Tuesday, September 25, 2012

KISWAHILI kama USHOGA.......na watendakazi wetu "wafu"

Photo Credits: Mugishagwe Bolg
Februari 24, 2010 niliandika POST HII iliyokuwa na kichwa kisomekacho Wanasiasa wetu na sakata la Ushoga / Usagaji. kuhusu pendekezo la Mbunge wa Uganda kuwa watu wanaoendekeza vitendo vya ushoga wauawe.
Nilipinga nikianza na maelezo SAHIHI kuwa mimi si shabiki wala siendekezi wala kuunga mkono ushoga, lakini sikuamini kama ilikuwa sahihi kuanza kuwaua sasa ilhali hatukuona jitihada makusudi kuwasaidia wasiwe walivyo.
Katika tileo hilo, niliandika
"Tuanze kwa kutambua kuwa MASHOGA NA WASAGAJI ni wenzetu, waliozaliwa katika familia ambazo nyingi ni za watu wasio mashoga wala wasagaji.
Kwa hiyo kama wamezaliwa katika familia zilizo tofauti na walivyo leo, NI LAZIMA TUJIULIZE kuwa NI WAPI TULIPOJITENGA NAO NA KUWAFANYA / KUWAACHA WABADILIKE NA KUWA WALIVYO?
Sisi kama JAMII TUNA SEHEMU YA LAWAMA kwa kuwa ama hatuwasaidii kutokuwa walivyo, au tunachochea kuwa walivyo hata kama twatenda haya bila sisi kujua. Suala hili la USHOGA NA USAGAJI halijaanza leo wala mwaka jana ambapo wanasiasa wameonekana kulivalia njuga.
Nakumbuka nikiwa mdogo tulisikia utani wa "kushikishwa ukuta huko Lamu" na baada ya kukua na kung'amua nikajua kuwa ni suala la USHOGA NA USAGAJI lakini hakuna aliyethubutu kujadili nasi kuhusu suala hilo mpaka leo hii ambapo mambo yanaonekana kuwazidi nguvu naanza kuwaona WANASIASA wakija na hatua zao za zimamoto ambazo zinafikia hatua ya kuwaadhibu hata wale watakaoshindwa kuwataja mashoga na wasagaji wawaju.
TATIZO KUBWA NI MOJA KWA NCHI ZETU ZA KIAFRIKA.
Hakuna kiongozi anayetaka kujishughulisha na chanzo cha tatizo. Wanakurupuka kwa namna za KUAHIRISHA tatizo na kisha kutumia uhahirisho huo kujipatia kura za kurejea madarakani.
Kisha tatizo larejea.
Wakati nasikia habari za kile nilichokuja kung'amua kama matendo ya kishoga na usagaji nilikuwa mdogo, na nina imani kuwa walikuwepo mashoga na wasagaji wachache saana ukilinganisha na sasa lakini kile wanachokiita "mila za kiAfrika" ziliwazuia wazazi, walezi na viongozi kujadili ATHARI za kujikita kwenye tabia mbaya kama hizo na matokeo yake ndio tuonayo sasa ambapo tatizo hili LIMEOTA MIZIZI na twasikia harakati za KUWAFUNGA NA KUWAUA.
Kisha baada ya hapo?????"
SASA TUHAMIE KWENYE MSHABIHIANO WA USHOGA NA KISWAHILI.
Ni nani asiyejua namna ambavyo kiswahili kinaharibiwa hivi sasa?
Yaani tangu kuingia kwa hivi viwezeshaji vya mawasiliano vilivyo na kiwango cha maneno ya kutumia, watu wameanza kuandika lugha ambayo inatupeleka pabaya.
Sijasikia wala kusoma onyo ama maelezo kutoka kwenye vyombo husika katika lugha ya kiSwahili.
Na tunatakiwa kuwaza iwapo hawa watoto (pamoja na wageni) ambao wameanza kujifunza kiSwahili katika zama hizi za Twitter na Facebook na Text msgs watakuja kujua kiSwahili halisi.
Hawa WATAWALA wenye mamlaka na ambao wanajua kuwa kile kizungumzwacho na "vijana wa kisasa sio kiSwahili sahihi" wanafurahia na kuangalia "ubunifu na utundu" wa WAHARIBIFU HAWA na kushindwa kusema lolote.
Wako wapi BAKITA ambalo liliundwa chini ya sheria namba 27 ya Bunge ya mwaka 1967.
Na ni nini kazi yao?
Kwa mujibu wa MAELEZO KATIKA TOVUTI YAO HII, wanasema "Kimsingi, BAKITA ndiyo inayofanya kazi ya kuratibu na kusimamia shughuli zote za kukuza, kuendeleza na kueneza Kiswahili nchini."
Katika tovuti hiyohiyo, BAKITA wanasema kuwa DHAMIRA YAO ni "Kukuza, kustawisha na kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha ndani na nje ya nchi kwa ushirikiano na wadau wengine." na pia DIRA YAO ni "..kuwa taasisi yenye nguvu kisheria, kifedha na inayotambulika kitaifa na kimataifa katika kuratibu, kusimamia na kukuza maendeleo ya lugha ya kiswahili. Kukubalika kwa matumizi ya Kiswahili katika Umoja wa Afrika (UA) na mafanikio ambayo lugha hii inayapata, vinatupa tumaini na imani kwamba kile tunachokiamini na ambacho tumekuwa tunakiamini siku zote kuwa Kiswahili kitakubalika duniani kote sasa taratibu kinaelekea kuwa kweli na kwa hakika zaidi."
WAKO WAPI?
WANAKABILIANA VIPI NA HILI LINALOONGEZEKA KILA SIKU?
Ukweli ni kuwa vijana wengi wanaharibikiwa kwenye mitandao ambayo BAKITA haina mpango nayo.
Tukishindwa kuzuia sasa mmomonyoko huu, tutakuja kukurupuka na kutoa kauli kama zilizotokea kwenye suala la ushoga.
Katika hili la mashoga, niliwaomba watawala, kuwa Chonde chonde "waheshimiwa". Kabla hamjasema tena ya Cameron....... na humo nikawakumbusha kuwa "Kama suala la mashoga na wasagaji linawakera kama ambavyo mmeonyesha kwenye kauli zenu, ni yapi ambayo mmeyafanya kulipunguza ama kuliondoa? Mimi na ninyi na wasomaji wangu tunajua kuwa kama tungekuwa na mashoga sifuri, basi tusingehofu kuhusu hili.
Lakini kwa kuwa idadi yao ni kubwa NA INAONGEZEKA KWA UHURU KILA UCHAO, mnaona athari zake. Lakini kabla hamjasema tena juu ya kauli ya Cameron, mtusaidie kutueleza ni yapi mmefanya kupunguza ama kuondoa ushoga Tanzania? Tena nimesikia Mhe Membe akisema SHERIA INASEMA WANAWEZA KUFUNGWA MPAKA MIAKA 30 JELA. Sina hakika ni wangapi walikuwa wakilijua hili, na sina hakika takwimu za Waziri na Rais zaonyesha ni wangapi wameshafungwa kwa hili?"
Sasasaaaa........
Juhudi za haraka na madhubuti zinahitajika kuhakikisha kuwa lugha ya kiSwahili haifikii mahala ambapo hatutaweza kuirejesha inapostahili kuwa.
SERIKALI INASTAHILI KUCHUKUA HATUA, KUHAKIKISHA KUWA INATUNZA LUGHA SANIFU YA KISWAHILI KWA KUWEKA MASHARTI MAKALI KUHAKIKISHA KUWA VYOMBO VYA HABARI  (VILIVYOJISAJILI) VINATUMIA LUGHA SAHIHI NA SANIFU. 

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA

Tuonane "Next Ijayo"

Saturday, September 22, 2012

Ana kwa Ana ya IskaJoJo na Hafsa Kazinja

Fuatilia mahojiano haya kati ya IskaJoJo Photography na msanii wa muziki wa Zouk Tanzania Hafsa Kazinja.
Wamezungumza mengi mema.
Karibu ujiunge nao.
 

Friday, September 21, 2012

Kali TV Online : This week's Around Town

This week Kali TV covers Tanzania Day at the Embassy of Tanzania in Washington DC.
Also Kali TV was at the Fest Africa celebration, celebrating African culture and heritage in Silver Spring, Maryland and gives you the highlights of Afro Exposure event in Silver Spring, Maryland.
ENJOY

Hafsa Kazinja kutumbuiza kesho Washington DC

Yule mwanamuziki wa Bongo Flava malikia wa Zouk Hafsa Kazinja Mtunzi wa wimbo uliotamba na unaoendelea kutamba Presure alioshirikiana na Banana Zorro atatumbuiza Jumamosi Sept 22, 2012 kwenye ukumbi mpya wa Moto Lounge Laurel
Hafsa aliyesema kuwa siku hiyo "kutawaka moto" amewaomba waTanzania na jamii yao kuhudhuria kwa wingi kuuzima nakuondoa pressure
Msikilize hapa chini Asante

Saturday, September 15, 2012

Hotuba kamili ya Mhe. Freeman Mbowe kwa waTanzania wa Washington DC



Freeman Mbowe akihutubia waTanzania
Sehemu ya umati uliohudhuria ukifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa chama Mhe. Freeman Mbowe 













Photo Credits: Abou Shatry wa Swahilivilla Blog
Hotuba kamili ya Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe alipokutana na waTanzania waishio Washington DC na vitongoji vyake jioni ya Sept 1, 2012.
Msikilize

Matangazo ya siku ya mTanzania Washington DC

Unaweza kufuatilia matangazo ya siku hii yanayoletwa kwenu na Bells Video Production LLC

Friday, September 14, 2012

Siku ya mTanzania Washington DC Sept, 15, 2012

Kwanza sikiliza UKARIBISHO WA Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar.

Mahali: Tanzania House, 1232 22Nd Street, N.W. Washington D.C.; 20037
Tarehe: SEPTEMBA 15, 2012
Kiingilio: BURE
Muda: (Saa 4:00 asubuhi – Saa 12 Jioni)

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Washington D.C. unawakaribisha Watanzania wote waishio maeneo ya DMV (District of Columbia, Maryland na Virginia) na vitongoji vyake, kuhudhuria siku ya Mtanzania, ambapo waTanzania watashiriki kuonyesha bidhaa, tamaduni, mila na desturi za Kitanzania kwa wageni (waMarekani na wa mataifa mengine) watakaotembelea ubalozini.

Madhumuni makuu ya Ubalozi kuandaa Siku ya Mtanzania
Kwanza ni kuwaelimisha wenyeji wa Marekani kuhusu Tanzania.
Pili kuitangaza zaidi Tanzania kwa kuvutia watalii wengi kutembelea Tanzania.
Tatu ni kutambulisha na kutangaza biashara mbalimbali na huduma zitolewazo na waTanzania waishio hapa Marekani.
Ubalozi unaomba Watanzania wenye bidhaa mbambali za Kitanzania, mapishi (wenye leseni), vikundi vya ngoma, muziki, mitindo, na waTanzania wenye kampuni za utalii, kujiandikisha ubalozini kuanzia tarehe 1 hadi 15 Agosti, 2012 kwa maandalizi ya siku hiyo.
Kwa Watanzania watakaopenda kujitolea kushiriki siku hiyo au kuonyesha bidhaa mbalimbali wajiandikishe kwa wafuatao:



Ubalozi unapenda kuwahamasisha Watanzania kuvaa vazi la Kitanzania.

                                   Karibuni Wote

IFUATAYO NI RATIBA YA MATUKIO YA LEO

Wednesday, September 12, 2012

Ndege zaidi ya ofisi. Ni zaidi ya uijuavyo

Kuna mengi ya kujifunza kuhusu hii ndege katika kipindi cha leo cha FRESH AIR cha NPR.
Nilipofika nyumbani nikaamua kuingia mtandaoni kufanya uchunguzi wa ziada, nikaisaka video ya National Geographic kuhusu ndege hii ya AIR FORCE ONE.
Kuna mengi ya kujifunza kuhusu uSIRI wa UWAZI wa WASIRI-WAWAZI hawa.
Ambacho sikujua ni kuwa ndege hii haijawahi kuchelewa kutua kwa zaidi ya sekunde tatu za muda uliopangwa.
I mean SEKUNDE TATU.
Duhhh!!!!!
Nimeifurahia
UKIWEZA, TAZAMA VIDEO HII ILI UJUE MENGI KUIHUSU

Monday, September 10, 2012

Ana kwa Ana na Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad


Mahojiano na Makamu wa kwanza wa Rais ZANZIBAR Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Katika mahojiano haya, Mhe. Hamad anaeleza kile kilichomleta Marekani, hali ya kisiasa Zanzibar
Anajadili maridhiano ya mwaka 2009 na kufafanua ni kwanini alipigania kura za chaguzi za 1995, 200 na 2005 lakini sio 2010 ambapo wengi waliamini ameshinda ukilinganisha na chaguzi zilizopita?
Anazungumziaje dhana ya ukubwa wa serikali Zanzibar ukilinganisha na idadi ya watu wakena ni kwanini tuwe na Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Zanzibar.
Nini kiini cha mgogoro wa sensa?
Na pia, kwa yeye kuwa sehemu ya serikali Zanzibar ilhali ni kiongozi wa chama cha upinzani Bara kunaleta mgongano wa maslahi?
Kwanini CUF inaonekana kupoteza mvuto nchini Tanzania?
Nini anazungumzia kuhusu mgogoro wake na Mhe. Hamad Rashid?
Zanzibar inakabiliana vipi na tatizo la ajira kwa vijana?
Je! Zanzibar ni nchi ya kijamaa ama kibepari?
Vipi anazungumzia tatizo la usafiri nchini Zanzibar?
 Elimu je?
Suala la Muungano lina utata gani?
Ni ipi tofauti ya Maalim Seif wa 1995 na huyu wa sasa?
Na mwisho nini wito wake kwa wote wamtazamao sasa?
Ungana nasi

Mkutano Mkuu wa Jumuiya DC

Karibu na mkaribishe na mwanajumuiya mwenzako

Wednesday, September 5, 2012

SIKU YA MTANZANIA Washington DC

Mahali: Tanzania House, 1232 22Nd Street, N.W. Washington D.C.; 20037
Tarehe: SEPTEMBA 15, 2012
Kiingilio: BURE
Muda: (Saa 4:00 asubuhi – Saa 12 Jioni)

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Washington D.C. unawakaribisha Watanzania wote waishio maeneo ya DMV (District of Columbia, Maryland na Virginia) na vitongoji vyake, kuhudhuria siku ya Mtanzania, ambapo waTanzania watashiriki kuonyesha bidhaa, tamaduni, mila na desturi za Kitanzania kwa wageni (waMarekani na wa mataifa mengine) watakaotembelea ubalozini.

Madhumuni makuu ya Ubalozi kuandaa Siku ya Mtanzania
Kwanza ni kuwaelimisha wenyeji wa Marekani kuhusu Tanzania.
Pili kuitangaza zaidi Tanzania kwa kuvutia watalii wengi kutembelea Tanzania.
Tatu ni kutambulisha na kutangaza biashara mbalimbali na huduma zitolewazo na waTanzania waishio hapa Marekani.
Ubalozi unaomba Watanzania wenye bidhaa mbambali za Kitanzania, mapishi (wenye leseni), vikundi vya ngoma, muziki, mitindo, na waTanzania wenye kampuni za utalii, kujiandikisha ubalozini kuanzia tarehe 1 hadi 15 Agosti, 2012 kwa maandalizi ya siku hiyo.
Kwa Watanzania watakaopenda kujitolea kushiriki siku hiyo au kuonyesha bidhaa mbalimbali wajiandikishe kwa wafuatao:



Ubalozi unapenda kuwahamasisha Watanzania kuvaa vazi la Kitanzania.

                                   Karibuni Wote

Tanzania Yangu....Yenye WIZARA ZISIZO NA MANUFAA KWA JAMII

Miaka ya karibuni tumeshuhudia kumomonyoka kwa maadili ya uandishi wa habari Tanzania. Fani nzuri na muhimu na kiungo muhimu kwa jamii yetu imeingiliwa.
Na kibaya zaidi, kama ilivyo kwa WIZARA nyingi zenye majina yasiyoendana na UTENDAJI wao, hatuoni lolote likitendeka inapotokea habari ikapotosha jamii.
Tunayo WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO ambayo KWA MTAZAMO WANGU ni kati ya WIZARA MFU ZAIDI NCHINI.
Dk. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Hii ni Wizara ambayo mpaka sasa sijajua inashughulikia vipi suala la HABARI kwa maana ya kuhakikisha NI MUAFAKA NA INAWAFIKIA WANANCHI WOTE.
Ni Wizara ambayo imeshindwa kufanya kazi ya kukuza (hata kutunza utamaduni) wa mTanzania ambao UNAMOMONYOKA KILA SIKU na pia ni Wizara yenye bajeti ya michezo lakini tunaona tunavyozidi kuwa KICHWA CHA MWENDAWAZIMU.
Vijana ndio haooooooo. Wanateseka na kuhaha kusaka maisha na HAKUNA (ama niseme hatuHABARIshwi lolote na Wizara hii kuhusu) mkakati wa kumkomboa kijana
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni moja ya WIZARA MIZIGO ZAIDI Tanzania hasa kwenye suala la michezo kwani zipo nchi (kama Marekani) ambazo HAZINA WIZARA ZA MICHEZO lakini zinafanya vema kwenye sekta hiyo.
Tanzania mpaka sasa hatujaona MKAKATI WA WAZI wa wizara hiyo kuhakikisha kuwa inatengemaa kwenye HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO.
Nikirejea kwenye fani yangu ya habari....huko ndio KUMESAHAULIKA
Wiki kadhaa zilizopita nilibandika picha ya kurasa ya mbele ya gazeti ambalo lilikuwa na habari inayopotosha jamii lakini HAKUNA LILILOSEMWA NA WIZARA.
Ninalowaza hapa ni kuwa,
  • Ni kwanini magazeti "yanayomchafua" Rais (mmoja) yafungiwe na kuacha haya yanayodanganya na kuharibu KIZAZI KIZIMA KISOMACHO?
  • Ni upi wajibu wa WIZARA YA HABARI nchini? Haionekani kusimamia upatikanaji wa HABARI SAHIHI NA MUHIMU kwa wananchi. Haionekani kuhakikisha kuwa wananchi wanaarifiwa kila kilicho sahihi. Haionekani kuhakikisha kuwa wananchi wa pande zote za nchi wanapata habari bila kujali kiwango cha maisha waishicho.
Leo hii nimekutana na habari nyingine (miongoni mwa nyingi) inayopotosha kabisa ukweli wa jitihada za kijana mwenzetu (Diamond) na bado Wizara imekaa kimya.
Labda hawajui uhakika wa safari yake, lakini wanaweza kuuliza na kuangalia UMUHIMU WA HABARI HII KWA JAMII.
HATA KAMA NI KWELI......
  • Kuna athari gani kwa Diamond kuitwa na Freemasons wa Marekani?
  • Ni maelezo gani yanayofuata baada ya kichwa hiki cha habari?
  • Habari hii ina athari gani kwa mamilioni ya wanaomfuatilia?
  • Na pengine ina athari gani kwa jamii nzima inayomuona kama kioo?
  • Si kuna uhuru wa kuabudu? Haujaingiliwa hapa (kama uongo huu ungekuwa kweli)?
Ninaloweza kuona ni kuwa (kama ilivyokuwa kwenye habari nyingi potofu) hakuna atakayewajibika kwa kuipotosha jamii namna hii.
Labda nikumbushe alichowahi kusema Malcom X kuhusu umuhimu wa vyombo vya habari kwani hii ni zaidi ya kazi kwangu.

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA

Tuonane "Next Ijayo"

NSSF WESTADI ndani ya DMV leo

USIKOSE.

Monday, September 3, 2012

Bin'Adamu....apumzikaye kusherehekea SIKU YA KAZI

Photo Credits: St Thomas Aquinas Pack 7 
Ni SIKU YA KAZI. Ama niseme kuthamini kazi. Ama siku ya wafanyakazi. Lakini vyovyote iwavyo, ni siku ambayo wengi wetu hapa Marekani tunakuwa na "siku ya mapumziko".
NDIO, DAY OFF katika kusherehekea SIKU YA KAZI.
Mmmmmhhh!!!
Umeona eeee?
Nilishaandika kuhusu kinyumenyume cha Bin-adamu katika kutenda, kunena na kuwaza. Kuwa kwanini tuwazishwe vitu kwa namna nyingine?
Kwanini nchi nyingi Afrika zisherehekee UHURU kwa staili ya gwaride kama la WAKOLONI WALIOTUTAWALA?
Kwanini siku ya wakulima isherehekewe mjini, na wapatao "day off" ni wale wasio wakulima ilhali wakulima hawapati sherehe yoyote siku hiyo?
Ni kwenye muendelezo huu wa KWANINI, najikuta naleta MASWALI YAFUATAYO, ambayo nilitumiwa na rafiki yangu, na si mawazo yangu.
TUMUWAZE BIN'ADAM NA UNAFIKI WA MAWAZO YA KIMATENDO.
Soma kisha uwaze, "bin'adamu anawaza nini kutenda atendayo?"
Japo nilitumiwa NICHEKE, lakini yaliniwazisha pia

-Why do supermarkets make the sick walk all the way to the back of the store to get their prescriptions while healthy people can buy cigarettes at the front?
-Why do people order double cheeseburgers, large fries, and a diet coke.
-Why do banks leave vault doors open and then chain the pens to the counters.
-Why do we leave cars worth thousands of dollars in our driveways and put our useless junk in the garage.

EVER WONDER .......
-Why the sun lightens our hair, but darkens our skin?
-Why can't women put on mascara with their mouth closed?
-Why don't you ever see the headline 'Psychic Wins Lottery'?
-Why is 'abbreviated' such a long word?
-Why is it that doctors call what they do 'practice'?
-Why is lemon juice made with artificial flavoring, and dish washing liquid made with real lemons?
-Why is the man who invests all your money called a broker?
-Why is the time of day with the slowest traffic called rush hour?
-Why isn't there mouse-flavored cat food?
-Why didn't Noah swat those two mosquitoes?
-Why do they sterilize the needle for lethal injections?
You know that indestructible black box that is used on airplanes? Why don't they make the whole plane out of that stuff?!
-Why don't sheep shrink when it rains?
-Why are they called apartments when they are all stuck together?
If flying is so safe, why do they call the airport the terminal?

HIVI TUNAWAZA NINI?

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

"Injinia" MIMI na ukarabati wa "nyumba TANZANIA"

PHOTO CREDITS: Cool fun pics
TANZANIA YANGU.
Naitazama Tanzania na matukio kedekede yanayoikumba.
Natazama namna ambavyo inazidi kumomonyoa imani na matumaini kwa wananchi.
Labda wananchi hawajui ukweli na wanaendeshwa na TETESI.
Lakini LABDA wenye kujua ukweli hawajali kuhusu TETESI zinazoiharibia sifa ya kweli nchi yangu.
Kila siku ni matukio, na kila matukio ni KUUNDIWA TUME na kila tume inahusisha wataalamu ambao kwa mujibu wa sheria wana haki ya kuwemo kwenye tume licha ya kuwa WAMO KWENYE MFUMO ULIOHUSIKA KIMAKOSA.
Ni vigumu sana kuunga tume huru nchini bila kuhusisha sehemu ya mfumo uliohusika katika kosa linaloundiwa tume.
Lakini hii haimaanishi kuwa WENYE MADARAKA WANATUMIA MADARAKA YAO VIBAYA.
Linamaanisha kuwa wenye madaraka wamepewa madaraka kuliko wanayostahili.
Ndio nchi yangu TANZANIA.
Ambayo pia naitazama kama NYUMBA ambayo sisi wananchi ni wakaazi na rasilimali zeti ni mali zilizomo ndani.
Ni nani mwenye jukumu la kuijenga Tanzania yetu iwe bora na makini?
Ni sisi wananchi. Wakaazi wa "Tanzaniani" na hata wale waliotoka "ndani" kwenda kusaka riziki nje lakini wanajua kuwa watarejea "nyumbani"
Jambo moja muhimu la kutambua ni kuwa, KABLA HATUJAIJENGA NYUMBA IITWAYO TANZANIA, NI LAZIMA TUIBOMOE. MSINGI WAKE UMEHARIBIKA HIVYO UKARABATI WOWOTE USIOHUSISHA MSINGI NI KUPOTEZA MUDA NA PESA NA MSINGI WOWOTE UTAKAOKARABATIWA BILA KUVUNJA KILICHO JUU NI MIUJIZA.
Ni LAZIMA tuubomoe msingi wa nchi, kisha tuijenge upya.
MIMI na WEWE tuna wajibu mmoja. Kujua ni vipi tutaweza kuibomoa nchi sasa bila kuathiri "watu na mali" zilizo ndani kwani tusipofanya hivyo, "mali na watu" hao wataangukiwa na kuta na kuwa hasara zaidi mbele.
TUCHUKUE HATUA....HATUA SAHIHI...HATUA MAKINI.
  • Tukibomoa kwa umakini, tutapunguza gharama na hata baadhi ya vifaa vya ujenzi vitaweza kutumika tena.
  • Tusisubiri MJENZI aliyeijenga kwa makosa atuambie kuwa alikosea. Lakini tusimpuuze na kutomshirikisha kwenye ukarabati huu.
  • Tusimtishe kuwa tutamfunga kwa makosa ya ujenzi wake lakini tuhakikishe kuwa anajua kosa lake na halirudii tena.
  • Tusitafute sifa kwa kumshutumu mjenzi wa sasa na kusahau kutafuta SIFA ZA ATAKAYEKARABATI.
MWISHO....
Tukumbuke kuwa NI RAHISI KUBOMOA.
Na hata asiyeweza kubeba hata tofali, asiyejua kusoma ramani, asiyefahamu kuchanganya saruji na mchanga na hata asiyejua KWANINI TUNATAKA KUBOMOA anaweza kuwa m'bomoaji mzuri....LAKINI SI MJENZI.
Ninalomaanisha ni kuwa...SI KILA MWENYE UJUZI WA KUBOMOA ATAWEZA KUJENGA.
Tuibomoe Tanzania ili tuweze kuijenga, lakini kabla hatujaibomoa, tuhakikishe tuna mtu sahihi, mwenye ujuzi sahihi, vifaa sahihi, mpango sahihi na maelezo ya muda sahihi atakaotumia kuijenga Tanzania yetu.
La sivyo, ukarabati utakuwa mateso zaidi ya nyumba mbovu tuliyokuwa nayo.

Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!!!!!!!!


Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA


Tuonane "Next Ijayo"

Sunday, September 2, 2012

Tanzania ni zaidi ya itikadi- Benjamin Mwaipaja

 Katibu Uenezi na Itikadi wa CCM-DMV Bwn. Benjamin Mwaipaja (kati) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA TAIFA Mhe. Freeman Mbowe. Kushoto ni Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Bwn Benjamin Mwaipaja, amewaomba wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa kuweka utaifa juu ya itikadi zao katika kuhakikisha kuwa nchi yetu inasonga mbele.
Katibu Uenezi na Itikadi wa Tawi la CCM DMV Benjamin Mwaipaja akiwa na Kada wa Chadema Mzee Emmanuel Muganda katika mkutano huo.
Akizungumza na blogu hii punde baada ya kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na tawi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) la Washington DC, Bwn. Mwaipaja, ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM tawi la Washington DC amesema kuwa licha ya tofauti za itikadi zilizopo baina yetu, sisi wanaDiaspora tunastahili kukumbuka kuwa tuna wajibu wa kuijenga Tanzania BORA NA IMARA kwa manufaa yetu, ndugu zetu walio nyumbani sasa na vizazi vijavyo.
Sikiliza mahojiano yangu na Ndg. Mwaipaja HAPA chini
Katika mkutano huo uliofanyika jana usiku katika kitongoji cha College Park jimbo la Maryland Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi na Mbunge wa Hai ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe walihudhuria.
PHOTO CREDITS: Abou Shatry wa SWAHILI VILLA BLOG

R.I.P Kaka David Mwangosi

Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Bwn. Daud Mwangosi 
Nimesoma kuwa mwanahabari mwenzangu David Mwangosi ameuawa kwenye vurugu kati ya Polisi na wafuasi wa CHADEMA. Amefia kazini
Kwa wale wenye fikra fupi kuhusisha,......kilichomkuta Kaka yetu ni sawa na ....
Rais kuuawa Ikulu.
Askari kuuawa vitani.
Mbunge kuuawa bungeni.
Daktari kuuawa chumba cha upasuaji.
Mtangazaji kuuawa studio.
Mkulima kuuawa shamba.
Mwalimu kuuawa darasani.
Ukisoma orodha hiyo, utagundua kuwa japo wote watakuwa wamekufa wakitekeleza majukumu yao, wapo watakaothaminiwa zaidi ya wengine kwa kuwa TUMEJENGA MATABAKA YA KAZI.
R.I.P Brother Mwangosi 

LAKINI NILIANDIKA HAYA MIAKA 3, MIEZI 2 NA SIKU MOJA KABLA YA KUUAWA KWA MWANDISHI MWENZANGU Bwn. DAVID MWANGOSI

Niliipa kichwa kisemacho TUNATAKA KUWAAMINI POLISI, LAKINI HAWAAMINIKI.
"Kuna matukio mengi yanayotendwa na askari polisi nchini ambayo yanasikitisha saana. Hatujui ulipo mstari kati ya usalama wa raia na siasa.
Kumekuwa na mambo mengi ambayo yanapunguza heshima na imani ya wananchi kwa jeshi hili. Kibaya zaidi ni kuwa Polisi HAWAAMINIKI katika yale watendayo. Si tunakumbuka yaliyotokea wakati wa mauaji yaliyoanzisha kesi ya kina Mhe Zombe?
Tuliambiwa nini na tukaja kugundua nini? Unadhani watu wanafikiriaje kuhusu jeshi lao?
TUMESHUHUDIA wasio na hatia wakihukumiwa, wakiuawa na hata kusingiziwa mambo mbalimbali. Unafika wakati WANANCHI WANAKOSA IMANI, UPENDO NA HESHIMA kwa jeshi hili na kuamua kujichukulia hatua mkononi.
Hili si jambo jema hata kidogo lakini badala ya kujitahidi kuwatisha na kuwafunga wasio na hatia, JESHI LA POLISI LIBADILI, LIBORESHE NA KUHESHIMU UTENDAJI WAKE WA KAZI NA KUTENDA HAKI KWA WANANCHI"


Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA


Tuonane "Next Ijayo"