Ni baada ya kufungwa jela na kukutana na huyo kijana mweusi (wa asili ya Afrika) ambaye alionekana kumjali na kuwaza naye kuliko walivyokuwa wale alioamini kuwa wanamuunga mkono. Na baada ya kutoka jela, alijaribu kurejea kwao na akagundua kuwa UBAGUZI hauna mwisho na hata ndani mwao wakaendelea kubaguana kuhusu "uzungu" wao jambo lililomfanya aichukie "jumuiya" aliyoamini ina umoja.
Ni kwa KUFUNGWA JELA kulikomfanya awape nafasi ya pili ya kuwafikiria watu alioamini kuwa HATOWAPENDA MAISHANI na hata alipotoka na kukorofishana na "wabaguzi" wenzake alimpa nafasi mwajiri wa kiyahudi ambaye naye alibadili mtazamo wake kuhusu wayahudi (anzia Dk ya 24:56-27:10)
Leo hii, FRANK MEEINK anajishughulisha na harakati za kueleza ukweli juu ya UMOJA WETU bila kujali rangi za mwili (jambo ambalo alijifunza kwa mara ya kwanza akiwa jela) na baada ya kuona mwanawe akibaguliwa na wanachama wenzake (anzia dk 20:00-24:49).
Tovuti yake imesema "Frank's life stands for tolerance, diversity and mutual understanding in racial, political and all aspects of society. Frank is truly an inspiration in any time of strife and conflict."
Na ni kwa kutumia NGUVU YA UBAYA WAKE WA AWALI, SASA HIVI ANAONEKANA KUWA NA USHAWISHI MKUBWA wa kuwawezesha vijana wengi wenye mtazamo wa kibaguzi kuwa na TABIA NZURI za kuthamini watu wa rangi zote.
Ni hapa unapoona namna ambavyo kile kiitwacho UBAYA kinavyoweza kuwa NGUVU PEKEE ya kusambaza wema.
BLESSINGS.

Labda tujikumbushe aliyoimba MFALME Lucky Dube aliposema Different Colour, One People


JICHO LA NDANI ni kipengele kinachozungumzia mambo mepesi na yaliyo ndani mwetu, ambayo yakiangaliwa vema na kwa tafsiri ama tafakari njema yanaweza ama ndio suluhisho kwa matatizo yetu. Kwa matoleo yaliyopita katika kipengele hiki, BOFYA HAPA

Monday, February 20, 2012

Mazishi ya Dada Christavina. Leo

Kwa niaba ya familia ya marehemu Christavina, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote waliohudhuria na kushiriki katika misa ya kumuaga Dada yetu Christavina iliyofanyika jana Jumapili Februari 19, saa 4 asubuhi (10 am) katika kanisa la Takoma Park Seventh Day Adventist, lililoko 6951 Carroll Avenue, Takoma Park, MD 20912.. Mungu awabariki sana na awazidishie.
Mazishi yatafanyika leo Jumatatu Februari 20. Tutakutana nyumbani kwa marehemu saa 2 asubuhi (8am), na saa 2.30 (8.30) tutaelekea J.B Jenkins Funeral Home iliyoko 7474 Landover Rd, Landover, MD 20785. Pia unaweza kwenda J.B Jenkins Funeral Home moja kwa moja.
Tutaondoka J.B Jenkins Funeral Home saa 3.30 asubuhi (9.30 am) kuelekea makaburi ya Gate of Heaven yaliyoko 13801 Georgia Avenue Aspen Hill (wakati mwingine GPS itaonyesha Silver Spring), MD, 20906.

Asanteni sana na tunamtakia mpendwa wetu Christavina, pumziko la amani.

Kwa habari zaidi unaweza kuwasiliana na:
Ndg. Magoma (202.607.1976);
Ndg. Adelaida (240.602.3183);
Ndg. Matinyi (301.792.2832);
Ndg. Mkakile(240.938.3177);
Ndg. Teddy (301.254.4169);
Ndg. Makaya (202.460.1044);
Ndg. Latifah (240.603.7353); au
Ndg. Rebecca(240 898 7161).

Tuesday, February 14, 2012

Mahojiano kamili na Prof. Lipumba

Jumamosi ya Feb. 12, nilipata nafasi ya kuzungumza na mwenyekiti wa taifa wa chama cha Civic United Front (CUF) ambaye pia alikuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995, 2000, 2005, 2010)
Mahojiano haya nimeyagawa kwenye sehemu tatu.
Katika sehemu hii ya kwanza, amezungumzia kilichomleta hapa nchini Marekani, hali ya siasa ndani ya CUF, kwanini chama chake kimepoteza mguso kwa wananchi, siasa za nchi na hata kujibu maswali toka kwa wasomaji mbalimbali waliouliza kupitia mtandao wa Facebook.

Katika sehemu hii ya pili, amezungumzia utata wa chama chake kuwa sehemu ya upinzani Tanzania Bara ilhali ni sehemu ya serikali Zanzibar, mambo yaliyo katika ilani ya CUF yaliyojumuishwa katika serikali ya Zanzibar, suala la chama chake kutoungana na CHADEMA kuing'oa CCM, na pia ni vipi tunaweza kuenzi umoja tukithamini u-Bara na uVisiwani. Mwisho anaeleza mambo ambayo CUF itafanya kuhakikisha kuwa Tanzania haiwi tegemezi wa misaada ya wahisani.

Katika sehemu hii ya tatu, anajibu swali iwapo atagombea urais mwaka 2015, anazungumzia kuhusu kitabu anachoandika kuhusu hali ya uchumi Tanzania, namna ambavyo serikali inawatumia wasomi kama yeye, msimamo wa chama cha CUF kuhusu Katiba ya Tanzania na mapungufu yake, maandalizi ya CUF kwa uchaguzi wa 2015, anajibu swali la kwanini wasiachane na urais na kugombea ubunge ili kuleta upinzani bungeni, nafasi ya mwanamke ndani ya CUF, nafasi ya upinzani kuiodoa CCM madarakani 2015 na NAMNA YA KUIBADILI TANZANIA.

Monday, February 13, 2012

Maendeleo ya msiba wa Dada Christavina

Kwa niaba ya familia ya marehemu Christavina, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote waliohudhuria na kushiriki katika harambee ya mazishi ya Christavina. Mungu awabariki sana na awazidishie.
Pia, tunapenda kutoa shukrani kwa waumini, waimbaji na wachungaji wa The Way of the Cross Gospel Ministries kwa ukarimu wao na moyo wao wa upendo.
Kwa kifupi harambee ilifanikiwa sana. Jumla iliyopatikana ni kama ifuatavyo:
Pesa (Cash) $4,421
Hundi (Checks) $3,250
Ahadi (Pledges) $1,520
Jumla $9,171
Kwa mara nyingine, tunashukuru sana.
Kwa wale ambao bado wangependa kusaidia, tafadhali fika kwa mume wa marehemu anuani ni 3237 75th Avenue Apt 201,
Landover (or Hayattsville), MD 20785.
Tupo kila siku jioni kuanzia saa 12 jioni (6pm). Kwa wale wa mbali, bado tunapokea michango kwa kupitia
Capital One Bank,
Account# 1351500235;
Routing # 255071981.
Jina la Account ni Lavorn Cryor.

Mipango ya mazishi:
Misa ya kumuaga marehemu itafanyika Jumapili Februari 19, saa 4 asubuhi (10 am) katika kanisa la Takoma Park Seventh Day Adventist, lililoko 6951 Carroll Avenue, Takoma Park, MD 20912. Misa hiyo itamalizika saa 6 mchana (12 noon). Baada ya hapo tutarudi nyumbani kwa mume wa marehemu kwa chakula cha mchana. Mume wa marehemu ameomba, kwa heshima, mwili wa marehemu usipigwe picha. Tutashukuru kwa hilo.
Mazishi yatafanyika Jumatatu Februari 20. Tutakutana nyumbani kwa marehemu saa 2 asubuhi (8am), na saa 2.30 (8.30) tutaelekea J.B Jenkins Funeral Home iliyoko 7474 Landover Rd, Landover, MD 20785. Pia unaweza kwenda J.B Jenkins Funeral Home moja kwa moja.
Tutaondoka J.B Jenkins Funeral Home saa 3.30 asubuhi (9.30 am) kuelekea makaburi ya Gate of Heaven yaliyoko 13801 Georgia Avenue Aspen Hill (wakati mwingine GPS itaonyesha Silver Spring), MD, 20906.

Asanteni sana na tunamtakia mpendwa wetu Christavina, pumziko la amani.

Kwa habari zaidi unaweza kuwasiliana na:
Ndg. Magoma (202.607.1976);
Ndg. Adelaida (240.602.3183);
Ndg. Matinyi (301.792.2832);
Ndg. Mkakile(240.938.3177);
Ndg. Teddy (301.254.4169);
Ndg. Makaya (202.460.1044);
Ndg. Latifah (240.603.7353); au
Ndg. Rebecca(240 898 7161).

Sunday, February 12, 2012

Ana kwa Ana na Prof Ibrahim Lipumba

Sehemu ya mahojiano yangu na mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995, 2000, 2005, 2010)
Amezungumzia mambo mengi juu ya chama, siasa za nchi na hata kujibu maswali toka kwa wasomaji mbalimbali waliouliza kupitia mtandao wa Facebook.
Karibu umsikilize hapa

Ama tazama sehemu ya kwanza ya video ya mahojiano hapa chini

Wednesday, February 8, 2012

Msiba Washington DC

Familia ya Kusaga na Lavorn Cryor wanasikitika kutanga kifo cha mpendwa wao Christavina Cryor kilichotokea Feb, 7 nyumbani kwake kwa Saratani ya Utumbo (Colon Cancer).

Christavina alianza kuugua August 2011 na kulazwa Holy Cross Hospital na baadae kuhamishiwa Georgetown University Hospital.


Februari 6, 2012 aliruhusiwa kurudi nyumbani majira ya saa 3 usiku lakini alifariki masaa matano baadae

Marehemu Christavina alizaliwa October 12, 1983. Ameacha Mume na watoto wawili, (wa kiume miaka 4 na wa kike miaka 2.)

Katika usia wake, marehemu aliomba azikwe hapa.

Kwa wale ambao hawataweza kufika msibani lakini watapenda kutoa rambirambi kwa mchango wa fedha, tafadhali tumia huduma ya benki kama ifuatavyo.

Capital One Bank, NA
Routing Number: 255071981
Account Number: 1351500235

Tunatanguliza shukrani zetu kwa msaada katika kufanikisha shughuli za msiba huu

Msiba upo:
3237 75th Avenue Apt 201,
Landover, MD 20785.

Taarifa zaidi tutawaletea kadri tupatavyo. Tunaomba tujumuike pamoja tuweze kuwafariji wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.

Tanzania ni nini na mTanzania ni nani?

Nakumbuka nilipokuwa ninamsoma Da'Yasinta na uTANZANIA wake anaojivunia (msome hapa) . Nikafurahia saana. Katika maoni kama kawaida nikamsoma Kaka Kamala aliyeleta CHANGAMOTO nyingine akiuliza "tanzania nini na mtanzania ni nani?" na hilo likanifanya nirejeshe mawazo kwa wale ambao wanajua wanatokea Afrika lakini hawana hakika na watokeako. Hivi wana pa kupenda ama wataipenda Afrika kwa ujumla wake? Lakini kuna mengi ndani ya Afrika ya kumfanya mtu asiyelazimika kuipenda aipende? Vita, Ubadhirifu, Ufisadi ama? Tarehe 7 Aprili 2009 nilikumbuka saana nyumbani kisha nikaandika kuhusu siku nitakayorejea nyumbani (Bofya hapa kuisoma post hiyo). Nilijiuliza kuhusu nyumbani kisha "nikasindikiza" toleo hilo na wimbo wake Luciano uitwao When Will I Be Home (Bofya hapa kuusikiliza) ambao pia (kwa mshangao wangu nilipousikia mara ya kwanza) unaitaja TANZANIA kama nchi anayojiuliza kama ndiko iliko asili yake ama la.
Nakumbuka mwanzo wa miaka ya 2000, Kaka-Rafiki Gotta Irie aliniandikia mail kunieleza kuwa alikuwa na mpango wa kumualika Luciano kwenda kufanya onesho nyumbani. Nilifurahi kusikia hivyo kwa kuwa mimi ni msikilizaji na mpenzi wa muziki wa Luciano, na aliporejea toka huko (katika onesho ambalo niliambiwa kuwa lilifana licha ya mahudhurio kuingiliana na matukio ya kidini), lakini hata aliporejea toka huko, Luciano ameendelea kuizungumzia Tanzania na anasema katika kukaa nchini na kutembea alijifunza mengi na kisha akaandika wimbo wa Remember When ambao kama aelezavyo kwenye mahojiano haya yajayo, alipata wazo hili akiwa Tanzania. Nikajiuliza MAPENZI aliyonayo kwa nchi ambayo inazidi kumong'onywa na wabadhirifu na namna anavyojitahidi kuielimisha jamii juu ya uzuri wa Tanzania nikaguswa saaaana. Luciano ni msanii nimpendaye (wacha nikiri) na haipiti siku bila kumsikia.
Yeye yuko nje ya nchi na nje ya bara la Afrika lakini amekuwa akijihesabu (kama walivyo wengi) kuwa ni mwAfrika. Na mara kadhaa ameunganisha hisia zake na Tanzania. Lakini hiyo yamfanya kuwa mTanzania? Hivi hawa wafadhili waliowekeza sehemu kubwa ya rasilimali zao nchini Tanzania kwa manufaa ya watu wasio na uwezo mkubwa / wahitaji tunaweza kuwaita waTanzania licha ya kwamba hawakuzaliwa na pengine hawana uraia wa Tanzania?
Vipi juu ya wale waliozaliwa nje ya nchi na wazazi wenye asili ya Tanzania na ambao wanaendelea kushiriki katika mapambano ya kuikomboa nchi, tunaweza kuwaita waTanzania?
Kwani Tanzania ni nini hasa? Na je! MTanzania ni yupi? Na uTanzania ni nini?
Yule mzawa na mwenye uraia wa nchi anayeinyonya nchi kila uchao, ama yule mwenye mapenzi na nchi na kujaribu kila awezavyo kuona inaenda muelekeo ulio mwema?
Kama walivyoimba Morgan Heritage kwenye wimbo wao Nothing To Smile About (japo wao walizungumzia zaidi hali ya Jamaica ambayo kwa namna moja ama nyingine yafanana na kwetu), tunasikia jinsi watu wanavyoisifia Tanzania kutokana na takwimu mbalimbali. Kwa Amani, Upendo na "mafanikio ya kuinua maisha ya mtu wa chini" japo kwa wale walio nchini wanaona namna mabadiliko yamaanishavyo kuzidi kusubiri bila mafanikio.
Ni jambo la kusikitisha sana kama unakutana na mtu anayekusimulia mafanikio haya tena kwa furaha kuu huku sisi tutokao vijijini tukijua hali halisi waishio ndugu zetu ambao tumewatembelea muda si mrefu uliopita. Simaanishi kuwa hakuna maendeleo lakini sidhani hata kama viongozi wetu wanatambua hali halisi wanayokabiliana nayo wakazi wa vijijini ambako hasa ndiko uliko UTI WA MGONGO WA UCHUMI WETU.
Lakini si vijijini tu, hata baadhi ya sehemu za mijini na kwenye maJiji kama Dar na Mwanza ni ya kusikitisha.
TANZANIA NI NINI, NI YA NANI NA MTANZANIA NI YUPI?
Wacha nirejee kwa "mTanzania wa hiari" Luciano kwenye mahojiano haya ambapo anaeleza kuhusu Tanzania. Msikilize hapa katika mahojiano (ANZA DAKIKA YA 2 NA SEKUNDE 31) umsikie hisia zake kuhusu Tanzania na Africa kwa ujumla
.
Na hii hapa chini ndio video ya wimbo wake huo ambao ni kati ya nyimbo bora saana na zilizotulia na kufikirisha kuhusu asili ya watu weusi ambayo wengi wao wanajitahidi kuitafuta.
Itazame
Blessings

Sunday, February 5, 2012

Mhe. Freeman Mbowe na ujumbe kwa DIASPORA

Jana, ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendelo uliokuwa hapa nchini ulifanya mazungumzo na waTanzania waishio vitongoji vya Washington DC.
Ujumbe huo wa Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye ni Mbunge wa jimbo la Hai na kiongozi wa upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe na Mbunge wa Nyamagana ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Ezekiel Wenje, ulianza kwa kueleza mambo mbalimbali yaliyowaleta hapa nchini na pia kutoa salaam ama ujumbe wa Chama kwa waTanzania waishio nje ya nchi. Msikilize HAPA

Baada ya salam zake zilizotanguliwa na zile za Mhe Wenje, ukafika wasaa wa maswali na Majibu ambapo wananchi waliohudhuria walipata fursa ya kuuliza mambo mbalimbali kuhusu Chadema na Tanzania kwa ujumla. Moja ya maswali yaliyoulizwa ni namna ambavyo Chadema inalichukulia suala la mgomo wa madaktari unaoendelea kuathiri huduma za afya nchini Tanzania. Mhe Mbowe analijibu hilo HAPA ambapo pia anaeleza namna ambavyo uoga wetu unakwamisha harakati za kuishinikiza serikali kufanya mabadiliko yatakayoifaa jamii.

Swali jingine lililoulizwa lilikuwa ni juu ya tatizo za utawala wa sheria kwa wote, juu ya matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo nchini na mchakato wa uraia wa nchi mbili ambayo yalijibiwa kama yasikikavyo HAPA

Likaja swali toka kwa mwanamama aliyemtaka Mwenyekiti Mbowe afafanue tetesi ama shutuma kuwa Chadema ni Chama cha waChagga. Hapa
anafafanua dhana zote hizo na ile aliyosema iliwahi kusambaa kuwa ni "chama cha waKristo"
Msikilize

Pia likaulizwa suala la namna ambavyo Tanzania inaweza kuondokana na utegemezi wa nchi wahisani katika bajeti yake. Hapa
anajibu swali la jinsi ambavyo anaamini Chama chake kinaweza kuondoa utegemezi wa misaada ya nchi wahisani

Lakini pia alizungumzia namna ambavyo tunastahili kuondokana na zile fikra za malighafi na kuanza kuwekeza katika "maliwatu"
Mzikilize hapa chini alivyoichambua


Panapo majaaliwa, mwishoni mwa juma hili tutafanya mahojiano na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF). Kama una swali ambalo ungependa kumuuliza, basi shiriki nasi hapa, ama kupitia changamoto at gmail dot com.

Photo Credits: Abou Shatry wa Swahilivilla blog

Ana kwa Ana na Balozi Seif Ali Idi

Mwishoni mwa mwaka jana pia nilipata fursa ya kumhoji Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idi. Alikuwa mkarimu sana kuzungumza nasi juu ya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ziara yake, maendeleo visiwani Zanzibar, ajira kwa vijana na hata ajali ya meli ya Mv Spice Islander na suala la ushirikiano baina ya chama tawala CCM na wapinzani wao walio katika serikali ya umoja wa CUF.
Msikilize hapa chini

Ana kwa Ana na Nape Nnauye

Mwishoni mwa mwaka jana, nilibahatika kupata fursa fupi ya kuketi na kuhojiana na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Nape Nnauye. Alikuwa nchini kwa ziara fupi ya kikazi na pia alikutana na wanachama wa matawi ya CCM hapa nchiniTulijadili mambo machache tofauti kuhusu chama anachoongoza na migogoro iliyomo ndani mwake.
Karibu kusikiliza mahojiano yetu hapa chini

Thursday, February 2, 2012

Maulid ya mfungo sita hapa Washington DC

TANGAZO

EMBASSY OF TANZANIA IN WASHINGTON DC.

Calling for Nominations of Tanzanians in the Diaspora who have excelled in their careers or who have been honored for service to the community

We invite nominations for Tanzanians in the USA who have excelled in their careers or who are known to have made a significant contribution in their field or to the community. This includes those who have been awarded by a renowned institution for their work and those working for International organizations at a senior leadership position. In sending your nominations please include the following:-

· A short bio of the nominee detailing his/her achievements

· Contact details of the nominator and the nominee including email address and telephone number;

· Current photograph of the nominee in high resolution;

Nominations must be submitted via email to ssaleh@tanzaniaembassy-us.org or mkasiga@tanzaniaembassy-us.org not later than February 15, 2012. Those who will receive highest number of nominations or have notable awards will be included in a publication celebrating 50 years of Tanzania Mainland’s Independence.

Should you require any further clarification please contact Suleiman Saleh at 202-884-1097 or at 202-320-2927, E-mail: ssaleh@tanzaniaembassy-us.org or Mrs. Mindi Kasiga at 202-884-1097 or 202-390-7196 Email: mkasiga@tanzaniaembassy-us.org

EMBASSY OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

1232, 22 STREET NW

WASHINGTON DC 20037

February 1st, 2012