Monday, May 31, 2010

Za Kale vs Maisha ya Sasa......USIA KWA WATOTO & TUPATUPA

Baadhi ya wasanii wa Juwata Jazz Band. Watatu waliosimama toka kushoto (kwao) ni Joseph Maina, Tx Moshi William na Athuman Momba ambao wote sasa ni marehemu. Lakini ujumbe wao utadumu milele
Sina hakina ni wangapi walibahatika kupata nafasi ya kuusiwa na wazazi wao kuhusu mabadiliko ya maisha kulingana na nyakati mbili (ujana wa wazazi na wetu sisi). Ni ukweli kuwa kuna mabadiliko meengi ya kimaisha kuanzia thamani ya pesa mpaka, matumizi yake, umuhimu wa kuweka akiba na mengine mengi.
Pengine huwa tunausiwa lakini si kwa kuongea kama BABA/ MAMA NA MWANA, bali mara nyingi ni wakati wa kugombezwa na kufokewa.
Lakini pia si wengi ambao katika hali ya kirafiki wanaweza kueleza matatizo wanayopitia kwa kuwa walishindwa kuwa na umiliki mzuri wa pesa zao. Ni CHANGAMOTO YETU sote kuweka malengo mema na kuelekeza mabadiliko ya maisha kwa wale watutegemeao.
Leo hii tunao JUWATA JAZZ BAND (ambao sasa wanafahamika kama Msondo Ngoma Music Band) ambao wanakuja na nyimbo zao mbili kuhusu umuhimu wa kupanga vema matumizi. Wa kwanza ni Usia kwa watoto na wa pili ni Tupatupa ambao ni juu ya kijana anayejutia matumizi yake mabaya ya pesa.
Katika USIA KWA WATOTO, twasikia nafasi ya BABA anayewakusanya watoto na kuwaeleza maisha yalivyokuwa huko alikotoka na kuwafananishia na namna yalivyo hivi sasa. Si jambo lionekanalo kufanyika zaidi kwa jamii yetu hivi sasa, lakini ni lazima VIJANA watambue maisha yalivyokuwa miaka kadhaa iliyopita ili kuweza kutambua fika kama wanaendelea kwa kuwa na mambo mapya ama wanaendeleza yale yaliyowahi tokea.
Lakini pia katika TUPATUPA tunamsikia kijana ambaye maisha yalimnyookea na sasa yamemgeuka na anatumia nafasi hiyo kutoa USHUHUDA wa namna ambavyo maisha yanaweza kubadilika na kukufanya uwe na maisha ambayo hukuwahi kuyawaza ulipokuwa na pesa.
ANAISHI KUWAONYA WALIMWENGU KUWA "mkifuata anasa mtapoea kaka mimi"
Sikiliza, burudika na jifunze.

Kisha TUPATUPA

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

Sunday, May 30, 2010

Nawaza. Hivi ni mimi, wao ama mfumo wa maisha usiopingika?

Kwa walio wengi, TEKNOLOJIA ama u-SASA vyatakiwa kumaanisha UBORA. Na ni hapo ninapowaza kama UBORA huo tunautafsiri katika usahihi wake. Nimekuwa nikiwaza na bado nawaza kuhusu mifano mambo haya na hii ni mifano michache ambayo ningependa kushirikisha KUWAZA ili kujua kama niwazalo ni wazo langu, ni wale niwawazao ama ni mfumo wa maisha ambao mimi, wao na wewe hatuna uwezo wa kubadili?
Ninapowaza MAENDELEO, TEKNOLOJIA na UWEZESHWAJI WA SASA katika fani na maisha, nashangaa kuona bado ya kale yanaendelea kuwa na UBORA kuliko sasa. Uncle Charles Hilary. Mkongwe ambaye tangu akiwa enzi za RTD amekuwa zaidi ya nyota kwangu. SABABU?? Msikilize anaposoma Habari, anakuwa na sauti iendanayo nayo, anapotangaza matangazo ya vifo ni sawia, akiwa kwenye muziki unapenda, atangazapo mpira utapenda, atoapo uchambuzi wa mambo mbalimbali utashangazwa na upeo. Sasa hivi uliza ni wangapi wenye "viwezeshwa" vya kompyuta wanaweza hayo?
Photo credit:
Da Candy
Nianzie kwenye Habari. Siku hizi natambua kuwa kuna VIFAA VYA KISASA vyenye nuweza kumsaidia mtangazaji kuwa na sauti nzuri na kufanya mengi apendayo tofauti na ilivyokuwa miaka ya themanini. Lakini ni mtangazaji gani hii leo nyumbani Tanzania anaweza simama na kusema ni bora kuliko wale waliozungumzwa HAPA?. Lakini twajua kuwa watangazaji wetu wa sasa wanasifika kwa kazi njema na wanapata tuzo nyiingi kila mwaka kwa "kazi nzuri"
Hili lanifanya niwaze kama TEKNOLOJIA inaonekana kutupa kiburi na kudhani tutaweza kutenda kila tupendalo hata kama hatuna vipaji. Tunasikia "stereo" nzuri lakini ujumbe, maudhui, fikra, uchambuzi, upembuzi na mtiririko wa matangazo ni sikitisho.Kipa Athumani Mambosasa akidaka mpira wakati Simba na Yanga zilipokwaana uwanja wa Nyamagana 1974
Photo Credit:
Michuzi Blog
Labda nirejee kwenye michezo. Ninatambua kuwa timu za sasa zina vifaa viingi vya kuwasaidia wachezaji wawe katika hali nzuri njeeema kimchezo. Wana gyms, wanakula vema wanafuata ushauri nasaa kuwapima na kuwaweka katika "shape' ili wawe vema. Lakini licha ya tuzo na sifa na mapato mazuri wapatayo, ni nani anaweza kusimama ndani ya Tanzania na kusema yeye ni mlinda mlango mzuri zaidi ya wakongwe kama kina Athuman Mambosasa? Na kama hakuna, ina maana hawafanyi kazi kama walivyotakiwa ama ni mazingira hayawaruhusu kuwa vile walivyokuwa wakongwe hao? Photo Credit @Reuters via Dominion Post
Ama tukizungumzia soka ulimwenguni, kuna mchezaji yeyote ambaye leo hii anaweza kusimama na kusema ni bora kuliko PELE?
Nawaza kama ni wachezaji wa siku hizi wanaocheza chini ya kiwango, ama ni sisi tunaowapima isivyo vema ama ni mfumo wa maisha unaowafanya wa kale kuendelea kuwa wakali?
Labda nirejee kwenye sanaa ya maigizo. Nimekuwa mfuatiliaji wa mambo ya maigizo kwa miaka mingi. Shukrani kwa wazazi wangu ambao wamenijengea mwanzo mzuuri wa kupenda sanaa hii. Nimekuwa pia nikishiriki maigizo tangu nikiwa na miaka 5. Lakini ninaposikiliza michezo ya zamani (baadhi ziko HAPA (kwa Da Subi) na kuangalia video za michezo ya kuigiza ya siku hizi, nashangaa kuwa NINAPATA HISIA ZA TUKIO HALISI nisikilizapo hizi za kale kuliko niangaliapo video hizi. Hayati Mzee Pwagu ambaye maishani mwake alikuwa zaidi ya muigizaji. Waliokuwa waelimishaji wakubwa waliofanya kazi kwa ufanisi na kuleta taswira halisi ya wazungumzacho licha ya kuwa walikuwa wakisikika tu redioni na si kuonekana. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
Photo credit:
BongoCelebrity.com
Nawaza kama licha ya teknolojia iliyopo, kuna muigizaji yeyote anayeweza kusema anawakilisha na kuwasilisha hisia na ujumbe wake vema kuliko waliofanya haya kwa "zana za kizamani" kama kina Mzee Pwagu, Pwaguzi, Jangala na wengine? Ni kweli kuwa wasanii wa sasa hawajui kuwa wana la kujifunza toka kwa WAKONGWE ama hawaamini kuwa kuna lolote wanaloweza kujifunza? Ama wanajifunza na kutendea kazi lakini mfumo wa maisha wawalazimisha kuwa walivyo?
Sikiliza CLIP hii ya PWAGU NA PWAGUZI ambayo "fundi mitambo" SUBI wa WAVUTI ameitengeneza kutoka East African Tube

Nimalizie na wanamuziki. Hapo wala sina ninaloweza zaidi ya kuuliza kuna anayeweza kusimama kidete leo hii kusema kuwa ana "masauti" ya kuwazidi waliotangulia kama Marijani Rajabu, Hemedi Maneti, Moshi William na wengine?
Ndivyo walivyokuwa wakirekodi miaka hiyo. Tofauti na sasa ambapo wasanii wanaweza kurekodi "track" moja moja na kwa msaada mkubwa wa "copy, cut and paste" na bado kuna "effects" za kompyuta.
Photo credits:Picture Depot
Ama licha ya teknolojia iliyopo sasa, kuna anayeweza kusimama na kusema anapiga reggae bora kuliko Bob Marley ambao walikuwa wakirekodi kwa zana "duni" ukilinganisha na za sasa?

Ni hapa ninapowaza tena kama twategemea kuliko tunaloweza kupata toka kwa washiriki wetu wa sasa ama ni kweli kuwa washiriki wa kale walikuwa na mengi ambayo wa sasa hawayapati kutokana na sababu fulani za kimfumo wa maisha?
Kwani ni mimi tu niwazaye haya ama?
Naishia kujiuliza hivi NINAWAZA NINI?
***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

Friday, May 28, 2010

Them, I & Them.....SAVE THE WORLD......Luciano

Amani heshima na upendo kwa waungwana nyote.
Nimekuwa nikiwaza namna ambavyo jamii yangu imefika hapa ilipo ambapo kila juhudi za kuisaidia kuondokana na matatizo kama ya rushwa, ufisadi (sina hakika kama kuna tofauti).
Lakini nawaza hizi harakati za kuibadili jamii kama zitawezekana iwapo tunajitahidi kusaka suluhisho la matatizo bila kujua ama niseme kwa kulikimbia suluhisho hilo. Ni lini TUTATAMBUA KUWA NJIA KUU YA KUIBADILI JAMII NI KUWABADILI NA KUWAFUNZA WATOTO /VIJANA?
Ati watoto wanaenzi rushwa na ufisadi na twaamini tunaweza kuja kuwa na kizazi kisichohusudu rushwa?
Leo sitasema sana, bali turejee kwenye MAFUNZO ya LUCIANO katika wimbo huu SAVE THE WORLD upatikanao katika albamu yake ya A New Day ambaye anasema "if you wanna save the world, you gotta save the children. Set an example for the children to follow, make a brighter tomorrow"

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

Thursday, May 27, 2010

Ubaya wa uzuri ni UZURI WAKE.

*Umeshajiuliza kinachowafanya watoto wa WACHA MUNGU kutoshitukiwa pale wanapomkacha Mungu? Ni kwa kuwa wazazi wamewalea katika misingi ya kutodanganya na KUAMINIWA na hivyo wanatumia UZURI wa kuaminiwa kutenda MABAYA kwa kuaga wanaenda kwenye shughuli isiyo sahihi.
*Umeshawaza hatari kubwa inayozikabili nchi zenye amani? Ni kuwa kwa kuwa na amani hiyo, nchi hizo haziwezi kuwekeza pesa nyingi kwenye kujihami na vita na matokeo yake ni kuwa wanaposhitukizwa, inakuwa ni maangamizi. Yaani UBAYA wa amani (ambayo ndio UZURI) ni amani yenyewe.
*Ati sehemu ambayo haijawahi kuwa na matukio ya wizi ndio yasemekana kuwa rahisi kuibiwa kwa kuwa waishio huko hawana mbinu nyingi za kukabiliana na wizi huo na hata kuwanasa wezi hao. Kwa maana nyingine UZURIwa kutokuwa na wezi ndio UBAYA wa eneo hilo kwa kushindwa kujiandaa na wabaya hao.
*Ati watoto "wapole" ndio wanaoonewa mashuleni na kwenye sehemu nyingine kwa kuwa tu ni wapole. Upole / kutopenda ugomvi ambako ni kUZURI kwasababisha watoto hao kuonewa ambalo ndio UBAYA wa UZURI walionao
*Naona wananchi wasiopaza sauti zao kuhusu mali wanyonywazo na viongozi, wanazidi kunywonywa kwa kuwa tu (ni wazuri) hawasemi
YAANI NAONA NAMNA AMBAVYO UBAYA WA UZURI NI UZURI WAKE

Wednesday, May 26, 2010

THAMINISHA........Da Subi wa Nukta 77

Kuna wakati ambao unakosa la kusema kuhusu mtu ama kitu. Na hiyo ni kutokana na ushiriki wa mtu ama watu kwenye jambo ama mambo fulani.
NAOMBA katika kipengele hiki kipya NIMTHAMINISHE DADA SUBI.
Mmoja kati ya wale ambao wamejitolea saaana kujenga, kuboresha na kuhakikisha blog na tovuti zaendana na wakati. Amekuwa "mtoa tip" katika masuala mazima ya teknohama katika suala la NINI CHA KUFANYA na pia NINI CHA KUEPUKA.
Kila siku nimekuwa nikimwambia Dadangu huyu mpenzi kuwa NIMECHOKA KUELEZA NINAVYOTHAMINI MCHANGO WAKE na ninaloomba ni kumthaminisha hapa Mbunifu Da Subi
ASANTE SAANA DADA SUBI NA NAPENDA UJUE KUWA LICHA YA UFUPI AMA UCHACHE WA MANENO HAUMAANISHI KUTOTHAMINIKA KWA UFANYAYO.
Najua huoni tabasamu wala ridhiko nyusoni mwetu kwa yale uyafanyayo. Na pengine ni kwa kuwa watufunza ama kutushirikisha mambo kwa mafungu ama kwa uchache huoni kama ni mengi utupayo. Lakini kwangu binafsi na wale nishirikianao yale uliyonifunza, UFANYAYO NI MUHIMU NA MAKUBWA SAANA KWETU.
Na ndio maana naona ni vema kuweka thamani yako nikianimi kuwa WASOMAO HAPA, NAO WATATHAMINISHA UWAFANYIALO
Wimbo huu hapa chini ni maalum kwa ajili ya yale mema ututendeayo. Kwangu mimi, YOU ARE A HERO.

Do you see the smiles on their faces
after you have done what you do best
do you see satisfaction on their faces
after you have blessed themw ith your gift
you don't think iit's much
but to them it means the world
they wake up in the morning and wish you were there
don't have to lie to gain their trust
you have never won a Nobel prize
they have never seen you on the TV
your little contribution makes their lives a little bit better every day

chorus
You're a hero x8

big it up, big it up for the fireman
big it up, big it upfor the street cleaners
big it up for the man aNd the woman
who take care of abandonded children
big it up, big it up for the grandmothers
who are left to take care of the children
big it up, big it up Wo!!


**THAMINISHA ni kipengele kinachounganisha makala ama matoleo mbalimbali ya watu mbalimbali wanaojitolea kuboresha maisha ya wengine na hata wale wanaoona vema kuthaminisha yale waliyotendewa na wengine. Kwa matoleo zaidi BOFYA HAPA**

Tuesday, May 25, 2010

Ili uokoaji usiwe uuaji katika ajali.....

NIMEKUWA MHANGA WA AJALI NA NIMESHUHUDIA TOKA TUKIONI NAMNA AMBAVYO UOKOAJI WA MAISHA YA MAJERUHI UNAVYOTENDEKA.
Lakini nilipokutana na makala hii ya
Dr Faustine nikaona ni vema kushirikiana nanyi kuweza kupata uelimishaji zaidi.
ENDELEA NA KILE ALICHOSEMA
DR FAUSTINE
Picha toka Maktaba ya Changamoto yetu
....... Ni muhimu sana kukumbuka kinachookoa maisha ya majeruhi si uharaka wa kukimbizwa hospitali bali ni aina ya huduma aliyopata eneo la ajali.
Mara nyingi fikra zetu ni kukimbiza majeruhi hospitali badala ya kutoa huduma ya kwanza pale pale alipo.
Pia uhamishaji/ubebaji wa majeruhi kama ilivyo kwenye picha hizi unaweza kuleta madhara zaidi kuliko kusaidia. Mifupa inaweza kuvunjika, kama mtu alipata madhara ya uti wa mgongo, mtikisiko unaweza kumfanya mtu huyu akapooza kabisa na pia ubebaji usio makini waweza kusababisha kifo.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika eneo la ajali kama yafuatayo:

1: Kuhakikisha kuwa mazingira yanaruhusu kuokoa majeruhi. Hakikisha kuwa hakuna mafuta yanayovuja kwenye gari au hatari ya moto kulipuka.
2: Fanya uhakiki wa haraka wa walio hai na wenye kuihitaji msaada. Marehemu haitaji kuokolewa.
3: Kama majeruhi hajabanwa, jaribu sana kumsaidia pale pale alipo bila kumsogeza.
4: Kama majeruhi atahitaji kusogezwa uangalifu mkubwa utumike na kuhahakisha zile sehemu za maumivu zinalindwa vyema.
5: Hakikisha njia ya kupitisha hewa ya majeruhi iko wazi na hakuna kitu kinachoziba.
6: Hakikisha majeruhi anapumua. Kama majeruhi anapata shida kupumua inabidi asaidiwe kufanya hivyo.
7: Hakikisha majeruhi ana mzunguko mzuri wa damu na havuji damu kwa wingi. Kama majeruhi anavuja damu kwa wingi, ni muhimu kujaribu kuzuia uvujaji wa damu. Mara nyingi waweza kutumia sehemu ya vazi la majeruhi au la mwokoaji kufunga sehemu ya juu ya sehemu inayotoka damu kwa wingi au kugandamiza sehemu hiyo kama haijaathirika kwa ajali.
8: Hakikisha sehemu zilizovunjika zinakuwa "stabilised" ilikupunguza maumivu na kupunguza athari zaidi.


** Kwa kumalizia unapotaka kumsaidia majeruhi kumbuka: A: Airway; B: Breathing; C: Circulation.

Baada ya hapo ndio unaweza kufikiria kumpeleka majeruhi hospitali.

Pendekezo:
Kutokana na wingi wa ajali nchini, ni vyema vyombo vya habari vikasaidia kuelimisha jamii kuhusu hatua hizi muhimu zinazotakiwa kuchukuliwa kuwanusuru majeruhi pindi ajali inapotokea.
Majeruhi wengi wanapata madhara zaidi au kufa kutokana na uokoaji usio makini.

SIKU YAKO....Siku maalum Da Koero

Sijui ni lipi naweza kusema kueleza faraja niliyonayo kwa kufahamiana nawe. Najivunia mengi toka kwako. Kuanzia ukweli wa uwezo wako wa kuandika, kukosoa, kuchanganua na hata kushauri na kushaurika. Pengine niseme sifa ama umahiri wa KUSIKILIZA mbao hukufanya uwe na suluhisho ama kuwa na swali ama kupata suluhisho ama jibu la kitu.
Kwa muda mfupi tuliofahamiana na kuwasiliana nimejifunza mengi kuhusu na kutoka kwako.
Na hili lanifanya niwaze namna ambavyo wazazi wako Baba na Mama na ndugu zako, waliokuwa wafanyakazi wako, walio wanajumuiya wenzako na jamii nzima 9kama hii ya blog inavyojivunia uwepo wako
UWEPO WAKO NI BARAKA KWA WENGI WENYE MTAZAMO MPYA
Katika siku hii maalum kwako, nakutakia kila lililo jema katika miaka ijayo, nakupenda, nakuheshimu na nakuombea mafanikio.
Ni siku yako.... Siku maalum kwako Da Koero
Kwa kuwa najua kati ya nyimbo zoooote ulim-feel Nasio Fontaine, naomba nikuache na SALA hii toka kwake akimuomba MUNGU amuongoze katika maisha. Nami naomba milima na mabonde iliyo maishani mwetu uikabili kwa imani na naamini kwa msaada wa umwaminiye, UTAVUKA

Lakini pale palipo na VILIO, kumbuka kuwa ni Mungu pekee atufutaye / kuosha machozi. Sikiliza WASH AWAY TEARS yake Gramps wa Morgan Heritage

Happy BirthDATE Sis

Sunday, May 23, 2010

USWAHILI, MSWAHILI NA KISWAHILI

Tunatambulishana na kutambulisha vitu kwa namna ama mitindo mbalimbali (japo si lazima utambulishanaji huo uwe sahihi ama makini)
Mfano: Kuna mchekeshaji mmoja mwenye asili ya Amerika ya Kusini, aliwahi kusema kuwa si lazima uwe umezaliwa kwenye ukanda atokao yeye ili utambulike kuwa ni m-Latino, bali ukishafanya / kupata huduma za ki-benki (kama ku-cash check nk) kwenye liquor store, basi wewe ni m-Latino.
Nilifurahia tu sentensi yake kwa kuwa najua kinachowafanya ndiugu zetu hao wafanye hivyo, lakini jana nilipokuwa nasikiliza nyimbo kwenye mp3 yangu, nikakumbuka nilivyokuwa naitwa MSWAHILI.
Basi kama wako sahihi, hapa chini paonesha maisha na harakazi za kwetu

Na siwezi kupinga kilichonifanya kuitwa hivyo kwa kuwa nilijua fikra za walioniita MSWAHILI. Kwao waliamini kuwa kuongea kwa namna fulani ama hata kusikiliza miziki yenye mafumbo ama lugha fulani ni uswahili. Na mimi nilikuwa natimia kwenye tafsiri yao. Nilipenda na bado napenda maongezi yenye kueleza kitu kwa namna ya kibunifu. Nilipenda na bado napenda maongezi ambayo yana mifano na kuchangamsha akili. Nilipenda na bado napenda maongezi ambayo yana TUNGO TATA.
Yaani kwangu ningependa kusema "chupi ya maziwa" badala ya sidiria. Chumba cha bwenini ungesikia mtu akiulizwa kama fulani ni "bubu wa masikio" badala ya kiziwi kwa kuwa tu hakusikia ulichomueleza. Ni misemo miingi sana ya kueleza kitu kwa namna yake. "Mtoto' ingekuwa na maana nyingi kulingana na sentensi na sasa ukiongezea "mtoto si riz'ki" nayo ingemaanisha vingine. Ilikuwa raha.
Lakini pia nilipenda kusikiliza nyimbo zilizokuwa na MAFUMBO na hata TUNGO TATA. Sasa nikaambiwa hiz ni nyimbo za kiSwahili kwa kuwa zilikuwa zikisema vibaya na wengine kusema ati zilikuwa zikitusi. Lakini nililogundua ni kuwa nyimbo hasa MDUARA ni nyimbo za kufikirisha na pengine badala ya kuziita za kiSwahili, tujifunze kuuliza kisemwacho na kama kina utata basi tusiwe wepesi kuamua alichowaza muimbaji bali tuwaulize waimbaji.
Leo nimekumbuka haya baada ya kusikiliza albamu yangu yenye mkusanyiko wa nyimbo za mduara na nimeona nishirikiane nanyi mawazo haya. Nikisikiliza nyimbo SHANUO na SITISHIKI zao Chuchu Sound nafurahishwa na upangiliaji wa vina na matumizi ya kiswahili fasaha. Mfano wanaposema "maisha si mashindano japo kipato kikubwa unacho wewe". Lakini pia kuna tungo chache Tata ambazo waweza zisikiliza hapa

Pia maumbo yaoneshayo uhalisia wa maisha kama "ni rahisi kuteka maji kwa pakacha kuliko yeye kuniacha" ambalo ni funzo kuwa kuna sehemu nyingine si za kujisumbua "kuharibu"
Lakini kuna mengi ya kujifunza katika "kauli" zao mwishoni. Labda tusikilize ili kujua tujifunzalo na pengine uwaze NINA WAZA NINI nisikilizapo hizi na pia waweza KUWAZA kama wawazao akili zangu kuwa za "kiswahili" wako sahihi

Na sasa tuhamie kwenye SWEET BABY ya TOT-Plus. Kuna kauli ambazo zilikuza mashaka lakini moja ya ambayo nilibahatika kuwa na mdahalo ni ile ya "Anti" ambayo wamezungumzia ku"gonga hodi mara 2 mbele, kama kimya gonga kimya mara 3. Kama kimya mwaga mzigo wako hapohapo nje. Ataupata". Tofauti pekee niionayo kati ya kilichoimbwa hapa na kwetu uHayani ni kuwa sisi kama umegonga mbele na nyuma hujamuona mtu, waacha ka-jani ka mgomba ili wakirejea wajue kuwa kuna aliyekuja akawakosa. Hatumwagi mzigo wao (labda kama umeambiwa ama kukubaliana hivyo). Sikiliza mwenyewe na uwaze.

Katika nyimbo hizi, kuna misemo miiingi sana ambayo inaweza kwenda na maana halisi lakini ikanyambulishwa visivyo. Kama nilivyosema HAPA kwa Binti Mkundi, "Mfano wimbo wa Aungurumapo Simba RMX ambayo Banza aliweka uhalisia wa maisha yetu japo wapo waliotafsiri kama matusi. Alisema "RAHA YA CHUNGWA, UMENYEWE, KISHA UKATIWE". Mimi ni kati ya walaji wazuri wa chungwa, lakini kila ninapofikiria kulimenya na kubaki na harifu ya maganda baada ya kula najiuliza mara mbili kama "kweli nahitaji kula chngwa wakati huo ama la?'" Na nikimpata wa kulimenya na kukata, NAWEZA KULILA WAKATI WOWOTE. Katika wimbo huo huo, Banza akasema "RAHA YA DAFU, UKISHAKUNYWA YALE MAJI, SHARTI DAU LICHOKOLEWE". Sijui atakayepinga kuwa hu ni ULAJI wa asili wa dafu ni nani? Kama huna kichokoleo kizuri basi ndio ungehitaji "njia m'badala" kama kulivunja kisha ukatumia kichokoleo chako hafifu kulila. Na sehemu nyingine akasema "RAHA YA NANGA BAHARINI, MTONI ITASHIKWA NA TOPE." Kwa sisi tuliokulia kwenye misafara ya majini wajua nanga. Na kwa wavuvi wanajua karaha ya nanga yenye matope. Haimaanishi kuwahuwezi kushusha nanga mtoni (maana waliozoea kuvua mtoni wanafanya hivyo) ila SI KWA RAHA KAMA BAHARINI. Na huo ni ukweli ulio wazi. Sasa kutafsiri vingine na wanavyouliza watu nadhani si tatizo la muulizaji, bali la mtafsiri.
UKWELI NI KUWA NAWAZA SIJUI NINAWAZA NINI?

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

Friday, May 21, 2010

Them, I & Them: JUSTINE KALIKAWE .......Kitendawili

Marehemu Justine Kalikawe alipotwaa tuzo ya msanii bora wa ReggaeSafari ya mwisho ya Justine, nyumbani kwake Kitendaguro Bukoba

Nikiwa na baadhi ya wasanii walioshiriki wimbo ulioitwa HAKUNA (urejee hapa). Hapa ni ndani ya Bacyadr Studio kurekodi Video ya wimbo huo uliokuwa maalum kumuenzi Justin Kalikawe

Tukiwa Idara ya Habari Maelezo (2003) na Ras Pompidou, Jah Kimbuteh, Ras Inno, Bi Georgia (Mjane wa Justine) na meneja wake wa zamani Allen Mbaga kuzungumzia Tamasha la HAKUNA lililomuenzi Justine
Jana ni kati ya siku nilizokumbuka meengi saana kuhusu nyumbani. Na ni katika kuwaza huko nikajikuta nawaza SAFARI YANGU YA MAISHA na kujiuliza msururu mzima wa matukio ya maisha yangu. Nikawaza nimetoka wapi, niko wapi na pengine ninaenda wapi. Kama ilivyo kwa wengi wetu, tunaweza kuwa na majibu ya maswali ya tulipotoka na pengine tulipo (kwa mtazamo wetu0 lakini tuendako bado ni KITENDAWILI. Na ni kitendawili hicho tunachojiuliza ambacho kina meeengi yanayohitaji muda zaidi ya tujipao katika kusaka majibu. Nilipofikiria tulikotoka na kilichonileta huku na ninavyosonga ki-umri na kuwaza mustakabali (future) ya maisha yangu na familia, nawaza mengi. Lakini ni jana hiyohiyo ambapo Kaka Gotha Irie alinitumia picha ambayo tulipiga mwaka 2003 wakati tukirekodi video ya wimbo HAKUNA wake Justine Kalikawe. Hivyo nikaenda kumsikiliza Justine na kukutana na wimbo huu ambao nimeona nishirikiane nanyi kwa mara nyingine.

"nilikuja kutafuta ugenini, nikazoea pakawa ni nyumbani, sasa ninaelekea uzeeni, nibaki huku au nirudi nyumbani. Nilioa nikazaa na watoto, na nilipotoka kwao ni kama ndoto; lakini najiuliza siku nikirudi kwetu, niende nao au wabaki huku"
Hayo ni maneno anayoanza nayo mwanamuziki aliyepata kufanya vema saana katika miondoko ya Reggae nchini Tanzania Marehemu Justine Kalikawe katika wimbo wake Kitendawili. Kama ilivyo kwa nyimbo nyingi ambazo zinakuwa na UJUMBE HALISI wa maisha kwa hadhira, wimbo huu bado unaendelea kuwa na maana na mguso uleule kwa wale walio mbali na nyumbani na hasa wale walioanzisha familia ambapo ikifika suala la maisha baada ya kustaafu unarejea kujiuliza kama alivyojiuliza Kalikawe.
Haijalishi alitunga wimbo huu akiwa wapi, ama akijifikiria kama aliye wapi, lakini kwa kuwa alifanya kile afanyacho vema zaidi kwa kutunga nyimbo zenye uhalisia kwa jamii, bado sasa hivi ndugu wengi tulio mbali na nyumbani tukiusikiliza wimbo huu tunapata hisia halisi ya alichoeleza Justine na kuweza kujiuliza maswali ambayo naye aliuliza kwenye utunzi wake huu, bado ujumbe wake unawagusa wengi ambao kwa bahati mbaya kutokana na mfumo wa maisha ya sasa wameelekea popote duniani kwa namna yoyote kusaka chochote ili kuweza kurejesha uwekezaji nyumbani, na kama ilivyo kwa binadamu yoyote, unapofika mahali ndio unapoanzisha urafiki na "udugu" na uliokutana nao, na wakati muafaka ukifika unaanzisha familia na kwa majaaliwa ya Mungu unapopata watoto inakuwa baraka, lakini baadae waweza kujiuliza kama aliyojiuliza Kalikawe kuwa "nilikotoka niliishi na wazazi, babu na bibi, mjomba na shangazi, lakini huku mimi na familia, ndugu wengine ni eneo la kazi eeeee; katikati kuna bahari, tena ni mbali elfu kumi maili, nikisafiri nafika alfajiri tena ni mbali natumia utajiri eee"
Sijui la kusema, lakini namkumbuka Justine kama moja ya nguzo za muziki wa Reggae mkoani Kagera na Tanzania kwa ujumla. Alitumia lugha zake za Kihaya na Kiswahili kufikisha ujumbe aliokusudia kwa jamii husika na mara zote ALIELIMISHA, AKIBURUDISHA NA AMA KUIFUNZA JAMII KUJIKOMBOA KUTOKA KATIKA UTUMWA WA KIAKILI.
Justine alifariki ghafla mwezi wa nane mwaka 2003 katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Kagera mjini Bukoba miezi michache baada ya kurejea kutoka ziara ya kimuziki nchini Denmark. Aliacha mjane Georgia na watoto wawili Abayo na Niwe na mpaka mauti yanamkuta alikuwa ndiye msanii mwenye albamu nyingi zaidi za Reggae nchini Tanzania (8 za audio na 3 za video katika miaka 16 aliyodumu katika muziki wa Reggae). Katika kumuenzi, wasanii nyota wa Reggae nchini walitunga wimbo wa HAKUNA na kuandaa Tamasha maalum la kuenzi kazi na maisha ya Justine lililofanyika Don Bosco. Tulishapata kujadili FIKRA PEVU / MAONO ya Justine Kalikawe katika wimbo wa HAKUNA kwa kuhusisha na uchaguzi ujao HAPA
RIP Justine Kalikawe
Bofya player kusikiliza KITENDAWILI hiki



**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

Tuesday, May 18, 2010

HATIMAYE NIMEREJEA........Nilikokuwa

Hatimaye nimerejea wanandugu. Nilikuwa nimebanwa na mambo kadhaa na pia JUMAMOSI nilikwenda kushuhudia maonesho ya wazi ya ndege za kivita. Ilikuwa saafi sana japo ilikuwa ngumu sana kwa mimi kupiga picha na kurekodi video.
Lakini kwa sasa FURAHIA TASWIRA HIZI HAPA CHINI
Ndimi mimi ndani ya cockpit ya C-17. Yaani ile phobia aliyoizungumkia Kaka Mtondo HAPA na HAPA ndiyo ilikuwa kinikwaza. Ndege imetulia wala haijawashwa lakini bado ni mtetemeko
Mzee huyu alikuwa rubani wa vita ya pili ya dunia. Ana story huyooooooooooo.
Watu woote "macho juu"
Kisha ikaja "main event" ya Blue angel.
Hii "ndude" ni hatari. Inapiga "rivasi" hewani na kusonga kipembeni pembeni. Inatua na kuondoka wimawima. Iangalie hapa chini.

Hii JETCAR hapo juu nayo ilinogesha maonesho. Inakimbizana na ndege.
Ona ilivyokuwa imeachwa hapa
Halafu ilivyo-catch up hapa. Kumbuka gari ilianza 0mph wakati ndege ilishakuwa kwenye mwendokasi
Hii ilikuwa timu ya GEICO. Nayo ilinogesha
Na hii ndio C-17. Ndege yenye uwezo wa ku-taxi kinyume nyume na kuruka kwenye runway fupi saana. Angalia mwanzo mwanzo wa video hapa chini

Friday, May 14, 2010

Them, I & Them.......KNOW YOUR PAST...Morgan Heritage

"If you don't know where you're coming from, you don't know where you're heading. Past, Present and future"
Leo ni siku ya TUZO ZA MUZIKI WA TANZANIA almaarufu kama Kilimanjaro Music Award 2010. Hizi zaaminika ama kuaminishwa kuwa TUZO KUBWA ZAIDI NCHINI TANZANIA na kwa mujibu wa TOVUTI YA WAANDAAJI, "TUZO za muziki nchini maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards (TMA) zilianzishwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mwaka 1999 kama kichocheo cha kutambua wanamuziki nchini na kazi zao."
Ni hapa kwenye "dhumuni" la tuzo nilipojisikia kuandika makala haya ya leo.
Inashangaza sana kuona tunaweza kuaminishwa kuwa tutasonga bila kujua na kuthamini kule tulikotoka. NI UONGO.
Sasa tukiangalia kwa miaka yote ambayo Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiandaa tuzo, hatujaona wanalofanya baada ya "tukio" hilo la kibiashara kujali UWEPO WA WASANII hasa wale waliowafanya hawa wanaopata tuzo leo hii kupenda kazi hiyo? Hivi mmeshaangalia ORODHA YA WANAOWANIA TUZO HIZO? (Hapa) kuangalia kama kuna tuzo ya wakongwe WALIOSAFISHA NJIA KWA HAWA WAFANYA BIASHARA YA MUZIKI SASA? Watu waliojitolea kuifanya sanaa ya muziki kuthaminiwa ithaminiwavyo sasa hawaonekani kujaliwa hata kidogo. Walio hai na waliotangulia mbele ya haki kwa nini hawapewi heshima yao? Orodha ni ndefu ya watu walioimba kuiinua sanaa ya muziki, lakini hatuoni mahala ambapo hawa "wanaojifanya" kuenzi SANAA YA MUZIKI wanashindwa kuenzi walioifikisha hapa ilipo. Na ndio maana leo hii nakumbusha neno kuu lisemwalo kwenye wimbo know your past kuwa "Every man must know their past, so we can stand firm in the future"
Bila kuwaenzi walioifikisha sanaa ya muziki hapa ilipo, ina maana na hawa waliopo hawataenziwa wala kujaliwa muda mchache ujao na ndio maana HATUTAKUWA NA MUZIKI ULIOSIMAMA / KUTAMBULIKA kwa kuwa wenye dhamana ya "kupitisha" HISTORIA, ujuzi na uzoefu wa muziki hawathaminiwi.
NATOA WITO KWA WAANDAAJI WA KILI MUSIC AWARDS KUWAENZI WASANII WALIOTANGULIA KWANI BILA KUFANYA HIVYO HATUTAENDELEA WALA KUENDELEZA MUZIKI
Ndugu watano (L-R) Mr Mojo, Dada Una, Jah Petes, Gramps na Luke ambao wanaunda kundi zima la Morgan Heritage
Basi na tusikilize huku tukisoma maneno mazuri katika wimbo huu KNOW YOUR PAST wao MORGAN HERITAGE

[Intro]
What does it profit a man to gain the world
And loose his soul ?
If you don't know where you're coming from
You don't know where you're heading.
Past, Present and future

[Chorus]
Every man must know their past
So we can stand firm in the future, yes X2

[Verse 1]
History can recall, it can recall
The true essence of ourselves which we have lost
Trying so hard to attain for the future
We have let go what has kept us since creation
But through the Divine powerhouse of life
We'll know past, present and future

[Verse 2]
So many of us have gone astray
Chasing dreams which only fade away
Ignoring the blood, sweat and tears of our forefathers
Breaks the connection to our ancestors
We must all have true awareness of ourselves.
It is a part of a solution.

[Chorus x2]
Stand firm, stand firm, stand firm...

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

Thursday, May 13, 2010

Tunapofelisha kizazi kwa kufaulisha mitihani

Hivi majuzi nimeona matokeo ya kidato cha sita. Matokeo hayo hayakuonekana kuwa na mafanikio saana (kama ambavyo imekuwa kwa miaka kadhaa sasa) lakini hilo wala si jambo la kunishangaza. Lakini pia kati ya waliomaliza ama kuhitimu ni wadogo zangu. Wadogo ambao kwa hakika licha ya kufanikiwa kupata alama ambazo zitawawezesha kuendelea na masomo wayapendayo, bado wanaonekana kutofurahia hilo kwa kujiona kuwa walioshindwa kufaulu.
Binafsi wadogo hawa WALIFAULU KABLA HAWAJAINGIA MTIHANINI kwa kuwa walikuwa wakifanya kila lililo ndani ya uwezo wao kufanikisha ndoto yao. NA HILI NDILO NILIONALO KAMA KUFAULU. Kwa mtu kuweka juhudi kamili kuweza kujua kile anachostahili kujua ni mafanikio hata kama kile kinachoitwa matokeo ama madaraja hayajawa kama upendavyo. Naamini KUFAULU kwa kufanikisha juhudi halisi za kuelewa ufunzwacho na kufanikisha. Na ndio maana nasema wadogo zangu hawa walishakamilisha ufaulu wa maisha (kwa kuweka juhudi katika kila nafasi waliyokuwanayo ili kufanikisha malengo yao).
Lakini mifumo iliyojengwa na waalimu wetu (ambao yawezekana wamejengewa na waalimu wao) ni kuwa unastahili kupata daraja fulani ili uonekane umefaulu. Na ndio maana msisitizo hauko kwenye kuelewa na kuweza kutumia elimu katika maisha na kutatua matatizo ya jamii, bali ni katika kufaulu mtihani kwa kupata maksi kadhaa.
Tusemeje kuhusu WASOMI wetu wa IDARA YA MAWASILIANO IKULU? Unadhani hawakufaulu? Unadhani kuna sehemu yahitaji watu "waliofaulu" vema kama sehemu nyeti kama hizo? Umeshajiuliza wafanyalo huko? Basi SOMA HAPA ama HAPA uone WAFAULU MITIHANI HAWA WANAVYOLIFELISHA TAIFA KWENYE MAMBO NYETI KAMA MAWASILIANO HUKO IKULU
Na pia nimekuwa nikiona maswali meengi kuwa "kwanini wahandisi wa Tanzania hawabuni vitu vya kuisaidia jamii wakiwa nyumbani" na nahisi hili ndilo jibu lake. Kuwa waandisi ambao wamekuwa na alama nzuri darasani na kutunukiwa vyeti mbalimbali kuonesha UFANISI DARASANI lakini wanapoingia kwenye "ulimwengu wa kazi" inakuwa ni shughuli nyingine kabisa kwani wafunzwacho kwa nadharia hakionekani kuwa halisi kwenye utendaji wao. Ni hapo waajiri wanapoanza kusaka kama waajiriwa wao wana vyeti visivyo halali ama walipata matokeo hayo isivyo halali. Lakini mwisho wa siku ni kuwa WALIFUNZWA KUFAULU MITIHANI NA SIO KUFANIKISHA KAZI WASOMEAZO.
Yaani kwa wabunge ndio yaleyaleee. Kuonekana anafaulu kwa kupigiwa makofi katika kila asemacho hata kama hakina utekelezaji. Yaani twaifelisha jamii yetu kwa kufaulisha kile tunachoamini kuwa mtihani japokuwa kitu hicho si suluhisho la matatizo tuliyonayo.

Aaaaaahhh!!! NAWAZA KWA SAUTI TUUU!!!!!!!!!!

Wednesday, May 12, 2010

Hongera kwa Da Vicky Ntetema

Vicky Ntetema
Claudia Duque of Colombia, Tsering Woeser, a Tibetan living in China, and Vicky Ntetema of Tanzania will Receive 2010 Courage in Journalism Awards from the International Women’s Media Foundation. Mexican Journalist Alma Guillermoprieto is Lifetime Achievement Award Winner.
An investigative journalist from Colombia who has been robbed and kidnapped and who has received threats against her life and that of her daughter; a Tibetan journalist who is one of China’s best known bloggers, even though she is under constant scrutiny from the government, and a Tanzanian journalist whose investigations into a series of murders have put her in danger are winners of the 2010 International Women’s Media Foundation’s Courage in Journalism Awards.
“The work that these remarkable journalists do brings to light the dark corners of our globe,” said Judy Woodruff of the PBS News Hour, IWMF Courage in Journalism Awards chair. “They risk everything, including their livelihoods, their safety and the safety of their families, to unearth the truth and enlighten us all.”
Vicky Ntetema, 51, a freelance Tanzanian reporter who contributes to the BBC World Service. Ntetema uncovered one of her country’s horrible secrets when she began to investigate the brutal killings of albinos and their families. Working undercover, she learned that witchdoctors were murdering albinos to dismember their bodies and sell potions made out of their hair, legs and arms. Customers were told the potions would bring them good fortune. Witchdoctors are especially dangerous because they hold powerful positions in African traditional society, often use hired killers and are protected by local police. Ntetema has received death threats since she started her reporting. She has twice left Tanzania for her safety. She now reports wearing hijab to disguise her identity and often travels with a security guard. According to the BBC, some 170 witchdoctors have been arrested for the killings.

The IWMF Courage in Journalism Awards honor women journalists who have shown extraordinary strength of character and integrity while reporting the news under dangerous or difficult circumstances. The Lifetime Achievement Award recognizes a woman journalist who has a pioneering spirit and whose determination has paved the way for women in the news media. Including this year’s honorees, 69 journalists have won Courage Awards and 19 journalists have been honored with Lifetime Achievement Awards. The awards will be presented at ceremonies in New York on October 19 and in Los Angeles on October 21.

Founded in 1990 and now celebrating its 20th Anniversary, the International Women’s Media Foundation is a vibrant global network dedicated to strengthening the role of women in the news media worldwide as a means to further freedom of the press. The IWMF network includes women and men in the media in more than 130 countries worldwide.

Source: www.wavuti.com/4/post/2010/05/congratulations-to-victy-ntetema.html

SHUKRANI ZA PEKEE KWA DADA SUBI KWA KUTUSHIRIKISHA HILI NA PIA KWA DADA VICKY NTETEMA KWA KAZI ULIYOIFANYA KUIBUA MAOVU HAYA

Shule Shule Shule... Twafunzwa tufunzapo

Nimekuwa "nikihubiri" kuhusu SHULE hii tuiitayo blogu. Ambayo katika kila uandikalo, kuna uandikiwalo ambalo litakuwa na uelimishaji kwa kila mwenye mtazamo chanya. Na kuna wanaojitolea kuelimisha wakiwa wanaficha utambulisho wao, na wengine wanakuja wazi kuelimisha kile wanachoamini na kukielimisha kwa nguvu zote.
Na leo napenda kuleta maoni ya Kaka Evarist Chahali aliyotoa kwenye ileeee mada niliyoandika kuwa Blog zetu na "maradhi" ya Bongo flava (irejee hapa).
Kaka Chahali anaelimisha na kuendeleza mjadala akisema
"Naomba kukupongeza kwa uchambuzi huu makini.Pamoja na pongezi hizo,naomba uniruhusu kutofautiana nawe japo kidogo.Kwa mtizamo wangu (unaoweza kuwa si sahihi) lengo la kuanzisha blogu linabaki kuwa miliki ya bloga husika.Kwa mantiki hiyo,bloga anaendelea kuwa na haki na uhuru wa kuendeleza maudhui ya awali ya kuanzisha blogu yake kama ambavyo anavyokuwa na uhuru wa kubadilika kulingana na sababu mbalimbali (kwa mfano kwenda na wakati,kutanua hadhira,nk).Blogu si Biblia au Koran kwamba kubadili cbochote ni kukufuru.
Pia,tunaweza kuwa hatuwatendei haki bloga 'wanaoendeshwa na kusaka umaarufu,au 'wanaoiga'au 'wanaokurupuka',nk kwa vile kile tunachoita kusaka umaarufu,kuiga au kukurupuka kinaweza kabisa kuwa ni sehemu ya ubunifu wao.Na katika 'kuiga' huko inawezekana wanachofanya ni kufuata mkondo wa vinara wa fani.Tunashuhudia kwenye soka,kwa mfano,wanasoka chipukizi wanavyojitahidi 'kuiga' idols wao kama Beckham,Messi,nk.Kama 'kuiga' huko kunaweza kuzaa maendeleo basi nadhani ni jambo jema.Kumuiga mzee wa changamoto ili nami niweze kuitumikia jamii kiufanisi au haya nikidhi tu mapendezeo yangu si jambo baya (kwa mtizamo wangu).
Halafu,ninahofu kuwa bloga 'wageni'au'wachanga' wanaweza kutuona hatuwatendei haki 'kwa kuhukumu kazi zao'.Wanaweza kujiuliza tumepata wapi mamlaka ya kuunda vigezo vya ubora wa blogu (kwa kuzingatia mazingira yetu).
Sambamba na hilo ni swali nililowahi kujiuliza huko nyuma: tunablogu kwa ajili ya jamii au kwa ajili yetu?Jamii ni mkusanyiko wa watu wenye akili,upeo,ladha na matamanio tofauti,na kwa hali hiyo ni vigumu 'kuiridhisha' yote.Nafsi,kwa.upande.mwingine,ni moja.Ni mimi au wewe au yeye.U-moja huu unarahisisha kuridhika.Ni rahisi kuridhisha nafsi yangu kuliko ya mtu mwengine au kundi.Kwa.mtizamo wangu,alimradi bloga 'hachafui hali ya hewa' basi anaweza kufanya 'ile kitu roho yake inapenda' iwe ni kufuata nyayo ( 'kuiga') nguli wa fani au 'kuja kivyake'.
Binafsi sina tatizo na kukopi na kupasti alimradi huyo 'mkopaji' anaweka angalizo kuwa alichoweka hapo ni kwa mujibu wa au hisani ya flani.Hivi magazeti,radio na televisheni si ndio wanaongoza kwa kukopi habari?Na si kwamba kila mara wanafanya hivyo kwa kupenda bali habari zao nyingi hupatikana kutoka chanzo kimoja,hususan 'wire services'.Si ajabu kukutana na Habari kutoka Reuters au AFP ikiwa kama ilivyo kwenye magazeti,tv,redio na tovuti mbalimbali duniani.Sanasana itakuwa imeongezwa maneno mawili matatu au picha.Nafahamu kuwa neno linalotumika ni subscription lakini kimsingi ni copy and paste.
Tukumbuke kuwa si kila anayeanzisha blogu anataka kuelimisha,kuhabarisha,kuburudisha au kukosoa.Kwa vile kimsingi blogu ni mithili ya personal diary japo kwa mazowea tu inatarajiwa kuwa kama chombo cha habari basi kilicjomo humo kinategemea zaidi matakwa ya mmiliki kuliko sisi 'tunaoamua wenyewe kutembelea diary husika' (pengine diary si neno mwafaka lakini nadhani nimeeleweka).Kama kilichomo humo hakiendani na ladha,matarajio au matakwa yetu,tunaachana na diary hiyo.
Nimalizie kwa changamoto ndogo.Ukitafuta blogu zinazojihusisha na teknolojia ya android,kisha ukatembelea japo 20 tu,naamini utaafikiana nami kuwa exclusive content kwenye chapisho ina ugumu."

Tuesday, May 11, 2010

Isaya Zephania Yunge......Kijana wa sasa, kwa Tanzania ya sasa

Destiny.
Nimekuwa nikisema kuwa MPAKA KESHO ITAKAPOHESABIKA KUWA LEO, BASI VIJANA HATUTAENDELEA. Maana kubwa ya sentensi yangu ni kuwa mambo ya msemo wa VIJANA NI TAIFA LA KESHO hauna maana.
Hauna maana kwangu kwa kuwa wazee wanaendelea kung'ang'ania madaraka mpaka vijana wanapoelekea kuuacha ujana na wakati huo ndipo tunapojikuta tumekosa la kufanya kwa kuwa tulikuwa tukisubiri hiyo KESHO ambayo haijawahi kufika na haitafika. Hakuna ubishi kuwa wazee wengi na hasa kwenye siasa za nyumbani na ambao ndio wanaoonekana kuhusika katika maamuzi mengi yahusuyo Taifa na Vijana wanategemea saana uzoefu na wanatueleza kuwa hatuna UZOEFU katika kushauri na kuamua, lakini wanasahau kuwa "The trouble with experience is that by the time you have it you are too old to take advantage of it. " — Jimmy Connors
Lakini kati ya watu wachache ambao wameonesha kuanza harakati za kuibadili dhana hiyo potofu na kuamua kujikita katika kuibadili jamii yetu akiwa na umri wa ujana ni Kaka mdogo ISAYA ZEPHANIA YUNGE. Ni kijana mdoog ambaye ameweza kuwa na mipango halisi ya kuibadili jamii yetu. Niliweza kuwasiliana naye kwa njia ya mahojiano ya maandishi na kisha kupanga kufanya mahojiano ya sauti na kuyarekodi kwa njia ya simu. Mipango yangu ilishindikana ila alikuwa mkarimu saana kunieleza kila nilichohitaji kujua kuhusu yeye kwa njia ya maandishi na nikaona nishirikiane nanyi katika kipengele hiki cha MWANANCHI MIMI ambacho ni maalum kwa wale waliokwenda "mwendo wa ziada" kuiokoa jamii.
Isaya alizaliwa 23/03/1990 katika kijiji cha Nyangunge, wilaya ya Magu, mkoani Mwanza akiwa ni mtoto wa kwanza katika kwa wazazi wake ambao walitengana akiwa na miezi michache tangu kuzaliwa. Akielezea anavyokumbuka maisha yake ya utotoni, anasema "nikiwa na umri mdogo mama yangu alilazimika kunipeleka kuishi na bibi yangu wilayani Magu ambapo Bibi alikuwa akijishughulisha na Siasa, Kilimo na Ufugaji hivyo kukua na kulelewa hapo na bibi yangu ambaye alinifunza kilimo cha mpunga na ufugaji wa ngombe, mbuzi na mondoo, nikiwa na umri wa miaka mitano tayari nilikuwa Mchungaji bora wa Mbuzi na Mhamiaji wa ndege katika mashamba ya Mpunga."
Harakati za Isaya katika kuikomboa jamii ziliznza mwaka 2005 ambapo alianza kufanya kazi za kujitolea katika shirika lisilo la kiserikali liitwalo KULEANA na akiwa hapo, walikuwa na kikundi cha watoto kilichoitwa SAUTI YA WATOTO,ambacho kiliwawezesha kupata mafunzo mbalimbali ya haki za watoto na wajibu wao na kupitia mafunzo hayo, waliweza kuelimisha jamii kwa njia ya redio, ambapo walikuwa na kipindi kila Jumamosi katika kituo cha Radio free Africa ya jijini Mwanza, kipindi ambacho kilikuwa kinafadhiliwa na UNICEF.
Hata hivyo, nia ya kujielimisha haikuishia hapo, kwani Isaya amenieleza kuwa "mwaka 2006 nilipata mafunzo ya uelimishaji rika juu ya masuala ya UKIMWI chini ya mradi ulioitwa Abstinence and Behaviour Change to Youth (ABY) uliokuwa unadhaminiwa na International Youth Foundation. Tangu hapo nimekuwa nikifanya kazi kama muelimishaji rika wa kujitolea mashuleni na katika jumuiya na kwa sasa natoa zaidi mafunzo hayo ya UKIMWI na stadi za maisha kwa Watoto wa mitaani , vile vile kupitia kipindi cha redio-katika redio iitwayo Passion FM nimeweza kutoa mafunzo hayo kwa hadhira kubwa zaidi juu ya masuala ya UKIMWI, stadi za maisha, na haki za watoto. "
Mwaka 2006, Kaka Isaya alichaguliwa na wajumbe wa baraza la watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo, ambalo liko chini ya usimamizi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Akiwa na washiriki wenzake wa Junior 8
Mwaka unaofuata (2007) alichaguliwa kuwakilisha Tanzania kama UNICEF-Youth Ambassador katika Mkutano wa Junior 8 ambao ni mkutano tangulizi wa vijana wa nchi za G8, katika mkutano huo uliokuwa na vijana 75 kutoka nchi za G8 na nchi zinazoendelea ambazo ni Brazil,China, Tanzania, Sierra Leone, Central Africa Republican, Ethiopia, India, Moldova, Algeria na Cameroon ambapo nchi hizi zilitoa vijana 10 ikiwa ni mmoja kila nchi. Anaendelea kunijuvya kuwa "nikiwa katika mkutano huu nilichaguliwa kuwa UNICEF-Africa Youth ambassador na nikahudhulia kikao cha G8 ambapo nilipata nafasi ya kuongea na kuwakilisha maoni yangu."
Akiwa na viongozi George Bush na Tony Blair katika mkutano wa G8
Mwaka 2007, Isaya alianzisha shirika lisilo la kiserikali liitwalo JUNIOR 9 FOUNDATION, ambalo linashughulika na watoto wa mitaani na waishio katika mazingira magumu. "Junior 9 Foundation inawasaidia kwa kuwapeleka shule watoto wa mitaani ili wapate elimu ya msingi na kutoa vifaa na mahitaji ya shule kwa watoto waliokatika mazingira magumu."
Kwa hakika niliguswa, nimeguswa na nimefurahishwa saana na HARAKATI za Kaka mdogo Isaya na nimeona ni vema kumleta hapa KUENZI juhudi zake za kuibadili jamii akiwa na umri muafaka.
Kwa sasa anasoma kidato cha tano TAQWA HIGH SCHOOL-Ghana Campus.
HEKO KAKA ISAYA NA MUNGU AKUJAALIE
Naomba nisindikize pongezi zangu kwa UJANA WA LEO wa Isaya na kibao hiki kiitwacho YOUTHS TODAY

Saturday, May 8, 2010

Wakati nawaza wawazayo "wapakwa mafuta"

Hivi hawa "wapakwa mafuta" wanawaza(ga) nini?
"Tired of leaving church feeling like I've just been robbed
2 hours of rambling not much mention of God"
Hii ni nukuu ya wimbo wake Tanya Stephens uitwao WHAT A DAY (urejee kwa undani hapa) ambayo inaendelea kuwa na ukweli katika makanisa yetu ya "kileo"
Binafsi mimi ni muumini. Tena muumini mzuri wa kiKristo ambapo huwa najivunia yale nijifunzayo kanisani mwetu. Na (labda kwa kuwa ni dhehebu), bado kuna muelekeo wa meengi nifunzwayo toka Tanzania mpaka hapa U.S.A. Lakini kama nilivyowahi kusema, linapokuja suala la IMANI, kunakuwa na "upenyo" mkubwa saana wa kila mtu kuhubiri kile aaminicho na wakati mwingine kwa "mtindo" aaminio ndio wafaa kuwakilisha na kuwasilisha mahubiri yao.
Ni haya yanayonifanya kuwaza kama sote twamuamini Mungu mmoja na hata kama wakristo wote wanapelekwa sehemu moja kwa kutumia mahubiri tofauti na hata njia tofauti za kuwafanya wafike mbinguni.
Na "wakati nawaza wawazayo wapakwa mafuta hawa", huwa naishia kujiuliza WALIWAZA / WANAWAZA NINI kuhubiri hivi ama kwa mitindo hii?
Watazame wachache hapa chini kisha uwaze nami
Tuanze na "Nabii" Tito ambaye yeye anahimiza ndoa za mitara na unywaji pombe.


Turejee hapa Marekani tukutane na Rev. Fred Phelps


Yawezekana huyu ana yake ya kumfanya aseme kivyake na kuwakusanya aaminio ni wake. Lakini sasa tuangalie upande mwingine wa huyu "anayekusanya kondoo" wagomvi kwa namna ya kipekee. Angalia chini aina nyingine ya "UTUMISHI" kisha jiunge nami kufikiria "alipokuwa anafikiria kuanzisha hili, ALIWAZA NINI?"


Labda tuwaangalie hawa walioamua "kuwafikia wengine" kwa style ya kipekee kwa namna hii. Hebu tuanze na Pastor Willie Ramos ambaye najitahidi kuwaza anapoandaa "somo" ama Ibada ya siku ANAWAZA NINI?


Ama huyu anayeonekana "kuwakuna" zaidi waumini wake kwa mtindo wake wa kuwafikishia neno la mungu. Ukiweza anzia dk 1:06 na umalizapo jiunge nami kuwaza "ALIWAZA NINI" kuanza mahubiri kwa mtindo huu?


Na vipi kuhusu huyu mhubiri anayehubiri kuhusu ushoga na usagaji?

Najua yako mengi ya kujiuliza kuhusu namna ambavyo hawa waliopewa dhamana ya kulichunga kundi la waumini wanafanya maamuzi yao. Na si kwa yale waongeayo na namna waongeavyo, bali hata kwa namna waruhusuvyo mambo mengine kutendeka chini ya himaya ama maamuzi yao. Labda jaribu kufikiri huyu aliyemruhusu huyu "mwimbaji" kuingia madhabahuni na kuimba aliwaza nini? Labda ilikuwa ni ibada ya "watu maalum", ama ni yeye "aliyejitengeneza" ili kuondoa aibu. Lakini katika hali ya kawaida, unaweza kuwaza kama alikuwa sawia na kama waliomkaribisha waliwaza sawasawa.
Sikiliza uimbaji huu hapa chini


***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

Thursday, May 6, 2010

Them, I & Them......TRINITY....Lucky Dube

Eneo la tukio "likisafishwa" kwa gari-shukiwa likiondolewa eneo la tukio baada ya kuteguliwa bomu lililokuwa ndani mwake
Photo: Giancarli for NYDailyNews.com
Mwishoni mwa juma lililopita kulitokea jaribio la kulipua "milipuko" ambayo kwa hakika ingeathiri maisha ya watu wengi (hata kwa kuwashitua na kuwaogofya kama isingeua ama kujeruhi) na mpaka sasa mshukiwa mkuu amekamatwa kuhusiana na jaribio hilo. Hili si jaribio la kwanza kushindwa kufanikiwa (kwa wategaji) tangu kutokea milipuko ya Septemba 11, 2001.
Lakini hapa swali laja kuwa kwanini bado twaendelea kuweka maisha ya wasio na hatia katika hatari? Ni kwanini licha ya kupigana nao huko wanakoaminika kuwepo, kwanini wanaendelea "kuchipuka" kila mahala ulimwenguni? Luciano aliwahi sema kuwa "they kill trhe wicked but still more rise. Without proper justice we shouldn't be suprised". Na hapo tunaendelea kujiuliza kama hata wao kujaribu kuua wananchi na mataifa kujaribu kuwaua ni sehemu ya suluhisho. Ni hapa ninapomkumbuka Nasio aliyesema kuwa "War is not the solution. Never was, never will it be so". Na hapa ni kwa lolote lile.
Ila ninalohisi kuwa la kipekee katika hili la sasa ni kama hawa wahusika wa pande mbili wanajua wanachopigania. Kuna uwezekano kuwa kama kungetokea kukawa na kuelewana na kueleweshana juu ya u-mimi na u-wao, mambo mengi yangemalizika kwa mmwagiko mdoogo saana wa damu. Lakini nahisi SI MAGAIDI WALA MATAIFA YAPAMBANAYO NAO WANAOJUA UPANDE WA PILI UKO VIPI, UNAHITAJI NINI, UHESHIMIKE VIPI, WACHUKIZWA NA NINI NA WAWEZA KUSHIRIKIANA NAO VIPI KUILETA AMANI AMBAYO WOTE WANATAKA KUISAKA KWA NCHA YA UPANGA.
Ni fikra hizi zinazonirejesha kwenye wimbo huu wake LUCKY DUBE uitwao TRINITY ambao unazungumzia mambo yafananayo na haya.
Japo aliimba wakati wa harakati za kusaka amani kutoka kwa ubaguzi na ukoloni, lakini MAUDHUI NA NJIA ALIYOSHAURI KAMA SULUHISHO IKINGALI NA UWEZO WA KUTATUA HATA HILI LA SASA.
Ukimsikiliza anapoanza wimbo wake anaanza kwa kusema "I'm sleeping with my one eye open 'cause I think you gonna come for me. You're sleeping with your gun in hand, you think I'm gonna make my move..." Na huu ndio UKWELI wa maisha yaliyopo katika pande hizi mbili za ulimwengu niuzungumziao ambao ni wa mataifa yanayopambana na kile waitacho ugaidi na hao magaidi. Haya mataifa makubwa hayaishi kuchunga kila upenyo wa mawasiliano wakihisi magaidi watawaingilia, ilhali hao waitwao magaidi wanahaha kila walipo wakihisi watashushiwa shambulizi. Lakini kinachosikitisha ni kuwa unaposikia habari za upande wa pili, zinakuwa zimepotoshwa kiasi ama kuongezewa jambo (kwa makusudi ama bahati mbaya) kwa nia ya kuungwa mkono. Na kwa bahati mbaya kuna ambao wanakwenda kupigana "kwa sababu hizo wanazoambiwa ambazo wakati mwingine si sahihi". Sasa ni kwanini kusiwe na uwezekano wa kuepusha haya kwa kuweka ukweli bayana kuhusu kila upande (hasa kwa kuwa kuna ambao tumeshaona uongo ulivyotuingiza matatizono) na kuepusha yale yanayotugombanisha yasiyo ya kweli na pengine kuungana kama alivyosema "now that we know where we went wrong, Let's unite ".
Katika wimbo huu, yanaongelewa yaleyale yaliyohusika katika kugombea AMANI NA USAWA kwa njia ya kuelewana.
Msikilize LUCKY DUBE huku ukimsoma katika mafunzo mazuuuri saana akisema TRINITY

I'm sleeping with my one eye open
'Cause I think you gonna come for me
You're sleeping with your gun in hand
'Cause you think I'm gonna make my move

I've been chasing white people all my life
You've been chasing black people all your life
Now that we know where we went wrong,

it's time some truth came out here

You going to educate me about white people
I will educate you about Black people

and we'll unite
That's why they call me trinity
And my game is unity

Chorus
Trinity, unity

My brothers have been chasing racists all the time
Your brothers have been chasing freedom fighters all the time
But at the end of the day
We didn't know much about each other yeah

When you saw a black man you saw a criminal,
When I saw a white man I saw an oppressor
But now that we know where we went wrong
Let's unite

You will educate me about white people
I will educated you about black people

That is why they call my trinity
Cause my game is unity

Chorus till fade...


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA