Tuesday, November 30, 2010

Kosa la kwanza la Rais Kikwete......

ONYO: Usisome kama nia yako ni kusoma sio KUELEWA. Rais Jakaya Kikwete akihutubia taifa punde baada ya kuapishwa kuongoza nchi kwa awamu ya pili. Photo credit: Chingasite
Ni kweli kuwa UCHAGUZI UMEMALIZIKA na sasa ni harakati mpya za kuanza KUIJENGA Tanzania yetu katika muhula wa mwisho wa awamu ya nne ya uongozi wa Taifa.
MOSI nirejee ambayo nilishasema awali, NAWAPONGEZA woote walioshiriki katika mchakato wa kumsaka "kiongozi bora" atakayeleta mabadiliko yenye manufaa kwa wananchi.
Shukrani kwa
1: Walioshinda kushinda,
2: Walioshinda kushindwa (ambao wamefanya "juu chini" kutangazwa washindi)
3: Walioshindwa kushinda
Haijalishi "umeangukia" katika kundi gani hapo juu, lakini utakuwa umepata changamoto nzuri ama katika kutekeleza utakiwayo kutekeleza sasa kwa wananchi waliokuchagua, ama katika kujipanga upya kwa uchaguzi ujao kwa wanaopanga kugombea tena.

PILI, nieleze kuwa kumekuwa na MATUMAINI YA MAFANIKIO katika muhula huu. Na matumaini haya yameonekana kuwa makubwa sana. Watu wengi wametabiri UTENDAJI katika awamu hii kwa kuwa wamewekewa watu ambao hawakuwemo katika mfumo wa uongozi uliopita. Kwa maana nyingine, BUNGE LA SASA LINA MABADILIKO KIDOGO na hasa mabadiliko yaliyohusisha "kuanguka kwa vigogo" kadhaa wa chama tawala ambao hakuna aliyetaraji wangeng'olewa kirahisi na watu wa upinzani. Ilishangaza wengi kuona wagombea wa chama tawala licha ya kuwa na "viwezeshwa" vya hali, mali na "mfumo", bado waliweza kukosa nafasi walizozipigania kwa nguvu. Lakini TAFSIRI YAKE SI NGUMU.... WATU WAMECHOSHWA NA VIONGOZI WASIOWAJALI.
Lakini kwa wale ambao wanadhani "ndugu hawa" walioenguliwa ama kunyimwa ridhaa ya kwenda bungeni ndio wamekwisha kisiasa, wanastahili kufikiria mara ya pili.
Tumeanza kuona harakati za Raisi kutumia HAKI YAKE YA KIKATIBA kuteua wasaidizi wake katika nyanja mbalimbali ili kutekeleza kazi zake. Tumeshaona uteuzi wa BARAZA LA MAWAZIRI ambalo kwa heshima na taadhima niliwaomba MAWAZIRI WAORODHESHE WATATENDA NINI, VIPI NA KUFIKIA LINI? (Irejee hapa). Sijajua VIGEZO vya uteuzi huo, na wala sina hakika kama katika vyeo vya kuteuliwa kuna ambacho kina "udogo" wa utendaji ukilinganisha na ubunge. Najua wakuu wa mikoa (ambao kama nilivyosema hapa nawaona kama MZIGO KWA SERIKALI NA WANANCHI na CHANZO CHA KUDIDIMIA KWA MAENDELEO NCHINI), na pia kuna wakuu wa wilaya, kuna makatibu wa wizara, wabunge wa kuteuliwa, mabalozi n.k. Na pia tumeona ambavyo Mhe Raisi ameanza kwa kuteua wabunge ambao mmoja wa wateuliwa AMEZUA GUMZO (hapa) kutokana na kuhusishwa na tuhuma ambazo bado hazijathibitishwa kwa wananchi.
Lakini bado nawaza kama Waheshimiwa wastaafu kama Mhe. Lawrence Masha, Mhe Monica Mbega, Mhe Phillip Marmo, Mhe Getrude Mwongela, Mhe Batilda Buriani na wengine wengi hawatanyakua nafasi za kuteuliwa. Ninawaza pia kuwa kama niko sahihi (kwamba hakuna cheo cha kuteuliwa chenye udogo wa shughuli kuliko ubunge), ni kipi kitamfanya Mhe Raisi ateue watu ambao wameshindwa kuwatumikia wananchi wao ilhali wanajua fika kuwa watakuja kuwaomba kura miaka 5 ikiisha? Kama watu hawa walipuuza NGUVU YA KURA YA WANANCHI mpaka yalipowakuta ya kuwakuta, ni vipi watawajibika ilhali wanajua atakayewateua hawatamuomba kura na hataenda tena kwa wananchi kuomba kura kwa kuwa muhula wake umeisha?
SINA HAKIKA KAMA RAISI ATATEUA YEYOTE KATI YA "WALIOSHINDWA KUSHINDA" UCHAGUZI lakini pia sitashangazwa na hili japo nitasikitika sana.

Na katika kumalizia sentenzi iliyo kichwa cha habari hii, nasema.......
KOSA LA KWANZA LA RAISI KIKWETE LITAKUWA NI KUPUUZA NGUVU NA MAONI YA WANANCHI YA KUTAKA MABADILIKO IKIWA ATAWATEUA WATU WALIOSHINDWA KATIKA UCHAGUZI ULIOMALIZIKA.
Hili litakuwa kosa kama atateua yeyote kati ya walioshindwa na halitakuwa kosa mpaka atakapotekeleza kile ninachoona kina uwezekano wa kutendeka.
Mpaka wakati huo, naendelea KUFUNGA NA KUOMBA kwamba Mheshimiwa Raisi aheshimu matakwa, nia na haja ya mabadiliko iliyooneshwa na wananchi.

Na hivi ndivyo nionavyo tatizo lijalo na natunza haki ya kukosea na kukosolewa. Labda namna nionavyo tatizo ndilo tatizo.

Tuonane "NEXT IJAYO"

Thursday, November 25, 2010

Nionavyo mimi....MAWAZIRI WAORODHESHE WATATENDA NINI, VIPI NA KUFIKIA LINI?


Hakuna ambaye hajasikia BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI lililotangazwa jana na Mhe Raisi Kikwete. Maoni juu ya baraza hilo ni mchanganyiko na wapo walioonekana "kulikubali" na pia waliolipinga ama kutoridhishwa nalo.
Wengi wa waliolikubali wameonekana kukubali zaidi uteuzi wa Mhe John Magufuli na Mhe Anna Tibaijuka katika wizara zao. Ni jambo la kufurahisha kuona BARAZA LINAUNGWA MKONO na wananchi. Kuna imani ama matarajio kwamba KUTAKUWA NA MAFANIKIO kutokana na kuungwa mkono kwa baraza hili. Hizi ni dalili njema.
LAKINI pia kuna walio na shaka. Wanaosema "wengi ni walewale" na wanahisi "ushikaji" umetawala uteuzi huu..
Wacha nami nianze kuweka yale nilonayo moyoni.
KWANZA niwapongeze wanaomuunga mkono Raisi (kwani hata bila kumuunga mkono baraza "litasonga"). Na pia wale wanaopongeza uteuzi wa Mama Tibaijuka niungane nao, lakini pia NIONYE AMA KUTAHADHARISHA kuwa Mama Tibaijuka ANAINGIA KWENYE MFUMO (pengine uliomomonyoka) AMBAO UNAWEZA KUWA KIGINGI KATIKA UTENDAJI WAKE. Bado naamini kuwa utendaji wa Umoja wa Mataifa ulikuwa na mazingira mazuri ya kazi yasiyo na mchanganyo na mkanganyo wa siasa kama ilivyo Tanzania yangu. Natumai watu watakaokuja kuangalia uongozi wake wataliweka hili katika fikra.
Ni hapa ninaporejea kwenye mada kamili kuwa
KABLA HAWAJAJITAMBULISHA KWETU KAMA MAWAZIRI, NINAPENDA WAJIPANGE NA KUANGALIA NI NINI WATATIMIZA KATIKA MIAKA MITANO IJAYO NA NI VIPI WATATIMIZA HAYO KWA KUFUATA ILANI YA CCM.
MAWAZIRI hawa wanalazimika kuwa na mipango kamili. Ninachukia kuona kila miaka mitano iishapo, tunalinganisha utendaji kazi wa mtu kwa kitu tusichokijua. Sasa watueleze ni nini tutarajie miaka mitano ijayo na kisha watupe mgawanyiko wa namna watakavyotimiza hayo kwa kufuata ilani za CCM. Wananchi WANA HAKI ya kujua utekelezaji wa AHADI HIZI ZA RAISI KIKWETE.
TOVUTI ZA WIZARA KUFAFANUA KAZI ZAO...Mhe. RAISI...ATI UMESEMA WIZARA YA MAHUSIANO NA URATIBU? Labda TOVUTI ZA WIZARA zitafafanua ni nini wizara inafanya ama inastahili kufanya. Hii Wizara ya Mahusiano na Uratibu ningependa kujua inahusika kuhusianisha na kuratibu nini? Pia "Mchanyato" wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo unatuelekeza wapi? Na katika TAARIFA YA MAREKEBISHO YA WIZARA KUTOKA MWANDISHI MSAIDIZI WA RAISI imesema "wizara ya vijana imehamishwa kutoka wizara ya kazi na kuihamishia wizara ya habari kwa sababu kuu mbili. Kwanza ni kushahabiana na michezo na utamaduni,...." NINAWAZA KUHUSU MSHAHABIANO HUU. Ni kweli kuwa katika yote yawafaayo na kuwahusu vijana, Ikulu imeona mshahabiano wao na Michezo na Utamaduni tu? Si Elimu, si Sayansi na Teknolojia, si Afya, Si Uwekezaji, Si Maendeleo ya Jamii, si Utawala Bora, si Uchumi, si Utalii, si Madini, si mafunzo ya jamii si, si, si ........?
Ningependa zaidi kujua zaidi kuhusu hili
AJALI ZA BARABARANI. Ni nani atakayechukua jukumu la kushughulikia kuzuia ajali na kuratibu usalama wa wananchi? Je! Ni Wizara ya Ujenzi (Barabara na Uwanja wa Ndege), Wizara ya Uchukuzi (Reli, Bandari, Usafiri Majini) ama Wizara ya Usalama wa Raia (ambayo hata sijui imekuwa "faded" ndani ya wizara ipi? Ama ni wizara gani?
WIZARA YA UCHUMI??? Nilipowasiliana Kaka Jeff Msangi na awaza kama wizara ya fedha ndiyo ishughulikayo na masuala ya uchumi. Ama mchakato wa uchumi ama uharibifu kutokana na madini utasimamiwa na Wizara ya Fedha, wizara ya Madini ama Wizara ya Mazingira?
Kuna mengi ya kuwaza na kuchangia kuhusu baraza hili ACHILIA MBALI KUWA NA WANAWAKE 9KATI YA BARAZA LA WATU 50.

"Wacha niachie" hapa, naamini nawe utaona la kuongeza katika kuisaidia TANZANIA YANGU ISONGE MBELE
Tuonane "Next Ijayo"

Wednesday, November 24, 2010

Kwenu wapinzani. Ms'ojua ushindani na kukalia ukinzani uwageuzao "washindwani"

Photo Credit: Alternatives-Economiques Blog
Nilisikia msemo kuwa the moment you discover the "cool", is the same moment the "cool" thing loses it's "cool". Nikaambiwa haya hutokea zaidi katika biashara. Kwamba unapodhani umegundua kile ambacho hakijagunduliwa, kisichopatikana na kilicho "cha pekee", ni wakati huohuo ambao unafungua milango kwa "waigilizaji" walio wengi kukimbilia hapo na matokeo yake ule mfumo wa "supply vs demand" unafanya kazi yake.
Labda suala hapa ni lile lile kuwa HAKUNA NAMNA YA KUDHIHIRISHA KUWA UNAWEZA KUTUNZA SIRI, KWANI NI LAZIMA UISEME ILI MTU AJUE NI IPI ILIYOKUWA SIRI NA UKISHAISEMA UMESHAPOTEZA KILICHOKUFANYA UJIVUNIE...U-SIRI.
Bahati mbaya ni kwamba mifano hii ya kibiashara inaonekana kuwafikia hata "wafanyabiashara wa siasa" nchini Tanzania.
Yaani punde baada ya waTanzania kuamini kuwa WAMEWEKA UPINZANI HALISI BUNGENI, wale "wengine" wenye kuendekeza maslahi zaidi ya wananchi wamerejea kwenye upande ambao unawafanya wananchi wazidi kukubaliana na tafsiri ya Da Subi ya siasa kuwa "siasa si-hasa, bali visa na mikasa".
Tulianza kuyaona mapeeema baada ya uchaguzi pale tulipokubaliana kuwa yawezekana "Ni kweli Dk Shein kashinda..lakiniii..... labda Maalim Seif hajashindwa pia" (irejee hapa) na kikubwa tulichowaza hapo ni kama "kukubali" huku kuliendana na mahitaji ya wananchi ama mahitaji binafsi ya Maalim Seif ambayo hayakutimizwa katika chaguzi tatu zilizopita. Kisha likaja suala la kutangazwa uongozi wa upinzani Bungeni (hapa) ambapo tuliambiwa bayana kuwa "Vyama vingine vya upinzani vyenye wawakilishi Bungeni, TLP, CUF na NCCR-Mageuzi vimekataa kujunda ushirikiano na CHADEMA na badala yake, vinatarajiwa kutangaza safu yao baada ya makubaliano."
Hatujatulia, tukasikia kuhusu wapinzani kutaka kupelekana mahakamani kwa sababu za kampeni ya Kawe na sasa twaona vita ya "demokrasia" inaendelea.
SUALA HAPA SI NANI ANAFANYA NINI, BALI NI NANI NA NANI WANAPINGANA NA KUPIGANIA NINI?
Ni maadui wangapi ambao upinzani wanao na ni wangapi ambao wanaweza kuwa na namna mija ya kuwaondoa? Kama ni MARADHI, UJINGA, MALAZI NA MAISHA DUNI YA WANANCHI, ni kwanini WAKINZANI hawa hawaungani kuwateketeza?
Kama wote ni waenguka wa chama tawala na wanataka kufanya kile kinachozembewa kufanywa na chama tawala, ni kwanini wanashindwa kutafuta palipo na msimamo wa pamoja, wakaungana na kisha wakaweza kumng'oa huyo wapangaye kumng'oa?
Sasa yaonekana "vita dhidi ya matatizo ya wananchi" (ambayo ilistahili kuanza) ndio imekwisha (mpaka mwezi Juni 2015) na sasa ni "vita" ya kusaka umaarufu kwa migongo ya wenzao.
Hivi ni kweli "umoja" unatakiwa kuwepo wakati kila mmoja anasaka UTAWALA?

Sasa na huu ni ujumbe "Kwenu wapinzani. Ms'ojua ushindani na kukalia ukinzani ufanyao 'washindwani'", watu wanataka mabadiliko. Mkanganyiko wa nani anafanya nini kwa manufaa ya fulani na si wachagua si mwema. Hauzifai jamii zilizowaweka madarakani huko bungeni, wala hauifai nchi yetu kwa ujumla. Ni lazima mkumbuke kuwa nyote mwafanya harakati za kusaka maendeleo, lakini cha kusikitisha ni kuwa MWASAKA MAENDELEO KWA KUDIDIMIA UENDELEZI. Yaleyale NILIYOANDIKA HAPA
Kama ulikosa kilichoimbwa, sikiliza na kufuatilia mashairi yake chini.

"Listen people to a story that was written long ago,
Bout a kingdom on a mountain and the valley folks below
On the mountain sit a treasure, buried deep beneath the stone
And the valley people thought they'd have it for their very own.

Chorus
Go ahead and hate your neighbor, go ahead and cheat a friend
Do it in the name of heaven, you'll be justified it in the end
There won't be any trumpets blowing On the judgment day
On the bloody morning after one tin soldier rides away.

So the people of the valley sent a message up the hill
Asking for the buried treasure, tons of gold for which they'd kill
Came an answer from the mountain, "with our brothers we will share
All the secrets of our mountain, all the riches buried there."

Now the mountain cried with anger, "Mount your horses, draw your swords"
And they killed the valley people, so they won their just rewards
Now they stood beside the treasure, on the mountain, dark and red
Turned the stone and looked beneath it, "Peace on earth" that all it said.

Chorus
Go ahead and hate your neighbor, go ahead and cheat a friend
Do it in the name of heaven, you'll be justified it in the end
There won't be any trumpets blowing, On the judgment day
On the bloody morning after, one tin soldier rides away.".... x2

Kama huoni player BOFYA HAPA

Sunday, November 21, 2010

Za Kale vs Maisha ya sasa....LAU NAFASI

Jinsi miaka inavyozidi kusonga ndivyo mabadiliko katika ubora wa muziki yanavyozidi kuwepo. Kwa nchini kwetu ni kugugumizi kuzungumzia muziki kwa ujumla kama una maendeleo ama kuna maendeleo katika muziki japo wenyewe umegota.
Miongo kadhaa iliyopita Tanzania ilikuwa ikiheshimika sana katika sanaa ya muziki na wasanii wengi wakubwa Afrika waliutambua muziki wetu. Hii ilifanya kuwe na utata kiasi juu ya nani alikuwa anaiga muziki wa nani hasa katika mapigo.
Lakini leo hii tunaambiwa kuwa muziki Tanzania umekuwa. Tunaoneshwa studio utitiri na vyombo vya kisasa, lakini wasanii wachache kuliko waimbaji ambao hawawezi kufululiza masaa mawili ya tamasha kabla sauti hazijawatoka. Sijui tunaendelea kimuziki ama muziki unaendelea kivyetu?
Basi leo tuwasikilize wana Kilwa Jazz. Moja kati ya bendi zilizofanya vema saana. Mtandao shirika wa BONGO CELEBRITY katika bandiko hili la wimbo wa ROSE WAUA, umeeleza historia fupi ya bendi hii nami nainukuu. Ilisema bendi ya Kilwa Jazz ilianzishwa "tarehe 15 Julai mwaka 1953 na kundi la wanamuziki waliokuwa wanatokea Kilwa na waliojimega kutoka Tanganyika Jazz Band.Hao waliongozwa na Ahmed Kipande na kaka yake Hassan Kipande (walihamia jijini Dar-es-salaam wakitokea Kilwa katika miaka ya 1940s,Hassani alitangulia mjini). Huyu Ahmed nasikia alijifunza mwenyewe kupiga Saxaphone. Aliinunua moja kuukuu kutoka kwa mlami mmoja aliyekuwa anafanya kazi Barclays Bank,akajifunza mwenyewe.Dah! Baadaye yeye na kaka yake wakajiunga na Tanganyika Jazz Band iliyokuwa na makao yake makuu pale New Street(siku hizi Lumumba Street).Kaka yake,Hassan,alikuwa anapiga gitaa.Hao walibakia na Kilwa Jazz mpaka ilipovunjika mwaka 1967.

Ingawa mwanzoni Kilwa Jazz ilianzishwa na watu waliokuwa na asili ya Kilwa na marafiki zao zaidi,baadaye wanamuziki kutoka pande mbalimbali walijiunga na Kilwa Jazz.Kufikia mwaka 1966 ilikuwa na wanamuziki takribani 26(15 wa bendi “A” na 11 Bendi “B”) na wanachama zaidi ya 50 wakiwemo baadhi ya viongozi enzi hizo.Usishangae,enzi hizo bendi zilikuwa na wanachama. Katikati ya miaka ya 60s Kilwa walihamia katika jengo lililokuwa linaitwa Madobi pale Kariakoo kuelekea Jangwani. Wakati huo bendi kubwa zilikuwa Western Jazz Band,Dar-es-salaam Jazz Band na wenyewe Kilwa Jazz Band."

Tukumbuke kilio cha Wana Kilwa Jazz waliokuwa wakiumia rohoni kwa kuhitaji nafasi ya kusema na fulani kidogo.
Burudika na elimika kwa kibao hiki
Lau Nafasi

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

Saturday, November 20, 2010

WALIOGOMEA MIDAHALO....Wengi wao ama wana UJINGA, ama wamejawa DHARAU

ONYO: USISOME HAPA KAMA
1: WAKASIRIKA KABLA YA KUFIKIRI
2: UNAAMUA KISHA UNAFIKIRIA ATHARI
3: HUPENDI KUJUA UKWELI HATA KAMA UKWELI NDIO UPENDO

"Speak the truth and speak it over. Love God and leave, is my only destination." NASIO
Tafsiri ya UJINGA niliyonayo ama niliyoambiwa (na ambayo naisimamia) ni ile isemayo kuwa mjinga ni MTU ASIYEJUA, NA ANAJUA KUWA HAJUI. Kwa tafsiri hii, ina maana UJINGA ni hatua moja bora kutoka UPUMBAVU na iliyo rahisi kuirekebisha kwani aliye mjinga anaweza kurekebishika akiamua kuufanyia kazi ujinga wake.
Ina maana kwa tafsiri hii ya Ujinga, naamini kuwa wabunge wa CCM (ambao waligomea midahalo) walitambua wazi kuwa walitakiwa kueleza sera zao kwa wananchi na kuzipambanisha ili kuweza kuwapa nafasi wananchi kutambua aliye bora kwao. Lakini KWA AMRI TOKA LUMUMBA (makaoni mwa chama), tena toka kwa watu ambao hawajui mahitaji ya asilimia kubwa ya wananchi, wagombea hawa WAKAKACHA midahalo kwa kisingizio cha kuwafuata wananchi huko walipo. Suala si kuwafikia, bali ni KUWAPATIA ALIYE BORA KWA MATATIZO YAO. Na nina hakika wale WALIOOGOPA midahalo walikuwa hawajui namna ya kuwakomboa wananchi wa na walijua fika kuwa hawajui (rejea tafsiri ya ujinga) na kwa kuwa wao hawakuwa pale na hawako pale kumfaa mwananchi zaidi yao wenyewe, wakaona wafanye lililo bora kwao nalo ni kupanga mikakati ya kuchaguliwa hata kama hawatakuwa na manufaa kwa wananchi wao kama wale ambao wangepambanisha nao sera.

Kinachokera zaidi ni namna WANAVYOJIDAI kupata "ushindi wa kishindo" na kusingizia kuwa ushindi huo watokana kukubalika kwao. Hawa watu wanajisifia kufaulu bila kufanya mtihani. Ama kwa uhalisia zaidi niseme wanajivunia KUSHINDA KWA "KUTAZAMIA".
Nafarijiwa na Nasio Fontaine ambaye katika wimbo wake DANGEROUS (usikilize mwisho wa post hii) aliimba akisema "...i heard your speeches,... your empty promises (promise is a confort to a fool), but now that i know, your words are dangerous"
Lakini siamini kuwa wabunge wote wako hivyo. Siamini kama wote hawakuwa na suluhisho la matatizo ya wananchi. Siamini kuwa wote walikuwa hawapendeki. Siamini kuwa wote ni WAJINGA. Ila kwa wale wasio na sifa hizo mbaya hapo juu, na ambao wangeweza kuwadhihirishia wananchi kuwa wao ndio wanawafaa na wakaamua kutofanya hivyo basi hakuna ubishi kuwa WAMEWADHARAU WANANCHI WAO

Wameona hakuna haja ya kutekeleza haki ya kikatiba ya wananchi kwa kuwapa nafasi ya kuchuja kile waaminicho na wafikiriacho ukilinganisha na wenzao. Hii si dharau kwa wananchi tu, bali kwa nchi.
Na kama nilivyoonya hapo awali, usisome hapa kama huna KIFUA cha kuukubali ukweli. Na huu ni ukweli toka katika upande wa wahitaji, upande wa wasio na tumaini na upande ambao ulikuwa na imani na watawala hawa. Kama alivyosema Lucky Dube kwenye wimbo wa SOLDIRES FOR RIGHTEOUSNESS kuwa "We are the soldiers for righteousness. And we are not sent here by the politicians you drink with. We' re sent by the poor. We' re sent by the suffering. We' re sent by the oppressed"
Ni ukweli huo ambao twauona na kuusimamia sasa. Ni wakati wa kuwawajibisha waheshimiwa mliongia madarakani na naamini hakuna ubishi kuwa KWA KILA JEMA MTAKALOTENDA TUTAWAPONGEZA NA KWA KILA BAYA MTAKALOTENDA TUTAWAKOSOA. Kama isemavyo fulana hii hapa chini, tunasimama katika kilicho sahihi na si kuendekeza "mapinduzi" ya wasiojua uhitaji wa wahitaji wao.
Labda niwe wazi kuwa, sasa ni wakati ambao tutaanza KUWEKANA SAWA na kurekebishana hasa katika kipengele (label) hii ya POLITICS FIX (kama ambavyo nataraji mnirekebishe) na hii itakuwa ni njia moja muafaka na muhimu katika kulikomboa taifa.
Na kwa WABUNGE VIJANA, wale wapya ambao mlionekana kuwa na "UJANA WA MAWAZO" mtambue kuwa kuwepo kwenu hapo kumekuwa tumaini kubwa kwa wengi, kwa hiyo kushindwa kuwakilisha vema na kujikuta mnaingia katika "MFUMO WA UZEE WA MAWAZO" ULIOWACHOSHA WANANCHI mtajishushia imani kwao. Japo wapo ambao mmeshaanza hilo.
Mfano mzuri ni mwanablogu ninayeheshimu kazi zake aliyegeuka kuwa m'bunge Dr Faustine wa Faustine Baraza ambaye sasa ni m'bunge wa Kigamboni, alikuwa mkosoaji mkubwa wa matendo ya serikali na chama, aliandika kuhusu ziara za Rais na mambo mbalimbali, lakini alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge akaamua kuifunga blogu ambayo aliitumia kuanika uozo wa "WENZAKE WA SASA." Ukurasa wake huu hapa ulio na kumbukumbu za aliyokuwa akiyasema akiwa nje sasa umewekewa KUFULI. Nilipomuuliza katika ukurasa wake wa Facebook alinijibu kuwa alikuwa amebanwa na mambo ya kampeni lakini angeurejesha hewani punde. HAKUTIMIZA AHADI YAKE. Sasa kafungua ukurasa mpya ambao naamini utaendana na matakwa ya watawala wake kuliko wananchi aliokuwa akiwatetea kwa dhati.
NI WAKATI WA KUWEKA MBELE MASLAHI YA WANANCHI NA SI CHAMA
Tumsikilize Nasio akitukumbusha kuwa THEIR WORDS ARE
DANGEROUS

NA HIVI NDIVYO NIONAVYO TATIZO. NAMI NATUNZA HAKI YA KUKOSEA NA KUKOSOLEWA.LABDA NAMNA NIONAVYO TATIZO NDILO TATIZO

Edwin Beatus Macha Memorial Day

Taarifa toka ukurasa maalum wa blogu maalum iliyofunguliwa kwa ajili ya kumbukumbu ya Kaka Edwin Macha (hapa), inasema
"Wapendwa, Jumamosi ya Novemba 20, 2010 ndio siku maadhimisho rasmi ya kumbukumbu ya kifo cha mpendwa wetu yatafanyika.

Yataanza saa 3:00 Asubuhi katika ukumbi wa M1, na kufuatiwa na maonesho mbalimbali ya kumuenzi, kukiwepo na 'Presentations' kutoka kwa watu mbalimbali na Law Sociey-SAUT.

Pamoja na kuhudhuriwa na wanachuo, jamaa na marafiki, wazazi wa Edwin pia watahudhuria, wakiambatana na ndugu wengine. Wazazi pia watapata fursa ya kuelezea maisha ya Edwin kwa ufupi na mkasa mzima uliopelekea mauti yake.

Tafadhali, mjulishe na mwenzio kuhusu kumbukumbu hii muhimu ya mtu muhimu, mpendwa wa mioyo yetu.

Roho Yake Ilazwe Mahali Pema Peponi.......... AMINA."


Taarifa za kifo cha Kaka Edwin na zile kuhusu mazishi yake zilipata andikwa kwa undani HAPA kwenye Blogu ya MO DEWJI na kisha barua toka kwa mmoja wa rafiki zake kupitia tovuti ya WAVUTI ilieleza mengi na kuuliza maswali kama ilivyonukuliwa HAPA

Thursday, November 18, 2010

Ni zipi athari za mitandao ya kijamii kwenye chaguzi zetu???

Credit: Simon Whatley
Nimewaza kwa kina namna ambavyo kusambaa kwa mitandao ya kijamii KUNAATHIRI michakato ya uchaguzi barani Afrika.
Hakuna ubishi kuwa mitandao hii imekuwa na ATHARI (zaweza kuwa nzuri ama mbaya) kwa jami zetu lakini bado nawaza NI IPI UIJUAYO?
Tunaona namna ambavyo wagombea wanatumia mitandao kama Facebook kukusanya uungwaji mkono, lakini kinachoweka shaka ni uelewa na uhalali wa waungaji mkono ambao wengine si halisi ama hawatumii majina na utambulisho halisi hivyo kutojua wako wapi na wanataka nini?
Lakini pia tumeona namna ambavyo matumizi ya mitandao kama YOUTUBE yanavyoweza kuepusha kero za polisi kwa kurekodi watendacho. Kakangu Chacha Ng'wanambiti aliandika kuwa kwa mara ya kwanza ameona Jeshi la Polisi likituliza ghasia bila kukiuka haki za binadamu, nami nikamjibu ni sababu ya Youtube..
Unadhani huyu kaka hapa chini angefanywaje kama kusingekuwa na video kamera? Si mnakumbuka "mbiringidhano" uliowakumba wa Zanzibar mpaka video zao "zikanyofolewa" kwenye mitandao ya kijamii?
Credit: The LHR
Na ndio maana nauliza kuwa NI ZIPI ATHARI (CHANYA NA HASI) ZA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA CHAGUZI ZA AFRIKA???

Wednesday, November 17, 2010

Eid Mubarak

Kwa niaba ya wana-CHANGAMOTO WOTE, napenda kuwatakia waumini wote siku njema ya Eid na baraka tele ziambatanazo nayo EID MUBARAK

Sunday, November 14, 2010

Manny Pacquiao.......mkanda wa 8, katika uzito wa 8 tofauti

Manny Pacquiao akisherehekea mkanda wake katika uzito wa Super Walter baada ya kumshinda mpinzani wake "mgumu" Antonio Margarito.
Photo Credit: Getty Images via Yahoo Sports!

Hili ndilo limfanyalo Manny Pacquiao aitwe KING OF POUND FOR POUND. Yaani kwa tafsiri isiyo rasmi ni MFALME WA UZITO MBALIMBALI. Usiku wa kuamkia leo ameweza "kumvuruga" mpinzani wake Anthonio Margarito katika pambano la kugombea mkanda wa World Boxing Council super welterweight katika pambano lililofanyika mbele ya mashabiki 41,734 waliojitokeza ndani ya uwanja wa Cowboy. Hili lilionekana kuwa kati ya mapambano magumu zaidi kwa Pac-Man ambaye wengi walisema hajawahi pambana na "kichwa ngumu" kama Margarito ambaye jana aliingia uwanjani akiwa na "faida ya urefu wa inci 5 na pia paundi 17 zaidi ya Manny.
Paquiao ameshakuwa bingwa wa dunia katika uzito wa paundi 112, 122, 126, 130, 135, 140, 147 na usiku wa kuamkia leo akatwaa taji la uzito wa Paundi 154
Na hizi hapa chini ni dodoso za pambano hilo toka Yahoo Sports

Kisha msikilize alipohojiwa na ESPN baada ya pambano

NA SASA TUNAJUA KWANINI FLOYD MAYWEATHER ANAMKIMBIA BONDIA-MWANASIASA HUYU WA UFILIPINO

Saturday, November 13, 2010

HONGERA TOVUTI YA BUNGE

Labda na nyingine za serikali zitaiga mfano huu....
UKURASA WA BUNGE
Nimekuwa mkereketwa mkubwa wa namna ambavyo tovuti za vyombo ama vitengo vya serikali zinavyopuuzwa na kutokwenda na wakati. Hili ni kuanzia Ikulu mpaka kwenye balozi zetu.
Aprili 19 nilipotoa maoni kwenye post hii ya Da Subi, nilisema "Ingia TOVUTI YA IKULU (http://ikulu.go.tz/)uone utakachokutana nacho. Anyway, hao wako busy, basi twende kwenye SHIRIKA LA UTANGAZAI TANZANIA (http://www.tbc.go.tz/)ambayo ilikuwa hewani kwa wiki moja baada ya hapo iko matengenezoni kwa miezi sasa. Who cares.
Lakini zinazofanya kazi nazo umeona updates zake? Angalia hii ya Idara ya Mawasiliano Ikulu (http://mawasilianoikulu.blogspot.com/)ambayo licha ya Rais ambaye ni msafiri kuliko uhitaji, bado updates zao ni za kusikitisha.
Anyway, labda hilo si tatizo. Kuna ambao wanaweka HABARI ZA UONGO. Kama nilivyoandika kwenye post yangu ya leo kuhusu tovuti ya UBALOZI WA TANZANIA HAPA MAREKANI. Nimeiona web yao baada ya kukutana na maelezo haya ya Uncle John Kitime aliyesema "Umekosa website za vichekesho? Basi google Tanzanian Embassy USA, kisha fungua ukurasa wa Embassy of Tanzania, fungua About Tanza...nia, halafu fungua People and culture hapo ndo utajua kumbe Ze Comedy wako wengi. Je ulijua kuwa Zouk na ndombolo ni tradional music wa Tanzania? Je ulijua kuwa Pilau kizungu ni wild rice? Je... ulijua chapati ni bread? Halafu kuna michapo mingine kuhusu mtunzi wa wimbo wa Taifa nk"
Isome hapa (http://www.tanzaniaembassy-us.org/tzepeo.html)
Labda nikwambie kaka kuwa ukitaka kujua yanakoanzia haya, basi angalia tovuti hizi za vyuo kama zilivyoelezwa na mdau hapa (http://issamichuzi.blogspot.com/2010/02/yaaawnnext-please.html)
NI MWENDO WA KINYONGA, LAKINI TUTAFIKA TUUUUU!!"

Lakini leo nilipokuwa nawasiliana na Kaka Jeff Msangi, tukajadili mawili matatu kuhusu Bunge na ndipo aliponijuvya kuhusu UFANISI WA KITENGO CHAO CHA SASA CHA MTANDAO.
Wamekwisha weka picha na taarifa za wabunge wote waliochaguliwa na pia hata za mkutano wa Mhe Spika baada ya kuchaguliwa upo.
Tatizo nililoliona na ambalo ningependa kuona waungwana wakilishughulikia ni mfumo wa kuyaandika majina. Mfano, wameandika Mhe. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ambalo jina limeandikwa moja kwa moja kuanzia la kwanza mpaka la mwisho.
Kisha kuna majina kama Mhe. KAJUMULO TIBAIJUKA PROF. ANNA ambaye yeye wameanza na jina la kati kisha mwisho kisha cheo halafu jina la kwanza
na mwisho tuangalie la Mhe. FAUSTINE ENGELBERT DR.NDUGULILE hapa wameanza jina la mwanzo, kisha la kati halafu "cheo" kisha la mwisho.

ZAIDI YA HAPO PONGEZI KWENU
Hapo twategemea kuona "updates" za wasemacho, wasemapo na wasemavyo

ASANTENI NA HONGERENI KITENGO CHA TOVUTI YA BUNGE.

Wednesday, November 10, 2010

UJUMBE WA Da SUBI KWA WADAU WA WAVUTI.COM......

Da Subi wa www.wavuti.com
Kwa heshima na taadhima ya waungwana na wastaarabu (kwa tafsiri sahihi ya kamusi kwa maneno hayo na si unyambulisho), napenda kufahamisha wasomaji wa wavuti.com kuwa ninayo furaha na nimejawa na wingi wa shukrani kwa michango na changamoto zinazotolewa na watoa maoni. Kupo kuvumiliana kwa hali ya juu.

Walioanza kusoma blogu hii mwanzoni watakumbuka kuwa nilikuwa nikiandika na kuchapisha matoleo binafsi wakati mwingine kama 'mwendawazimu' kutokana na kushindwa kuwa na maneno ya kistaarabu wakati wa kuandika katika matoleo hayo, ili kufikisha ujumbe kusudiwa. Lakini kwa miezi ya hivi karibuni, matoleo hayo yamepungua. Sababu hasa ya kufanya hivi ni kutokana na kutaka kuacha kuandika zaidi habari za “mafumbo” na zenye kutumia tamathali za semi, na kuanza kuziandika peupe.

Nimepokea jumbe tatu tofauti zinazolandana, ndani ya wiki moja:-

- Mosi, unatoka kwa Mabalozi wawili kuniandikia kuwa huwa anasoma wavuti.com
- Pili, unatoka kwa mapadre wawili (mmoja yupo Tanzania, mwingine yupo Roma)
- Tatu, unatoka kwa kijana ambaye amepata “mchumba” kutokana na “mchumba” huyo kupendezwa na maoni aliyokuwa akiyaacha kijana (sikutarajia kuwa maoni yako yanaweza kukupatia mpenzi anayeweza kuwa mwenza wa maisha, so be careful with what you write, people take notes, you could be attracting or scaring away someone. Your words reflects your personality).

Dondoo za barua pepe hizo, mojawapo ikinitaka kusema jambo, ndizo zimenisababisha niandike toleo la leo.

Kwa siku za hivi karibuni, wavuti imekuwa ikipata wasomaji wengi zaidi (kwa mujibu wa takwimu “stats”).

Ni katika ongezeko hilo ninapenda kukufahamisheni kuwa wasomaji wa wavuti si watu wanaoperuzi mitandao tu kama ‘majuha’ la hasha! ni watu ambao husoma na kufuatilia zaidi habari zinazogusa maisha ya jamii ya Mtanzania aliyeko ndani na nje ya nchi.

Wapo watu wa umri na rika kubwa, wanaotimu miaka 70, wanaosoma wavuti.com (uthibitisho ninao, sitauanika)
Wapo vijana wengi wanaofika hapa kujua “kulikoni”, na hawa ni wengi.
Sina uhakika na watoto....

Hivyo basi, ninapenda kuomba samahani kwa mtu yeyote anayeweza kuwa amekwazwa na matumizi ya lugha aidha yangu binafsi au ya watoa maoni. Sina uthibitisho kuwa hili linaweza kuzuiwa kwa asilimia 100, hivyo tuvumiliane pale inapowezekana. Hii ni kutokana na kutokufahamiana kwetu na kutokana na uhuru wa matumizi ya lugha kwa mhusika. Tunafahamu kuwa mtu anapokuwa huru bila kufungwa na woga kuwa niandikapo haya watanifahamu, basi mtu huyo huweza kuandika atakavyo. Lugha na matumizi ya maneno haya yanaweza kuwaudhi baadhi yenu. Nami ninakusihini, tafadhali, kwa heshima yenu, mvumilie kama wazazi/walezi wanavyowavumilia vijana wao wanapokuwa na “frustrations” lakini huwarejeza kwa maneno ya upole na yenye maelezo yanayokidhi haja. Kwa hiyo, ili kuiwekea uwiano (balance) hali hii, ninawasihi pale yanapotolewa maoni yenye maswali, dukuduku na kutaka maelekezo, ili kupunguza jazba na kero, basi walao mchukue muda wenu kutoa maelezo au maelekezo ya wapi maoni hayo yafikishwe (nafahamu ipo tovuti ya wananchi.go.tz lakini ni kama “geresha”, kwamba mlitaka tovuti ya maoni, hiyo hapo! Kwa maana watu wanaandika na kuandika lakini majibu ni "nehi" yaani, hakuna).

Vijana, ni kweli damu zinachemka, lakini badala ya kutumia lugha ya matusi na kejeli ambayo itamzuia hata mwenye jibu kufikiria kutumia muda wake kujibu hoja hizo, basi tujidhili kidogo, andika kero na hasira yako lakini usimtusi mtu (hata ikiwa unadhani kutumia kwake cheo na madaraka vibaya ni tusi kubwa kwako na kwa wananchi, bado kumkosoa mtu huyo si vyema kutumia matusi, hebu mwaibishe kwa kumwekea kasoro zake ili aonekane “kubwa jinga” kwa kutumia lugha nzuri ili kuwathibitishia kuwa vijana si “waruwaru” kama wanavyodhania. Prove them wrong, use a diplomatic language, wenyewe watatia heshima).

Shukrani kwenu, mmewezesha kufikia ONE MILLION PAGE VIEWS in just ONE FREAKING YEAR!!!

This would have not been possible if it were not for YOU guys!

Let’s maintain wavuti.com a blog for sharing SCHOLARSHIPS, OPPORTUNITIES (jobs, grants, trainings, courses, seminars) and NEWS (local and international that affects our nation) and not to forget those “lighter moments”.

KUMBUSHIO NA SISITIZO :
wavuti.com hadi sasa HAIFUNGAMANI na mrengo wowote (siasa, dini, taaluma, rangi ya mtu, jinsia, kabila, rika, nk.)
Ninapokea ujumbe kupitia
subi@wavuti.com na kulingana na maudhui, ninauchapisha kwa wakati muafaka.

Ujinga mkuu ni kuwa MJINGA WA UJINGA WAKO

Nafananisha "tittle" hiyo na nukuu yake Saint Jerome (374 AD - 419 AD) aliyesema "It is worse still to be ignorant of your ignorance." Hakuna ubishi kuwa kati ya vitu ambavyo hatutaki kujifunza, ama niseme kati ya vitu ambavyo ni "DONDA NDUGU" nchini Tanzania, basi ni KUTOJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA TULIYOFANYA.
Naamini kuwa ufanisi wa BUNGE na SERIKALI ya Tanzania UNADIDIMIZWA na mambo mengi ikiwemo KUTOANDALIWA KWA WATAWALA / VIONGOZI TULIONAO. Labda hata kina Mwl Nyerere hawakuandaliwa lakini walikuwa na kipaji na hata moyo na nia ya kuongoza na walikuwawaadilifu.
Tumeona namna ambavyo watu wasio na ujuzi katika SAYANSI YA SIASA, UONGOZI na hata KIPAJI CHA UONGOZI wakijiwezesha kupata nafasi na kisha kuchaguliwa kuchukua nafasi mbalimbali na hasa za UUNGE nchini mwetu, lakini kibaya zaidi ni kuwa watu hao hao wanateuliwa kushika nyadhifa kubwa ndani ya nchi yetu bila ya kuwa na kile kinachoaminika kuwa utoshelezi a nafasi wazikwaazo. Kwa maneno mengine ni kuwa HAWAANDALIWI.
Leo hii kwa kuwa siasa na hasa ubunge umekuwa "dili la uhakika / msimamo", tunaona madaktari, wauguzi, waandishi, wanamuziki, mawakili na wengine wasio katika mfumo wa siasa (na ambao pengine hawajaingia katika mfumo huo) wakiamua kuzikacha nafasi zao kwa wingi zaidi kuwahi pale palipo na pesa...BUNGENI.
Ni kweli kuwa wapo wanaokuja kuwa viongozi bora, lakini ni nani anayewafunza hawa wapya "waliovamia fani"? Ama ndio zilezile kauli za kuwa "miaka mitano ya kwanza ilikwa ni ya kujifunza"? Nilipokodolea macho RATIBA YA SHUGHULI ZA BUNGE NOVEMBA 2010 (irejee hapa) sikuona mafunzo ya awali kwa WABUNGE WAPYA. Sikuona kile ambacho wengi huita ORIENTATION kwa wabunge wapya na hata warejeao ili kujua nini cha kufanya katika kutimiza KWA UFANISI kazi waliyotumwa na wananchi wao. Matokeo yake ndio yaleyale tuliyosikia mwaka 2006 kwa Mbunge kutolewa bungeni "kutokana na kukiuka kanuni ya Bunge, kipengele cha mavazi", kanuni (ninayoionayo ya kitumwa na isiyoendana na mazingira yetu Tanzania) ihimizayo kuvaa suti na glovu. Cha kushangaza ni kuwa baada ya tukio hilo, Mbunge wa Koani, Haroub Said Masoud (CCM), aliomba mwongozo wa Spika akisema zaidi ya asilimia 50 ya wabunge katika kikao hicho walikuwa wageni, lakini (kama livyo ada yao kwa ahadi),Spika alipokea mapendekezo hayo, na kusema Katibu wa Bunge ataandaa semina hiyo. Kisha kina "anon" wakaanza kubwabwaja kumsema m'bunge huyo badala ya kuuliza ni vipi bunge lilimtegemea m'bunge huyu kijana na m'changa atambue miiko ya bunge kama hajaandaliwa? Ni vipi bunge lilitegemea yeye (na wengine) waijue mipaka / kanuni / miiko hiyo ya bunge kama hakuna anayewapa mwongozo kamili, sahihi na RASMI???ACHANA NA MAVAZI, ACHANA NA KUONDOLEWA BUNGENI.
Hivi ni WABUNGE wangapi wanaojua kuwa WAAJIRI WAO NI WANANCHI NA SIO ILANI ZA VYAMA VYAO????
Ni wabunge wangapi wanaojua kuwa katika chaguzi za majimbo yao, wamependwa ama kuchaguliwa wao kwa kuwa ni SULUHISHO la matatizo ya wananchi wao na si kwa kuwa wananchi wengi wa hapo wanapenda chama lichogombea?
Ni wangapi ambao wanatambua kuwa wao ni SAUTI HALISI YA WANANCHI na sio "ujazo' wa kura za kupitisha, kupinga ama kuadhibu kile kionwacho ndivyo ama sivyo na wanachama wa chama awakilishacho?
Ni wangapi ambao wanaamini kuwa HAWALAZIMIKI KUUNGANA NA CHAMA CHAO katika maamuzi, kama maamuzi hayo yanawakandamiza ama kutowanufaisha wananchi wao?
Ni wangapi ambao wanajua kuwa hapo ni kama SHULE na wamalizapo muhula wanatakiwa kurejea NYUMBANI walikochaguliwa wakiwa na ripoti ya matokeo ya mtihani wao wa uwakilishi?
Ni wangapi wanajua wajibu halisi wa kuwashirikisha wananchi wao kile walichojadili bungeni, kukusanya maoni ya wananchi juu ya walilojadili na kisha kurejesha pongezi ama pingamizi la baadhi ya mambo ambayo wananchi wanaona hayawafai
Nina hakika ka wabunge wengi hawatekelezi haya na hasa hili la mwisho. Na wamekuwa wakikacha hili kwa miaka nenda miaka rudi, na HUU NI UJINGA. Na kutotekeleza hili ni UJINGA WA UJINGA HUO.... Na ni hili linalosikitisha zaidi kuwa tunakuwa wajinga wa ujinga wetu.Jambo ambalo ni HATARI na ndio UJINGA MKUU.

JICHO LA NDANI ni kipengele kinachozungumzia mambo mepesi na yaliyo ndani mwetu, ambayo yakiangaliwa vema na kwa tafsiri ama tafakari njema yanaweza ama ndio suluhisho kwa matatizo yetu. Kwa matoleo yaliyopita katika kipengele hiki, BOFYA HAPA

Sunday, November 7, 2010

Give Thanks and Praises.......BEHOLD by Culture

@ www.photosforsouls.com/nature57.html
I was travelling up the mountaine one day
And suddenly, I heard the voice coming to I and say,
Behold i come quickly to pay every man
According to the work that they have done.
And I know, it was the Voice, the voice of the MOST HIGH.
And I know, it was the Voice, the voice of the MOST HIGH.
Say BEHOLD, BEHOLD I Come quickly


This world is like a mirror, reflecting at what you do,
and if you face it smiling, it will smile right back to you.
So do unto others as you would have them do,
So you days, will be many many much longer
And I know, it was the Voice, the voice of the MOST HIGH.
And I know, it was the Voice, the voice of the MOST HIGH.
Say BEHOLD, BEHOLD I Come quickly


JUMAPILI NJEEEEEMA

Friday, November 5, 2010

Them, I & Them....SO MUCH TO COME....Morgan Heritage

"If you think the judgement started, there's so much more left to come. If you think your tears a-run yet, there are so many more tears to run, if you think you've seen the blood yet, there are so much more blood to run... WE FEEL IT FOR THE CHILDREN, FOR THE WORLD THAT THEY KNOW IT.... WILL NOT LAST FOR LONG" Morgan Heritage
Ni kauli ambayo nimeanza kuiona na kuanza kuiwaza kwa nchi yangu niipendayo TANZANIA. Uchaguzi mkuu wa Uraisi na wabunge ndio umemalizika siku 5 zilizopita na mpaka sasa KWA SABABU NINAZOJITAHIDI KUZIELEWA, hayajatangazwa. Lakini Morgan Heritage walishatuonya tangu 2003 kwa wimbo huu kuwa KUNA MENGI YAJA. Jah Petes Morgan. Lead vocalist wa Morgan Heritage
Tumeanza kusikia kauli tata kuhusu matokeo na usalama wa watu na mali jambo ambalo linasikitisha zaidi. Lakini hili si la kushangaza kwani Morgan Heritage wamesema "these are the days known as eve of destructions, with POLI-TRIX just leading every nation". Sina hakika na TUHUMA HIZI ZA DR SLAA KWA USALAMA WA TAIFA wala MAJIBU HAYA YA USALAMA WA TAIFA ama MAJIBU NA TUHUMA ZAIDI ZA DR SLAA KWA TUME YA TAIFA, lakini nijualo ni kuwa kuna mahala pema pa kujadili na kuyatatua haya.
Tatizo kubwa ni kuwa wanaoathirika si wale walio kwenye "usukani" wa tukio hili. Si wagombea walioshiriki, sio wana-tume wanaoshutumiwa "kuchakachua" kura hizo na wala si wale watakaamua nini cha kufanya, wanaoathirika zaidi ni WATOTO ambao hawakuhusika kwenye kampeni, kwenye kupiga kura, wala kwenye "kuhesabu" kura hizo. Na ni hao ninaowawaza, kuwaonea huruma na kuwaombea.
Ni wakati ambao lazima kutanguliza maslahi ya TAIFA mbele. Wakati wa kuchunguza NGUVU ZA KAULI na MATENDO yanayoweza kuathiri wengine.

Wimbo huu ufuatao ni kumbusho kuwa kuna mengi yajayo zaidi ya tuonayo. Kama ni dhuluma zikingali nyingi zikija, kama ni uhalifu, dharura na mengine yaathiriyo maisha ya watoto BADO KUNA MENI YA KUJA. Swali ni kuwa TUMEJIANDAAJE KUWASAIDIA AMA KUWAOKOA WATOTO?
Sikiliza wimbo huu wao Morgan Heritage wakisema SO MUCH TO COME wakizungumza mambo yajayo.

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

Thursday, November 4, 2010

AGENDA YA KWANZA YA UCHAGUZI WA 2015 IWE NI UCHAGUZI WA 2010

"A nation that forgets its past is doomed to repeat it." Sir Winston Churchill
Nilipobandika toleo langu la kwanza la kipengele cha "UCHAGUZI 2010" la Machi 11, 2009 nilipata barua pepe ikiniambia kuwa "uchaguzi ni mwakani wewe unaanza kuujadili sasa?". Naamini alilomaanisha mtuma ujumbe ni kuwa nilikuwa nimewahi mno kuanza kujadili mchakato mzima wa uchaguzi kwani bado kulikuwa na mwaka mmoja, miezi saba na siku 20 kabla ya "siku ya siku". Lakini sasa.... ni historia.
Uchaguzi mkuu wa Tanzania ndio umemalizika kwa wananchi "kutuma ujumbe" kwa wahusika kwa namna waliyoamini ni sahihi. Lakini wakati uchaguzi huo ukisubiri matokeo (ambayo naamini "yanawekwa sawa" kabla ya kutangazwa), naamini pia HUU NDIO WAKATI WA KUANZA RASMI MBIO ZA 2015 KWA WENYE NIA DHAHIRI NA HALISI YA KUIKOMBOA TANZANIA.
Ninasema mbio zianze kwani ni vema kwa wahusika kuanza kutengeneza mazingira mazuri ya uchaguzi kwa kujaribu kukosoa mambo mbalimbali yaliyojitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Na kama matokeo ya jumla kwa nchi kama Tanzania yanaweza kuchukua siku kadhaa "kuwekwa sawa" na kutangazwa, naamini KUBADILI MFUMO WA UCHAGUZI KUTAHITAJI MIAKA KADHAA.
Ni katika kuwaza namna ya KUBORESHA uchaguzi wa mwaka 2015, nikaona kukusanya haya machache ambayo nayaona kama ajenda / agenda ya kwanza katika kuelekea uchaguzi huo ili wakati ukifika tusirejee "kulia" kwa yale ambayo yalishatokea na tukayapuuza. Na ndio maana nilianza na hiyo nukuu ya Sir Churchill.
Sasa baadhi ya ajenda za CHANGAMOTOYETU kuelekea uchaguzi 2015 ni.....
1: MIDAHALO KWA WAGOMBEA URAIS NI LAZIMA.
Mwaka huu nilishangazwa, kusikitishwa na kukereka na namna ambavyo chama tawala kilionesha dharau kwa kugoma kufanya mdahalo. Sababu niliyoisikia ikitajwa ni kuwa wagombea watawafuata wananchi huko waliko. Huu ni upungufu wa elimu ya awali ya uraia.
Kuna haja kwa bunge kupitisha SHERIA ya midahalo (japo mitatu) kwa wagombea wote wa nafasi ya uraisi ili kuweza kuwapa uwanja wa kupambana. Mwaka huu tumeona walivyokuwa wakirushiana "ya nguoni" kwa kuwa tu hawakuweza kukabiliana ana kwa ana kupambanisha sera.
2: REJEO ZA AHADI ZA UCHAGUZI 2010
Sitashangaa kusikia kuwa ni asilimia chache ya waTanzania wanajua nani aliahidi nini wakati wa kampeni. Hili ni kwa kuwa siamini kama kila aliyejitokea na fulana ya chama huzika alikuwa amekwenda kusikiliza sera na si kingine. Baadhi ya wagombea wameonekana kwenye taswira wakiwa na umati wa kuridhisha japokuwa si hakika kuwa wote walioenda walisikia na kunukuu ahadi zilizotolewa. Kama hukubahatika kuziweka ktk kumbukumbu, ZISOME (za wagombea uraisi) HAPA
Kinachotakiwa ni kusubiri 2015 ili kujua zimetekelezwa vipi.
3: UCHAMBUZI WA AHADI ZINAZOTOLEWA.
Kwa bahati mbaya ni kuwa wengi wa "waandishi" wanawekeza kwenye kunukuu kilichosemwa na si kusaka uhalali wa kinachosemwa. Mfano, nilimsikia mgombea uRaisi kwa CCM akisema... ndani ya miaka 5 atahakikisha maji toka ziwa Victoria yanawafikia watu wa Tabora ilhali walio "mwaloni" katika mikoa ya Mwanza, Kagera na Mara hawana maji ya kutosha toka ziwa hilohilo ambalo lipo mwendo mfupi zaidi ukilinganisha na mkoa wa Tabora. Watu wakapiga makofi, vigelegele na naamini kura zikahahakishwa...Hakuna aliyehoji wala kudadisi usahihi wa ahadi kama hiyo na kuwa kama atafanya hivyo kwa Tabora baada ya kumaliza Kagera Mwanza na Mara.
4: KAMPENI SI NYUSO ZA WATU PEKEE.
Helikopta zilikuwa kivutio kikubwa saana (na pengine ukiongeza fulana, kuwaona wasanii bure, kofia, kanga na kadhalika..) vyaweza kuwa sababu pekee ya watu kufurika mikutanoni. Lakini swali hapa ni kuwa ni kwanini wagombea wahimize kuona maisha ya wananchi mikutanoni? Nina hakika kuna mahali ambapo wagombea wa mwaka huu hawatarejea tena mpaka miaka 5 ijayo watakapoomba kura. Je! ni asilimia ngapi ya matatizo ya wananchi hudhihirika kwenye mikutano ya kampeni?
Kuna haja wagombea wakatafuta namna ya kuungana na kujihusisha na maisha halisi ya wananchi kwa kuwatembelea na kuona mazingira waishiyo hivyo usafiri usiwe wa kupaa na kutua pekee. Labda ndio maana wagombea hawajui hata kero za barabara za "wananchi wao".
5: TUME YA UCHAGUZI.
Hapa najua sina la kunena. Hii ya mwaka huu imenifurahisha zaidi maana licha ta TEKNOLOJIA kutumika katika chaguzi za miaka hii, licha ya kuwa tume hii ilikuwa ikitambua na kujiandaa kwa uchaguzi huu tangu mwaka 2005 (ulipoisha uliopita), licha ya wagombea kusema miundombinu imetengemaa zaidi, bado tume ya uchaguzi imekuwa kero zaidi ya maelezo.. Hili wengi walilizungumzia na hata mtandao wa Bongo Celebrity uliliongelea.
Kwa ujumla TUME YA UCHAGUZI TANZANIA INASTAHILI MAREKEBISHO.
6: ELIMU YA URAIA KWA WANANCHI
Kati ya mambo yaliyosikitisha katika uchaguzi uliomalizika ni idadi ndogo ya waliojitokeza kupiga kura ukilinganisha na waliojiandikisha. Na pia kura zilizoharibika zimekuwa nyingi kiasi kwamba kama uharibifu huo ungezuiwa kwa elimu ya uraia kwa wapiga kura, labda matokeo yangekuwa tofauti na yalivyo. Mfano halisi ni nafasi ya Uraisi visiwani Zanzibar ambapo tofauti kati ya Rais Ali Mohamed Shein na aliyeshika nafasi ya pili, Seif Sharif Hammad ilikuwa ni kura 3471 ilhali zilizoharibika ni 6109. Kwa maana nyingine, kama theluthi mbili ya kura zilizoharibika zingeweza kuwa halali, kungekuwa na ushindi mpana ama wa tofauti zaidi.
Lakini yote juu ya yote, kusikia kitui kiliandikisha watu elfu ishirini na waliopiga kura ni elfu tatu hizi si habari za kupuuza hata kidogo.
Unahitajika uelimishaji kwa wapiga kura ili watumiapo muda wao (ambao wanatakiwa kuhimizwa kuutumia) kupiga kura, basi wahakikishe kuwa kura zao haziharibiki na uchaguzi wao unahesabika.

Uchaguzi 2015 ni "label" inayozungumzia namna nilivyoona uchaguzi wa 2010 na namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

Wednesday, November 3, 2010

Kwanini nafurahia kushindwa kushinda kwa walioshindwa?????

Photo credit: GVLN Rao blog
Nani asiyejua kuwa "mwanzo halisi wa mlima ni mwisho halisi wa bonde"?
Ama ni nani anayesahau kuwa furaha ya sasa ni akiba ya huzuni ijayo?
Na kuna aliyesahau kuwa huzuni ya sasa ni akiba ya furaha ijayo?
Basi kwa "MANTIKI" hiyo hiyo.... kuna mengi ya kufurahia kwa wale walioshindwa.
Kuna mengi ya kujifunza na kuna mengi ya kusahihisha.
Kwa maana nyingine, ni kwamba ili walioshindwa sasa wahakikishe kuwa wanafanikiwa baadae, kuna ulazima wa waliofanikiwa sasa kushindwa baadae.
Sasa ni kwanini NIMEFURAHIA "kushindwa kushinda kwa walioshindwa"? Ntakwambia baadae. Malizia "kumeza" matokeo kisha nikueleze UTAMU wa UCHUNGU walionao wale walioshindwa wiki hii huko nyumbani Tanzania na hapa nyumbani.
PamoJAH

JICHO LA NDANI ni kipengele kinachozungumzia mambo mepesi na yaliyo ndani mwetu, ambayo yakiangaliwa vema na kwa tafsiri ama tafakari njema yanaweza ama ndio suluhisho kwa matatizo yetu. Kwa matoleo yaliyopita katika kipengele hiki, BOFYA HAPA

Tuesday, November 2, 2010

Ni kweli Dk Shein kashinda..lakiniii..... labda Maalim Seif hajashindwa pia.

Septemba 3 mwaka jana niliandika makala yenye kichwa cha habari "Tunajidanganya wenyewe kudhani twawajali wengine (irejee hapa)" ambamo humo nilieleza kile ninachoamini kuwa UNAFIKI wa binadamu katika kudhani kuwa anampenda tu ilhali ukweli ni kuwa anapenda hisia anazokuwa nazo anapodhani anampenda mtu huyo. Nilisema (na hapa nanukuu) "Kuna ukweli ulioko 'nyuma ya pazia la akili zetu' kuwa, kila tufanyacho ni kwa manufaa yetu hata pale tuonekanapo ama kujitahidi kujifanya kuamini kuwa ni kwa manufaa ya tumfanyiaye." Ukweli huu umedhihirika hapo jana baada ya matokeo ya uRaisi huko Zainzibar kutangazwa ambapo mgombea wa CCM Dk Ali Mohamed Shein ametangazwa mshindi. Matokeo haya (ambayo blogu hii inayafurahia kuwa yamekwenda sawia bila vurugu kuu wala umwagaji damu), yalionesha kile ambacho wenye fikra chovu wameita UKOMAVU WA SIASA kwa kuwa mgombea wa chama cha upinzani Maalim SEIF SHARRIF HAMAD ameyakubali mara moja tofauti na chaguzi zilizopita. Hili lilizua mjadala na chuki kuubwa saana kwa wafuasi wengi walioamini kuwa kwa udogo wa tofauti za kura ni lazima kuna "uchakachuaji" uliojitokeza na hivyo kuamini kuwa Maalim Seif amewasaliti kuachia kiti hicho walichoamini kuwa "chao" kutwaliwa na Dr Shein.
Lakini wana haki ya kuwa hivyo maana wanaamini kuwa Maalim Seif ni "mpiganaji" wa kweli katika kutetea haki zao hasa wakikumbuka alivyosimma imara kupinga matokeo ya mwaka 1995, 2000, na 2005. Na hapo ndipo lijapo swali kuwa
MWAKA HUU KUMETOKEA NINI?
Ni kweli kuwa mwaka huu Maalim Seif ameshindwa "vibaya" kuliko awamu hizo tatu alizogombea? LA!
Ni kweli kuwa Maalim Seif ameona safari hii kuna ushindi wa dhahiri na ni kuwa ameshindwa kihalali??? Mmmmmmhhhh!!! SIJUI

Labda tuangalie takwimu hapa kule Zanzibar
JUMLA YA KURA ZILIZOPIGWA ni 364,924
KURA HALALI ni 358,815
KURA ZILIZOHARIBIKA ni 6109

DK ALI MOHAMMED SHEIN (CCM) amepata 179,809 sawa na 50.1%
MAALIM SEIF SHARIF HAMAD (CUF) amepata 176,338 sawa na 49.1%
SAID SOUD SAID (AFP) amepata 480
KASSIM ALI BAKARI (Jahazi Asilia) amepata 803
HAJI AMBAR KHAMIS (NCCR-Mageuzi) amepata 363
HAJI KHAMIS HAJI (NRA) amepata 525
JUMA ALI KHATIB amepata 497
Chanzo: http://www.wavuti.com/habari.html#axzz145HHz4Is

INA MAANA....tofauti kati ya kura za Dr Shein na Maalim Seif ni takribani nusu ya zilizoharibika. DUH!! BAHATI MBAYA SAANA HII

Ila ninalojua ni kuwa, katika huu mpango wa SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA, basi maalim Seif "atakuwa ndani" na kwa maana hiyo hakuna haja ya kuendelea kuburuzana.
Lakini swali jingine laja...
Kwani Maalim Seif alikuwa akigombea KWA MANUFAA YA NANI??????
Ya wale waliompigia kura na ambao waliendelea kutukana kwenye "chat rooms" baada ya yeye kukubali matokeo? Ama kwa ajili ya malahi yake binafsi?
HAPO NDIPO NINAPOTAKA UREJEE NUKUU HIYO HAPO JUU YENYE RANGI NYEKUNDU.
Na swali la ziada laja kuwa kama waliokuwa wakimpigia kura Maalim Seif walifanya hivyo ili aweze kuingia madarakani na kuwa mkombozi wao, si ataingia? Na akiingia si anaweza kuwa msaada kwao hata kama si Rasi? Tena kwa kuwa ameingia kwa "uhusiano mzuri na Raisi"?
Kwani waliyekuwa wakitaka akawatete si kakubali? Kwanini na wao wasikubali???
REJEA TENA NUKUU NYEKUNDU HAPO JUU
Labda nimalizie kwa kusema kile ambacho nilisema kwenye makala niliyoinukuu hapo juu kuwa
"Ukweli wa mambo ni kuwa HAKUNA JAMBO LOLOTE DUNIANI AMBALO ULIFANYA, UNAFANYA NA UNAWEZA KUFANYA NA LISIKUNUFAISHE AMA KUKUFAIDISHA KWA NAMNA YOYOTE. Ninalomaanisha ni kuwa kama itatokea ukapata faida ndooooog kuliko, ni ile ya kujua kuwa "hatimaye nimetekeleza" (wenyewe wanasema At least i did it) achilia mbali suala la kwanini umetekeleza.
Hakuna kisicho na faida maishani mwetu ambacho tunatenda.
Kama kuna ambaye anaamini kuwa alishatenda jambo lolote ambalo halikumnufaisha yeye, basi ajiulize mara mbili na kama hapati jibu la faida basi jiulize kama "uliridhika na yale mema uliyotenda?" Kama uliridhika na wema huo, basi faida yako ni hilo ridhiko."
YAWEZEKANA NI KWELI Dr SHEIN AMESHINDA URAISI WA ZANZIBAR.....LAKINI LABDA NA MAALIM SEIF NAYE HAJASHINDWA
Wakasirikao wamesahau "sig-out" ya Nguli wa habari za Africa SHAKA SSALI anayehodhi kipindi cha Staright Talk Africa
99;">Labda tuburudike na Nasio katika wimbo HYPOCRITES

NAWAZA KWA SAUTI TUUUUUUUU!!!!!!!!!!!!!!




Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA