Friday, October 31, 2008

Them, I & Them. NASIO ...........No Love

Nasio Fontaine
"They talking about Love, yet they got no love at all, talking bout peace, yet all i see is war. You talk about this, you talk about that. Poor people just a suffer (are suffering) while you live out FAT"
Ni maneno toka kwake Nasio Fontaine Mmoja wa wanamuziki wa Roots Reggae ambaye amesimama imara katika kutetea haki za wanyonge, kufumbua maovu ya viongozi na watawala na kufundisha njia m'badala za kujikomboa kwa tabaka likandamizwalo.
Namzungumzia Nasio na wimbo huu No Love Ijumaa hii kutokana na yale yaliyotokea wiki hii barani mwetu. Kwanza ni mkutano wa Bunge la Afrika na pili rabsha za Congo.
Tumeona viongozi wanavyosimama na kuzungumza kuhusu amani ambayo hawaonekani kuwa na nia ya kuisaka. Wanakwenda mikutanoni kuendesha vikao vya amani wakilipwa pesa nzuri na kuota vitambi wakati amani izungumziwayo haipo na wenye uhitaji wakiendelea kutaabika na machafuko hayo. Wengine bila hata aibu wanasema mapigano hayo wanayaleta kutaka kuleta Demokrasia nchini mwao na ndio maana Nasio kwenye wimbo huu akasema "you coming with your bribes and treachery to murder in the name of democracy. You living in your false pride and Luxury, while millions (are) dying in their poverty"
Wanapoomba kura wanakuwa na ahadi mbalimbali zenye kuwapa matumaini watu. Wanaahidi yale ambayo hawawezi kutekeleza wakijua wazi kuwa maslahi yao yanatangulia mbele na ndio maana hawajali vifo na ukimbizi utokanao na yale wafanyayo. Nalo hili Nasio aliliona aliposema "The wickedman ain't got no love for humanity, yet they got so much love for their vanity. Their need for way is rising high, while the sufferers are left to die (in starvation and hunger). Vote for me i'll set you free, are lies and hypocrices"
Nawasikiliza viongozi walivyoanza fitna na majungu ya kujifanya wanachukua kila hatua kusitisha machafuko yaendeleayo barani Afrika kwa kupanga safari nono za kwenda kujadili amani isiyopatikana.
Kama alivyosema Nasio nami ndivyo niaminivyo kuwa LOVE AND LOVE ALONE WILL CONQURE na sina shaka kuwa wenye kuanzisha haya kwa manufaa yao siku yao yaja.
Pole kwa wale wote ambao kwa tamaa za viongozi wao wamejikuta wakiwa wahanga wa machafuko ya namna moja ama nyingine.

Waweza kujua mengi juu ya Nasio Fontaine kwa kubofya http://www.nasioreggae.com/main.html

BLESSINGS
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**

Thursday, October 30, 2008

Uchaguzi wa Vijana CCM Wilaya ya Misenyi

Kamanda wa vijana na CCM wilayani Misenyi Protace Ishengoma akiteta jambo na Katibu wa CCm wilayani Misenyi Joseph Kagashe muda mfupi la kufungua mkutanio wa kuwachagua viongozi mbalimbali wa UVCCM wa wilaya ya Misenyi.
Mwenyekiti wa CCM wilayani misenyi Paul Mgomba akifurahia jambo na kamanda wa vijana wa CCM wilayani Misenyi Protace Ishengoma baada ya kufungua mkutano wa uchaguzi.
Habari na picha toka kwa Audax Mutiganzi na Mukebezi Rugarabamu. Misenyi Kagera
Kwa niaba ya wanaChangamoto wote, nawatakia mafanikio mema katika kuanzisha na kuendeleza mema mengi kwa manufaa ya jamii nzima.
Mzee wa Changamoto

Wednesday, October 29, 2008

"You looking good from afar, but you're far from looking good"

Rais Joseph Kabila
Gen Laurent Nkunda
Mi sijui kiapo chao kikoje ama kimeandikwaje, lakini najua asilimia kubwa (na nahisi na kiapo chao pia) kimesema juu ya kuwatetea na kuwalinda wananchi na mali ya nchi kwa manufaa ya wananchi. Leo hii wananchi ndio wanaokimbia makazi yao, wanakimbia kazi na maisha yao, wanaachana na familia na ama ndugu zao kwa kuwa tu kati ya wawili hawa hakuna atimizaye wajibu wake.
Nasio (ambaye ndiye mwenye sentensi hiyo hapo juu) alisema "war is not a solution, never was and never will it be so" na Luciano akaimba "they kill the wicked and still more rises, without proper justices we can't be suprised".
Kwa hiyo kumbe dawa si kuwaua waitwao waasi kama haki na usawa havitendeki nchini Congo na kwingine ulimwenguni maana "wengine wataanzisha vita".
Mmhhhhh!!!!!

Yalofichwa kwa viongozi yalifunuuliwa kwa wasanii.

Lazima kuna atakayebeba laana ya kilio hiki picha toka http://www.edondaki.blogspot.com/
Najaribu kupata pa kuanzia lakini nahisi ntaanza na swali la ni nini hiki?
Alisema Galinoma na nikaandika katika kipengele cha kila Ijumaa cha THEM, I & THEM niki-quote sentensi yake alipoimba "only this time, the downpressor man happens to be my own brother. Africans where are we going from here?". Ndiyo maswali tunayotakiwa kujiuliza kila wakati kwani ni sisi sisi tunaouana kila iitwayo leo kwa kutaka madaraka tunayopangiwa na wasioathirika na vita hivi. Namkumbuka Lucky Dube alipoimba kwenye wimbo wake uliobeba ajina la albamu wa Victims akionesha tofauti ya maovu waliyotendewa Babu zetu na wakoloni na ya sasa ambayo walio nje wanaangalia tunavyochinjana bila huruma akisema"Bob Marley said How long shall they kill our prophets while we stand aside and look. But little did he know that eventually the enemy will stand aside and look while we slash and kill our own brothers, knowing that alreadythey are the victims of the situation. Still licking wounds from brutality, Still licking wounds from humiliation" Kinachosikitisha ni kuwa anayesababisha kilio, majeraha na madhara haya ya kiakili, kimwili na kimazingira ni ndugu yetu. Ambaye anasema anapigania haki ya yule anayemuua. Na kati ya hao ni wale tuwaitao VIONGOZI. Nasio Fontaine aliimba kwenye wimbo wake wa Babylon You Doom alipowazungumzia hawa wanaosimama kupinga vita ilhali silaha zenye nembo za nchi zao ndizo ziuazo watu ambao viongozi wao wanaendelea kuua kwa kisingizio cha kusaka maisha mema kwa wawauao aliposema "babylon you speak of peace yet you make more war, you suppress the innocent to deceive the poor, death and destructions, hungry Baby Mother breasts run dry, yet you plan more war in your private sessions". Akaendelea kusema "you building more bombs and guns, yet babies are dying for hunger. We're the victims of your oppression. Blood of the innocent that you slaughter is upon your hands. You gave the gun, you set the fight, you sit aside and watch the slaughert."
Kuna mengi yaliyosemwa hapo awali na yanaendelea kuimbwa na kusemwa lakini sijui kwanini "viongozi" hawabadiliki na kuthamini utu na utaifa kuliko pesa.
Well. Kuna pande mbili. Ya wenzetu kaka zetu ambazo kwa manufaa yao na biashara za watengeneza silaha wanaamua kutothamini uhai wa wenzao na kuteketeza jamii kwa kisingizio cha kuleta maendeleo nchini mwao. Morgan Heritage waliimba kwenye swimbo wao so much more to come wakisema "these are the days known as eve of destructions, with POLITRIX just leading every nation" na ndilo tuonalo sasa. Wanaoathirika ni wale ambao hata hawajui maana na sababu ya vita. Watoto na kinamama na wenye ulemavu na mahitaji ya ziada ndio wanaobaki kuwa wahanga wa haya machafuko. Kusema hakumaanishi uoga, ila ni kuwa sauti ya wale wasioweza kupata nafasi ya kuandika haya maana wako kwenye mbio za angalau kusogeza dakika za maisha yao.
Kina mengi ya kuandika na kuna mengi ya ku-quote toka kwa wasanii hawa wema walioitetea na wanaoitetea Afrika na pengine wengine wanadhani kuandika haya ni ndoto kwani hayawafikii wahusika, lakini Tanya Stephens alisema "may be hoping for a change is a dream, may be life ain't as bad as it seems, but if dreaming is the best i can do then i'll be dreaming my whole life through." Nami ntaendelea kuota na kuomba kwa kuwa amani ni jambo nimuombealo kila mmoja. Si kwa kuwa naogopa kifo, bali kwa kuwa nawasilisha maneno ya wasanii wanaowasemea wasioweza kufanya hivyo. Lucky katika War and Crime alisema "I' m not saying this, because I' m a coward. But I' m thinking of the lives, that we lose everytime we fight Killing innocent people Women and children yeah Who doesn' t know about the good Who doesn' t know about the wars"

WE NEED TO "RISE UP, WISE UP, WAKE UP AND SHAKE UP"

Tuesday, October 28, 2008

Una bahati hauko kwetu

Kwetu ni Afrika na naamini kokote kule ndani ya kwetu (Afrika) wangehitaji maelezo ya kina ya huu wimbo wako. Yaani kumuimba Rais namna hii??!!!! Ila ndo ukweli ulivyo. Sijui ni CHANGAMOTO kwa wasanii wa kwetu kuimba ukweli (unaoweza kuwatoa kafara) ama kwa wasanii wa nje kama Alecia Beth Moore (Pink) kujitahidi ama kuficha ama kukata makali ya ujumbe ndani ya nyimbo zao.
Sina jibu, ila nisemalo ni kuwa hii kila mtu atai-judge kwa mtazamo wake. No wonder video hii iliyowekea maneno kwa lugha mbalimbali ina mamilioni ya watazamaji huko You Tube. Click hapa uone yaloimbwa kisha ufikirie ingekuwa kule kwetu huyu angepewa zawadi gani http://www.youtube.com/watch?v=mQYHKILXD4k

Monday, October 27, 2008

Kinachousibu muziki na sanaa ya asili nchini

Sisi Tambala waliporejea na kombe toka China

Kikundi cha Afrikali Ngoma Group
Hivi karibuni bloggers Michuzi Jr na Dada Sophy wameuliza swali linalorandana kuhusu muziki na ama wasanii wa miziki na kazi za asili. Sio hawa tuu, bali hawa ni wa karibuni ambao wameweza kuuliza maswali yaendanayo na hayo hapo juu. Kwa kaka Ahmad ameuliza juu ya mwenye dhamana ya kuuinua muziki wa asili nchini (BOFYA HAPA) ilhali Da Sophy yeye kauliza tunavyowaenzi wasanii wetu mahiri wa muziki wa asili kama kina Hukwe Zawose (BOFYA HAPA KUUNGANA NAYE)
Well, nilibahatika kushuhudia na kushirikiana kidogo na vikundi kadhaa vya muziki wa asili nikiwa nyumbani na vikundi kama Sisi Tambala (ambacho baadhi ya wasanii wake nimewaona Afrikali), Parapanda Arts, Simba Theatre na wengine kadhaa na nilipata ufahamu na uzoefu mzuri saana juu ya sanaa hii. Lakini ninapojiuliza kinachoisibu sanaa hii nzuri zaidi nchini naona makwazo katika sehemu kuu nne.
Kwanza SERIKALI ina dhamana ya kuendeleza utamaduni wetu (japo nimechoka kusema lakini sitokoma) na ina wajibu wa kujenga ukumbi wa kisasa kwa shughuli za sanaa ama kusimamia mkataba halali (na hapa napata shaka kidogo) utaowezesha wawekezaji kujenga ukumbi mwanana. Nakumbuka Rais Kikwete alipotembelea Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo mwanzoni mwa mwezi Machi 2006 na kuwapa changamoto ya kujenga ukumbi wa kisasa akisema kuwa ni aibu kuwa hatuna ukumbi wa kisasa. Bofya http://www.ippmedia.com/ipp/raha/2006/03/19/62374.html . Pia SERIKALI inastahili kuweka mwongozo wa usimamizi wa Chama ama chombo kitakachosimamia muziki na wanamuziki wa muziki huu kama ambavyo imefanya kwa FAT, TOC, TAA na vingine. Pia SERIKALI inastahili kusaidia katika mafunzo na uendelezaji kwa kozi na wataalamu wataowezesha wasanii na vikundi kujua namna nzuri ya kujiajiri na kuendesha shughuli zao. Kulipa Wakufunzi kama ambavyo imefanya kwa wengine kama Maximo
Pili ni WANANCHI ambao kwa namna moja ama nyingine wameingiwa na ule "utumwa wa kiakili" wa kuthamini na kusaidia kile kiachacho asili. Wananchi wanastahili kutembela vikundi na wasanii hawa kuona namna inavyowagharimu kutengeneza nyimbo na kazi zao ili waweze kuthamini kazi zao. Wananchi wengi hawahudhurii sanaa za nyumbani na inashangaza kukuta sanaa za nyumbani zinathaminiwa saana nje ya nchi ama na watu toka nje ya nchi huku watu wengi wakiendelea kushabikia mengi yabomoayo jamii kwa kuwa tu ni "maisha ama mfumo wa maisha ya kimagharibi" Nani anayewakumbuka Tatunane?Nani ameshawatembelea Simba Theatre, Wanne Star, Parapanda na wengine kuona kazi zao? Unadhani Ngoma Afrika wakija fanya onesho nyumbani watapata washabiki kama wafunikavyo Ujerumani? Uliona mapokezi kiduchu kulingana na kazi waliyofanya waliyopata Sisi Tambala waliporejea toka kwenye 7th China Folks Arts Festival ambako walipata ushindi wa Bara la Afrika na Ushindi wa jumla katika mashindano yaliyoshirikisha mataifa 22? Hadhira ya kiTanzania inastahili kuamka na kuanza kuthamini cha nyumbani kwanza.
Tatu ni VYOMBO VYA HABARI ambavyo kwa namna moja ama nyingine (vingi na si vyote) vimekuwa vikikimbilia kwenye mapato ya haraka hata kama hakumaanishi kuendeleza muziki, sanaa ama wasanii wetu. Vyombo vingi vya habari vimekuwa havitoi kipaumbele kwa sanaa na wasanii wa muziki na kazi za asili na hili limewafanya wale wanaotegemea kila kitu toka kwao kutopata habari kamili na sahihi kuhusu sanaa. Na kuna ambavyo hutoa habari zisizo sahihi kwa kuwa tu anayehabarisha hana ujuzi ama historia ama hisia na habari za sanaa. Na hii hufanya mengi mema yasitambulike kwa kuwa upeo wa mwandishi, mtangazaji na ama mtayarishaji ni mdogo katika hilo ashughulikialo.
Na mwisho ni WASANII wenyewe. Wasanii wanastahili kushirikiana kuanzisha ama kuendeleza Chama ama umoja wenye uhai na nguvu utakaowafanya watambulike na kuthaminika mbele ya jamii. Kuanzisha Tovuti (website) ama namna ya kisasa ya kuweza kuonesha kazi zao ulimwenguni na kisha kuwa na maelewano katika viwango vya maonesho. Kukiwa na kutoelewana, wapo watakaopata tenda kwa kuwa tu wako "cheap" na hiyo haimaanishi kuwa wanathaminika, ila wanapatikanika. Wasanii pia wanastahili kushikamana katika hili na kwa kufanya hivyo watakuwa na sauti kubwa katika jamii na vyombo vya habari, kisha watarejesha heshima yao, kazi yao na mwisho sanaa ya Taifa kwa ujumla.
Luciano alisema "never forget where we're coming from. Charge out your destination and let's use what we have for the uplift of the nation"
Hatujasahau asili yetu, malengo ni kwenye thamani ya sanaa hii na kwa wale waliopo kwenye sanaa kwa msaada wa wadau wengine twaweza kutumia kila tulichonacho kulinyanyua taifa katika sanaa hii.

Ni CHANGAMOTO YETU sote kuangalia tulipoanguka na kisha kurekebisha. Ndivyo nionavyo tatizo na yawezekana namna nilionavyo ndilo tatizo.

Friday, October 24, 2008

Them, I & Them: JUSTINE KALIKAWE .......Kitendawili

Marehemu Justine Kalikawe alipotwaa tuzo ya msanii bora wa ReggaeSafari ya mwisho ya Justine, nyumbani kwake Kitendaguro Bukoba

Nikiwa na baadhi ya wasanii walioshiriki wimbo ulioitwa HAKUNA (urejee hapa). Hapa ni ndani ya Bacyadr Studio kurekodi Video ya wimbo huo uliokuwa maalum kumuenzi Justin Kalikawe

Tukiwa Idara ya Habari Maelezo (2003) na Ras Pompidou, Jah Kimbuteh, Ras Inno, Bi Georgia (Mjane wa Justine) na meneja wake wa zamani Allen Mbaga kuzungumzia Tamasha la HAKUNA lililomuenzi Justine
Jana ni kati ya siku nilizokumbuka meengi saana kuhusu nyumbani. Na ni katika kuwaza huko nikajikuta nawaza SAFARI YANGU YA MAISHA na kujiuliza msururu mzima wa matukio ya maisha yangu. Nikawaza nimetoka wapi, niko wapi na pengine ninaenda wapi. Kama ilivyo kwa wengi wetu, tunaweza kuwa na majibu ya maswali ya tulipotoka na pengine tulipo (kwa mtazamo wetu0 lakini tuendako bado ni KITENDAWILI. Na ni kitendawili hicho tunachojiuliza ambacho kina meeengi yanayohitaji muda zaidi ya tujipao katika kusaka majibu. Nilipofikiria tulikotoka na kilichonileta huku na ninavyosonga ki-umri na kuwaza mustakabali (future) ya maisha yangu na familia, nawaza mengi. Lakini ni jana hiyohiyo ambapo Kaka Gotha Irie alinitumia picha ambayo tulipiga mwaka 2003 wakati tukirekodi video ya wimbo HAKUNA wake Justine Kalikawe. Hivyo nikaenda kumsikiliza Justine na kukutana na wimbo huu ambao nimeona nishirikiane nanyi kwa mara nyingine.

"nilikuja kutafuta ugenini, nikazoea pakawa ni nyumbani, sasa ninaelekea uzeeni, nibaki huku au nirudi nyumbani. Nilioa nikazaa na watoto, na nilipotoka kwao ni kama ndoto; lakini najiuliza siku nikirudi kwetu, niende nao au wabaki huku"
Hayo ni maneno anayoanza nayo mwanamuziki aliyepata kufanya vema saana katika miondoko ya Reggae nchini Tanzania Marehemu Justine Kalikawe katika wimbo wake Kitendawili. Kama ilivyo kwa nyimbo nyingi ambazo zinakuwa na UJUMBE HALISI wa maisha kwa hadhira, wimbo huu bado unaendelea kuwa na maana na mguso uleule kwa wale walio mbali na nyumbani na hasa wale walioanzisha familia ambapo ikifika suala la maisha baada ya kustaafu unarejea kujiuliza kama alivyojiuliza Kalikawe.
Haijalishi alitunga wimbo huu akiwa wapi, ama akijifikiria kama aliye wapi, lakini kwa kuwa alifanya kile afanyacho vema zaidi kwa kutunga nyimbo zenye uhalisia kwa jamii, bado sasa hivi ndugu wengi tulio mbali na nyumbani tukiusikiliza wimbo huu tunapata hisia halisi ya alichoeleza Justine na kuweza kujiuliza maswali ambayo naye aliuliza kwenye utunzi wake huu, bado ujumbe wake unawagusa wengi ambao kwa bahati mbaya kutokana na mfumo wa maisha ya sasa wameelekea popote duniani kwa namna yoyote kusaka chochote ili kuweza kurejesha uwekezaji nyumbani, na kama ilivyo kwa binadamu yoyote, unapofika mahali ndio unapoanzisha urafiki na "udugu" na uliokutana nao, na wakati muafaka ukifika unaanzisha familia na kwa majaaliwa ya Mungu unapopata watoto inakuwa baraka, lakini baadae waweza kujiuliza kama aliyojiuliza Kalikawe kuwa "nilikotoka niliishi na wazazi, babu na bibi, mjomba na shangazi, lakini huku mimi na familia, ndugu wengine ni eneo la kazi eeeee; katikati kuna bahari, tena ni mbali elfu kumi maili, nikisafiri nafika alfajiri tena ni mbali natumia utajiri eee"
Sijui la kusema, lakini namkumbuka Justine kama moja ya nguzo za muziki wa Reggae mkoani Kagera na Tanzania kwa ujumla. Alitumia lugha zake za Kihaya na Kiswahili kufikisha ujumbe aliokusudia kwa jamii husika na mara zote ALIELIMISHA, AKIBURUDISHA NA AMA KUIFUNZA JAMII KUJIKOMBOA KUTOKA KATIKA UTUMWA WA KIAKILI.
Justine alifariki ghafla mwezi wa nane mwaka 2003 katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Kagera mjini Bukoba miezi michache baada ya kurejea kutoka ziara ya kimuziki nchini Denmark. Aliacha mjane Georgia na watoto wawili Abayo na Niwe na mpaka mauti yanamkuta alikuwa ndiye msanii mwenye albamu nyingi zaidi za Reggae nchini Tanzania (8 za audio na 3 za video katika miaka 16 aliyodumu katika muziki wa Reggae). Katika kumuenzi, wasanii nyota wa Reggae nchini walitunga wimbo wa HAKUNA na kuandaa Tamasha maalum la kuenzi kazi na maisha ya Justine lililofanyika Don Bosco. Tulishapata kujadili FIKRA PEVU / MAONO ya Justine Kalikawe katika wimbo wa HAKUNA kwa kuhusisha na uchaguzi ujao HAPA
RIP Justine Kalikawe
Bofya player kusikiliza KITENDAWILI hiki


Thursday, October 23, 2008

MTAZAMO: Pale SERIKALI inapochochea ujinga

Choma tu hivyo vya zamani, twawaletea vipya
Ikulu ya kwanza Tanganyika ilivyotelekezwa huko Bagamoyo
Majengo ya kale "yakipigwa nyundo" kupisha ujenzi mpya huko Tanga
Asante ya picha kwa Da Chemi na MichuziJr
Kama wanangu watakua bila kuona historia ya asili yao basi watapungukiwa ufahamu wa asili yao hali itakayowafanya wawe kama WAJINGA. Na ni aibu kwa Taifa kuwa na kizazi ambacho sio tu hakioni historia yao, lakini yawezekana hata wasiweze kuisoma maana inateketezwa. Haya nimeyaandika baada ya kushuhudia taswira za hivi karibuni ambapo (kama uonavyo taswira hapo juu) vitabu ambavyo vilitumika kuwaelimisha viongozi na wakubwa zetu na pengine sisi wa rika la kati vinateketezwa kwa kuwa wameamua kuja na mitaala mipya / vitabu vipya. Pia majengo ya kale na sehemu za kihistoria zinazidi kuteketezwa kila iitwayo leo kupisha ujenzi wa "vikwangua anga".
Marcus Garvey alisema "A people without the knowledge of their past history, origin and culture is like a tree without roots."
Kama nasi tunakuwa na sehemu ya harakati za kutokomeza historia na na kuwafanya watoto wetu wawe wajinga, basi nasi ni wajinga na tunaochochea ujinga kwa vizazi vijavyo na kama serikali yenye jukumu, usimamizi na ama mamlaka ya kutunza kumbukumbu muhimu za kihistoria kwa ajili ya vizazi vijavyo haifanyi juhudi zozote kutunza historia hizo, basi nayo (Serikali) inachochea ujinga huu.
SERIKALI kuchochea ujinga? Ndio. Wala hujasoma kimakosa. Serikali ndicho chombo chenye mamlaka ya juu zaidi kimaamuzi nchini na chenye uwezo wa kuhakikisha, kuhalalisha na hata kusimamisha mambo mengi yanayotendeka nchini kwa manufaa ya wananchi na hasa vizazi vijavyo.
Lakini kupitia Magazeti tando na habari katika tovuti mbalimbali tumekuwa tukishuhudia ama kusoma juu ya kuharibiwa kwa historia na kumbukumbu nyiingi ambazo zina manufaa saana kwa wanetu na wajukuu wetu wa kisingizio cha "kupisha maendeleo" mapya yajayo. Kwa mtazamo wangu (na narejea tena mtazamo wangu) huu ni Ujinga maana kwa hakika kama walivyosema Morgan Heritage kuwa "every man must know their past, so we can stand firm in the future" nasi tulistahili kuyatunza haya ya kale kwa gharama zozote kwa manufaa ya vizazi vijavyo ili nao baadae waweze kutambua na kuoanisha walipo na walipokuwa wazazi wao. Bila kuwa na cha kuoanisha unadhani watatambuaje na kupangaje mustakabali wao? Ninapoona habari zainazoonesha kuharibiwa kwa sehemu za kihistoria kama ilivyo ubomoaji wa Majengo ya kale huko Tanga kwa kisingizio cha kupisha ujenzi mpya, ama utelekezwaji wa sehemu za kihistoria ambazo watalii na wajukuu zetu wangejifunza mengi juu ya tulikotoka mpaka harakati zetu za uhuru (kama ilivyoripotiwa na Michuzi Jr (hapa)] na sasa nisomapo habari juu ya kuchomwa kwa vitabu vya zamani vilivyotumika katika kutufundisha ili kupisha uingizwaji wa vitabu vipya ambako yaonekana kulianza zamani saana kama ilivyoandikwa na Da Chemi kwenye intro ya habari ya Da Subi (hapa) na Da Subi kwenye blog ya jamii ambako wengi wameona hili kama tatizo (hapa) nahisi kukerwa.
Najiuliza:
1: Ni kweli kuwa Serikali imeshindwa kuyaona haya yanayoonekana machoni mwa ulimwengu wote?
2: Na kama hawakuamua / kuruhusu yatendeke na hawazuii, kwanini nisiseme wanachochea ujinga?
3: Mbona nchi nyingi zinatunza saana "ukale" wao na kujivunia? Tunaona miji ikiitwaa Historical towns ama Old Towns ama Historical Streets ili kuonesha walikotoka na kwa hakika ni kati ya sehemu aghali kuishi ama kununua nyumba zake na zina masharti saana katika kuzikarabati maana hawataki kuharibu mtazamo wa kile kilichokuwapo.
4: Kweli nasi hatulioni hili?
Aibu kwetu na inashangaza saana.
Kwa bahati mbaya sana naona KAMA KUPOTEZA HISTORIA NI UJINGA, NA HAYA YANATENDEKA KWA MGONGO WA SERIKALI, NA HAKUNA KIONGOZI WA SERIKALI ANAYESIMAMA KUYAPINGA AMA KUKANUSHA UHUSIKA WAKE KATIKA HILI, BASI KWA HIARI AMA BAHATI MBAYA NAIONA SERIKALI IKICHOCHEA UJINGA.

Ni mtazamo tuuuuuu na ndivyo nionavyo tatizo. Labda hilo ndilo tatizo.

Happy Birthday Brother Mugisha


Haya Kaka. Ni mwaka mwingine katika maisha yako unaomalizika na kuanza mpya. Wakati unakamilisha "mwaka wa zamani" na kuanza "mwaka mpya", nakuombea kila lililo jema katika kufanikisha yale yote mema uliyopanga kufanya kwa mwaka huu uuanzao, na pia kukamilisha yale yote mema ambayo kwa namna moja ama nyingine hukuweza kukamilisha ndani ya mwaka uliopita.

Salamu za Baraka na Upendo toka kwetu sote na Kila la kheri kwako

Happy Birthday Brother Mugisha Bandio

Wednesday, October 22, 2008

Remembering Maestro Ndala Kasheba


Kama kuna wasanii waliojijengea heshima kwa kutunga, kuimba na kucharaza vema ala za muziki, basi miongoni mwao ni Ndala Kasheba. Mtunzi na mwanamuziki huyu mahiri aliyepewa jina la Maestro kutokana na kazi zake alikuwa msanii mwenye uwezo mkubwa sana wa kutunga nyimbo zenye kugusa matukio halisi yaikumbayo jamii ha hata wakati mwingine yaliyomkuta yeye binafsi.
Tunakumbuka nyimbo kama Kesi ya Khanga na hata Yellow Card ambazo sio tu zilipata umaarufu kwa umahiri wa mpangilio wa muziki, lakini pia aliezea mikasa halisi ya maisha jambo ambalo linaendelea kuwa funzo kwa wengi.
Kasheba ni kati ya wakongwe wachache waliotutoka miaka kadhaa, na leo tunapotimiza miaka minne tangu atangulie tuelekeako, bado tunajiuliza nani wajao kuendeleza kazi za wakongwe mahiri kama hawa. Sanaa ya muziki inazidi kupungua umuhimu wa uwakilishaji wa jamii kama ilivyokuwa enzi za kina Kasheba na wasanii wanajali zaidi hisia binafsi na kurandanisha majina badala ya kufumbua mengi yahitajiwayo kufanya hivyo huko vijijini na sehemu nyingine.
Ulitenda kazi yako Vema Ndala, na leo tunapotimiza miaka minne tangu ututoke, tunakumbuka na kuheshimu kazi zako na tunaendelea sio tu kufurahia kazizo, bali kujifunza yale yaliyoimbwa katika nyimbo zako.

Pumzika kwa Amani NDALA MAESTRO KASHEBA

Tuesday, October 21, 2008

Sherehe za Kazi na Maisha ya Mwl J. K. Nyerere ktk picha

Wimbo wa Taifa ukiimbwa
Rene Henry akiimba wimbo wa Black National Anthem
Wageni wakishangilia baada ya nyimbo kuimbwa
Baba Rick Tingling toka Nyerere Health and Education Fund akikaribisha wageni na kuelezea juu ya mfuko huo
Julius Nyerere III akieleza maisha na mahusiano yake na Babuye
Mgeni wa Heshima Balozi wa Tanzania USA Mhe Balozi Ombeni Sefue akitoa neno kuu Baadhi ya wanafamilia wa Hayati Mwl Nyerere waliosaidia kufanikisha siku hiyo.

Balozi Sifue akikata keki akishuhudiwa na mwanafamilia wa Nyerere


Baadhi ya wageni walikwa

"Alichopokea Mwl Nyerere toka kwa wakoloni haikuwa "nchi"" Balozi Ombeni Sefue


WaTanzania wameaswa kuendeleza umoja na mshikamano aliouanzisha Hayati Baba wa Taifa mwl J.K Nyerere kama njia mojawapo ya kumuenzi.
Rai hiyo ilitolewa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Ombeni Sefue wakati wa maadhimisho ya Kazi na Maisha ya Mwalimu Julius K Nyerere yaliyofanyika jioni ya Jumamosi ya tarehe 18 huko Washington DC.
Katika hotuba yake aliyoitoa kama mgeni rasmi, Balozi Sefue alisema wakati Mwalimu Nyerere anapokea nchi kwa wakoloni, ilikuwa ni milki yenye watu wenye makabila mbalimbali na ambao hawakuwa na namna moja ya kuwaunganisha na kuwafanya kuwa taifa, hivyo moja kati ya kazi zake za mwanzo ilikuwa kuiweka jamii pamoja, kuwa na namna moja ya mawasiliano na kisha kuvunja mipaka ya kikabila miongoni mwa wanajamii.
Amesema pia Mwalimu alianza kuwekeza katika elimu kwani wakati akikabidhiwa nchi alikuwa na wasomi wachache saana kiasi cha kumpa wakati mgumu katika hatua za mwanzo za kiutawala.
Balozi Sefue amesema mtazamo wa mwalimu kwamba "kuongea na wananchi kwa kutumia mkalimani hakunitofautishi na wakoloni, zaidi ya rangi" kulimpa changamoto ya kusambaza Kiswahili kama njia kuu ya mawasiliano na kujenga umoja na mshikamano ambao tunajivunia mpaka leo.
Siku hiyo ambayo iliandaliwa na The Nyerere Health & Education Fund ilihusisha Historia ya mwalimu, Harakati zake, mahusiano binafsi yaliyoelezwa na wajukuu wake, maelezo toka wawakilishi wa The Diaspora African Forum, Venezuela Solidarity Network na wageni wengine.

"If you can't go back, look back and make sure you stay connected to the Motherland" Ms Holland

Ms Mazie Green Holland akizungumza katika siku ya Maisha na Kazi za Mwl Nyerere

WaTanzania, waAfrika na wote wenye asili ya Afrika wamekumbushwa kutosahau walikotoka na kisha kufanya kila wawezalo kusaidia jamii ya "nyumbani" mahali popote walipo.
Rai hiyo imetolewa na Bi Mazie Green Holla kutoka The Diaspora African Forum wakati akitoa neno kwenye siku ya kukumbuka na kusherehekeha maisha na kazi za Mwalimu J. K. Nyerere iliyofanyika jioni ya Jumamosi ya tarehe 18 Oktoba kwenye ukumbi wa Kanisa la Mosaic lililopo 16th Street, NW jijini Washington DC.
Bi Mazie amesema japo si wote wenye kujua sehemu halisi iliko asili yao, lakini kwa pamoja weusi wengi twatambua kuwa tumetoka Afrika na ni wajibu wa kila mmoja wetu kuungana na kulisaidia bara hilo. Amesema kwa wale wasioweza kurejea barani Afrika kwa kutotambua chimbuko lao halisi, bado wanaweza kurejesha fikra zao nyuma na kutafuta namna njema ya kuunganishwa na Bara lao.
Akizungumzia kuhusu muunganisho wa waAfrika kupitia Diaspora hiyo yenye makao makuu yake nchini Ghana, Bi Hollad amesema imeweza kuwakusanya na kuwashirikisha waAfrika wengi waishio nje ya Bara lao kusaidia kukamilisha malengo na madhumuni makubwa ya Diaspora hii ya Afrika.
Kati ya madhumuni makuu ya The Diaspora African Forum ni kusaidia kuondoa kiwango cha umaskini katika nchi za Afrika zinazotegemea misaada ya nje kuendesha bajeti zao jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine imeziweka nchi hizo katika hali iliyopo.
Pia amesema Diasporas wanasaidia kunyanyua hali ya maisha ya waAfrika wenzao kupitia uboreshaji wa miundombinu, uwezeshwaji wa kijamii, chakula, makani na mambo mengi mengi.
Forum hiyo pia ni kati ya makundi yenye uwezo mkubwa kiuchumi ambayo yanasaidia kuboresha uchumi wa nchi zenye uhitaji.
Waweza kusoma mengi juu ya The Diaspora African Forum kwa kubofya http://www.diasporaafricanforum.org/home.htm


Ni CHANGAMOTO YETU sote DIASPORAS kuwa msaada wa namna yoyote katika kufanikisha nia njema za kuisaidia Afrika na waAfrika kwa ujumla.


DIASPORA: any population sharing common ethnic identity who were either forced to leave or voluntarily left their settled territory, and became residents in areas often far removed from the former. It is converse to the nomadic lifestyle

Saturday, October 18, 2008

Remembering Philips Lucky Dube.


Lucky katika onesho lake la Aug 25, 2007 Crossroads Entertainment Complex Bladensburg MD
Lucky na Back Up singers tar 25 Aug 2007 Crossroads Complex

Nilipomaliza kuangalia show yake usiku wa tarehe 25 Agosti 2007, niliwaeleza rafiki zangu kuwa sitakosa show ya Lucky Dube bila sababu ya msingi. Sababu ya kusema hivyo ni namna nilivyojivunia na kuvutiwa na onesho zima la Lucky. Kuanzia matumizi ya muda, ala, jukwaa (akiwa pamoja na back up singers wake) na hata uvaaji wao na namna alivyoiimbisha hadhira na kuifanya kuwa kitu kimoja japo ulikuwa ni mchanganyiko wa watu wa asili na imani tofauti.
Lakini wiki 7 baadae nikiwa bado nina kumbukumbu ya show ile nikapata habari za kuuawa kwake. Ilikuwa ngumu kuamini lakini ulikuwa ukweli kuwa mtu aliyetumia muda wake mwingi kupigania haki na usawa na upendo miongoni mwa jamii na kukemea maovu kama uporaji na mauaji, anajikuta akiwa mhanga wa yale aliyojaribu kuisaidia jamii kuondokana nayo.
Lucky alikuwa ASKARI anayepigania haki za kinamama na watoto, akipinga ubaguzi na ukandamizaji, akisimamia imani, kuelimisha kuhusu mfumo wa maisha upumbazao wengi, kutetea misingi ya muziki wa Reggae, Mapenzi, kuburudisha kwa hadithi za kusadikika ambazo ukweli wake upo katika jamii zetu na pia alikuwa mume kwa Zanele na baba kwa watoto wake 7. Ukisikiliza nyimbo zake nyingi, Lucky alikuwa ni msanii anayeelezea hadithi halisi tangu mwanzo wa nyimbo na unapomaliza kusikiliza wimbo unatambua alichokuwa akikisisitiza ama kukanya, ama kuelimisha. Ukisikiliza PRISON anaanza kwa kusema "somebody told me about this when i was still a little boy. He said to me crime does not pay, education is the key. As a little boy i thought i know what i was doing. But today here i am. I'm a Prisoner". Sikiliza wimbo wake wowote utaweza kuona mpangilio wa mashairi katika kueleza atakacho na hicho kilimtofautisha saana na wasanii wengine.
Sikiliza pia uhusiano wa midundo na ujumbe katika nyimbo zake utatambua kuwa alikuwa na uwezo wa kuiweka hadhira katika utayari wa kupokea ujumbe kwa mirindimo iendanayo na ujumbe katika wimbo
Lucky Dube katika miaka 25 aliyoshiriki katika sanaa hii ya muziki aliweza kutoa jumla ya albamu 23 ambazo 6 kati yazo alitoa katika mahadhi ya Mbaqanga, 1 katika mahadhi ya Afrikaans na 16 katika mahadhi ya Reggae. Ni mahadhi ya Reggae yaliyompa nafasi ya kutambulika, kuheshimika na kuelimisha jamii kwa upana wake ambako katika albamu hizo ameimba kuhusu mambo mengi yanayoathiri maisha yetu ya kila siku miongoni mwao ikiwa ni pamoja na Haki za wanawake na watoto (Hold On, Little Heros, God Bless the women), Mahusiano na Mapenzi (Romeo, Never Leave You, I've got you babe, Big Boys Dont cry, Lovers in a dangerous time, How will i know, Release Me) , Siasa (Political Games, Monster, Is This Freedom, Guns and Roses, The Way It Is, Together as one,) Maisha ya kufikirika (My World, Divorce Party,), Ubaguzi (Together as One, Trinity), Maovu (Crime and Corruptions, War and Crime, Crazy World, mfumo wa maisha upumbazao watu (Other side, Shut Up, Affirmative action, Love Me the way i am), ya kale na ya sasa (Changing world, Money Money), Imani (Take it to Jah, Shembe, Rastas,) na hata muziki ( Reggae is strong, Back to my roots, We Love It, Seriouss Reggae Bussiness).
Lucky Dube aliuawa na watu wanaodhaniwa kutaka kupora gari lake mbele ya nyumba ya nduguye alipotoka kuwapeleka wanawe usiku wa tarehe 18 Oktoba 2007. Ni kama alivyoimba katika wimbo wake wa CRIME AND CORRUPTON kuwa "do you ever worry about leaving and coming back in a coffin, with bullets in your head" ndivyo haswa ilivyokuwa hatima ya maisha yake. Kama alivyoimba katika Reggae Is Strong kuwa "Nobody can stop reggae" ndivyo kazi zake zinavyoendelea kuielimisha jamii kila kuikicha licha ya maisha yake kusimamishwa.
Kazi zake zitaendela kuburudisha, kuelimisha na kuikomboa jamii kutoka utumwa wa kiakili bila kikomo.

REST IN PEACE LUCKY

Friday, October 17, 2008

Them, I & Them. LUCKY DUBE .........Crime And Corruption


"Do you ever worryAbout leaving home and Coming back in a coffin, With a bullet through your head. So join us and fight this Crime and Corruption"
Hayo ni maneno ambayo ni kama yalitabiri mauti yake mwenyewe miaka 8 kabla hayajamkuta. Ni kutoka katika wimbo wa Crime and Corruption uliko kwenye albamu ya The Way It Is na ambacho pengine ndicho kilichotokea kuwa maarufu na kutiliwa umakini na walimwengu wengi mara baada ya kifo chake. Sababu kuwa ni namna alivyoeleza matukio yanayomsikitisha na kuendelea kufumbiwa macho na viongozi jamiini mwake. Lucky amewalilia viongozi kuacha kupuuzia hali halisi ya Rushwa na Maovu katika jamii yake na kukutana na wahanga wa matatizo hayo jambo ambalo aliamini labda lingefungua mioyo ya viongozi na kuendeleza kampeni za kupinga mambo hayo. Ukiusikiliza kwa makini, Lucky alianza na swali kwa "waheshimiwa" akitaka kujua sababu hasa inayowafanya wasione ukweli juu ya wakulima na askari wanaouawa kila siku huku wao (viongozi) wakitoa ripoti kuwa hali si mbaya na anawauliza " Is it the bodyguards around you,Is it the high walls where you live,Or is it the men with the guns around you twenty four hours a day;That make you ignore the crying of the people..."
Ni ukweli ambao aliuimba na kwa bahati mbaya saana ndiyo yaliyomkuta miaka minane baadae pale alipouawa katika aina ya uovu ambao si mgeni na umekuwa ukikemewa saana nchini Afrika Kusini. Aliimba katika kibao hiki juu ya wizi wa magari uliokithiri ambao wakati mwingine unafanyika mchana kweupe tena kwenye barabara kubwa kama Highway 54. Hiyo ni hali halisi ambayo hata baadhi (wengi) ya watu walioihama Afrika kusini wanasema wamekimbia maovu kama hayo na hata Kampuni ka bima ya Hollard Insurance iliamua kutowekea bima magari ya Volkswagen Citi Golf kutokana na kuibiwa sana nchini humo (bofya http://en.wikipedia.org/wiki/Crime_in_South_Africa). Lakini kama askari halisi wa Reggae na ambaye alikuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge, Lucky Dube aliweza kuimba haya na mengine mengi katika Albamu yake hii ya The Way It Is ambayo viongozi wengi waliamua na bado wapo wanaofumbia macho huku uovu huu ukiendelea kuziathiri jamii zetu barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

RUSHWA na MAOVU ni kati ya mambo aliyoyapigania saana Lucky Dube, na leo ikiwa ni siku moja pungufu ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu auawe, CHANGAMOTO YETU ni kuangalia namna ambavyo mengi mema yaliyoimbwa naye yanatafutiwa ufumbuzi katika jamii zetu. Video ya sehemu ya mazishi yake na heshima kwa Lucky ni hii hapa chini
Blessings
**Them, I & Them ni kipengele kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**

Thursday, October 16, 2008

Exclusive Bongo Mix from Dona Productions

"Its Oct and time to roll out the Sep/Oct Podcast that I did forAfrican Hip Hop Radio Bongo Flava edition. Make sure to check out theintro which features Dead Prez. Shouts out to Juma and all the Africanhip hop radio crew. We will be showcasing the Bongo Flava Podcast onAfrican Hip Hop Radio every month. Make sure to check out the introwhich features Dead Prez."

Download Link: http://www.zshare.net/audio/18219980db4a4c2f/

Tracklisting:

African Hip Hop Intro
MwanaFA - Bado Nipo Nipo
Wanaume TMK - Dar Mpaka Moro
Prof. Jay - Nang'atuka
MB Dog Feat. Madee - Latifa
Cloud Tissa Feat G-Solo - All Over
Inspector Harun - Shetani Hana Mwaka
Top Band Feat. Matonya - Beki Hazikabi
Queen Darleen Feat Ali Kiba- Najua Nakupenda
Joe Makini-Sitachoka
Ali Kiba - Zuu
AY - Usijaribu
Zanto Feat. Tilly One - Mpenzi Jini
Ay Feat Q Chillah - Binamu
MB Dogg - Naona Raha
Chidi Benz Feat K-Lynn - Naitwa Nani
Jay Moe- Maisha Ya Boarding
TID and MwanaFA- Raisa
MH. Temba - Mwaka Wa Shetani
Mez B - Kikuku
Noorah, Mwanafalsafa Feat Enika - Zai
Q Chillah feat Nyota Ndogo - Wivu
Professor Jay feat Jay Mo - Hapo Sawa (Remix)
Dataz and Squeezer - Wajua
Hafsa Feat Banana - Presha
Marlaw na Chidi Benz - Bado Nimenuna
Ali Kiba - Msela

Tuesday, October 14, 2008

Happy Birthday Brother Lusajo Anangisye

Ni mwaka mwingine kamili maishani mwako na naamini utaanza kwa mipango yenye mafanikio kuliko mwaka mwingine wowote uliopata kuwa nao. Mafanikio ni pamoja na kujivunia ushindi katika mengi yatukabiliayo na kujivunia huja baada ya mapambano, hivyo naamini utaendelea kupambana na maisha na sina shaka kuwa utayamudu kisha kujivunia huku ukitoa Sifa na Shukrani kwa mwezeshaji mkuu.
Kila la kheri katika kila jema utendalo na upangalo kutenda.
Happy Birthday Brother Sajo

Monday, October 13, 2008

Columbus Day??

Christopher Columbus

Ndio. Ni siku ya mapumziko nchini Marekani (na baadhi ya nchi nyingine ulimwenguni) wakisherehekea siku hiyo waiitayo Columbus Day inayokumbuka kuwasili kwa Christopher Columbus katika Americas mnamo Okt 12 1492.
Wana-Historia wanatambu ni nini kilifuata baada ya kugundulika kwa New World na matokeo yake kwa ulimwengu ni yapi. Na naamini madhara yake yakingalipo mpaka leo katika baadhi ya sehemu kama Afrika.
Ni nini hasa cha kusherehekea katika siku kama hii? Siku ambayo bado kuna upinzani wa umuhimu wa kuisherehekea kutokana na mateso waliyopata wazawa na watumwa ambayo kwa namna moja ama nyingine yalitokana na ujio wa huyo mheshimiwa? Soma http://en.wikipedia.org/wiki/Columbus_Day#Opposition_to_Columbus_Day na pia http://www.google.com/imgres?imgurl=http://carolynbaker.net/site/images/columbus.gif&imgrefurl=http://carolynbaker.net/site/content/view/156/&h=500&w=364&sz=186&tbnid=1NiozdmLUwIJ::&tbnh=130&tbnw=95&prev=/images%3Fq%3DChristopher%2BColumbus%2BPhotos&usg=__ccGCLdyIG9n2FAVeR0bPJQWcPSk=&sa=X&oi=image_result&resnum=1&ct=image&cd=1 uone mwenyewe.
Kwa msherehekeao, basi sherehe njema na wengine, siku kama kawaida.
Msikilize Burning Spear akimnanga Christopher Columbus hapa chini

I an' I all I know
I an' I all I say
I an' I reconsider
I an' I see upfully that:

Cristopher Columbus is a damn blasted liar
Cristopher Columbus is a damn blasted liar, yes Jah

He say 'im that he's the first one
Who discover Jamaica, I an' I say that:
What about the Awarak indians ?
And the few black man who were down here before him ?
The indians could'n hang on a long long
Here comes black man an'oman an' children
A ina Jam Dung run ya
Whole heap a mix up, mix up
Whole heap a ben up, ben up
Ha fi straighten out

Cristopher Columbus is a damn blasted liar
Cristopher Columbus is a damn blasted liar, yes Jah

What a long stay from home
I an' I longing to go home
Within a red, green an' gold robe
Come on, twelve tribe of Israel
Come on, twelve tribe of Israel
A outa Jam Dung land ya
A whole heap a mix up, mix up
A whole heap a ben up, ben up
Come on, twelve tribe of Israel
Come on, twelve tribe of Israel
A outa Jam Dung land ya, yes Jah

Cristopher Columbus is a damn blasted liar
Cristopher Columbus is a damn blasted liar, yes Jah
He's a liar, yes Jah
He's a liar, yes Jah
Columbus he's a liar, yes Jah

Sunday, October 12, 2008

Wasanii kama "chombo cha starehe" cha serikali

Mawaziri wakuu Mhe Pinda (TZ) na Mhe Odinga (KEN) wakifurahia ngoma
Mfalme Mswati na Rais Kikwete wakiburudika na mganda


Mwalimu wangu wa Fasihi alipokuwa akinifundisha maudhui katika uchambuzi wa vitabu alizungumzia uchambuzi wa namna waandishi walivyoonesha na ama kukemea tabia za wanaume kwenye tamthilia hizo kuwatumia "wanawake kama chombo cha starehe". Na katika fafanuzi zake akasema pale unaposoma na pakaonesha kuwa mwanaume amemtumia mwanamke kutimiza matakwa yake (hata kama ni kwa ujira mdogo) basi anakuwa amemtumia mwanamke kama chombo cha starehe.
Nikiweka hayo katika MAISHA ambayo kati ya wahusika ni Serikali na wasanii, naona kile alichonieleza mwalimu wangu kikitendwa na serikali badala ya wamanume kwa wasanii badala ya wanawake.
Yaani naona namna serikali inavyowatumia wasanii katika kukamilisha adhma zao huku wakiwapa nafasi ndogo katika kuondoa kero zao za kazi inayowaweka wao na wategemezi wao ulimwenguni. Namaanisha serikali kutotatua matatizo iliyo na uwezo wa kuyatatua ambayo wasanii wamekuwa wakilalamikia kwa muda mrefu na ambayo kutatuliwa kwake kutaboresha maisha ya wasanii na wategemezi wao.
Tumeona wasanii mbalimbali wakitumika katika Kampeni mbalimbali za kisiasa. Ni katika kampeni hizo ambapo wasanii hutumika kuhamasiaha kusanyiko la kumsikiiza mgombea na hata kuburudisha hadhira na kwa wakati huo huo kumuwezesha mgombea kunadi sera zake.
Tumeona pia wasanii tangu kale wakitumika katika Propaganda mbalimbali (kama Gezaulole n.k) na kwa kutumia nyimbo basi ni jamii kubwa hufikiwa na ujumbe ambao usingeweza kuifikia kama kiongozi angetoa hotuba za redioni ama jukwaani
Ni wasanii haohao (tena wengi wao wa sanaa za ngoma za asili ambao ndio wana kipato kidogo kisanii) tunaowaona kila kukicha kwenye Tovuti na Majarida Tando pamoja na kuwasikia kwenye vyombo vingine vya habari wakifanya kazi njema ya kuselebuka Uwanja wa ndege kila wanapoalikwa kwenye mapokezi ya viongozi wakuu wa nchi mbalimbali.
Pengine kubwa na lenye kuonesha "kuthamini burudani" ya wasanii wa nyumbani ni pale wanapoalikwa kwenda kuwatumbuiza waheshimiwa wabunge ambao kwa miaka nenda rudi wameshindwa kuweka sheria ambazo zingelinda haki na mapato yao.
Najua Waheshimiwa wabunge na wenye mamlaka wana-enjoy saana sanaa ioneshwayo na wasanii wetu, lakini kama wanaishia kuwalipa pesa ya onesho (kama hayo ya bungeni) ama kuwapigia makofi na pesa ya onesho la airport, ama kama ni suala la mkataba wa kupiga kampeni na ama propaganda za wasanii, basi napenda watambue kuwa "kwa mujibu wa tafsiri niliyopewa na mwalimu wangu ninayemuamini, nao wanawatumia wasanii kama chombo cha starehe".
Hivi si wakati wa kuweka sheria kali kwa wale wanaosambaza kazi za wasanii? Si wakati wa kupitia vyema hakimiliki na unyonyaji ufanywao kwa wasanii na watu wachache kujinufaisha kwa jasho la wasanii? Ni kweli kuwa viongozi serikalini hawayaoni haya ama hayana "sound" ya kisiasa? Nachukia kila ninapoona "politrix" inaingilia uhalisia wa maisha na kuweka pembeni suluhisho linaloweza kumnyanyua msanii, familia na taifa kwa ujumla.
Lakini pia lawama hizi ama haya yote yatokeayo yana mkono wa wasanii wenyewe. Kutokuwa na umoja miongoni mwao, kuendekeza njaa na majungu baina ya baadhi yao na kutokuwa na elimu na utawala wa KAZI YA SANAA kunawafanya wagawanywe na kutumika bila wao kujijua. Kutokuwa na hesabu kamili na halisi za namna ya kugharimisha muda na kazi zao kulingana na hali ya maisha ya sasa ukizingatia kuwa ndio kazi yao wategemeayo kwa maisha ya sasa na uwekezaji wa maisha yajayo.
Kama alivyosema Bob Marley kuwa "emancipate yourselves from mental slavery, non but ourselves can free our minds" nami naamini ni wasanii wenyewe wanaoweza kuungana na kuanzisha mjadala mwema wa kufuatilia malipo ya kazi na kutotumika kwa ujira mdogo.

Ni changamoto tuu

Friday, October 10, 2008

Them, I & Them. MORGAN HERITAGE ........ Don't Haffi Dread

Nikiwa na Jah Petes wa Morgan Heritage
Morgan Heritage toka kushoto Lukes, Peter, Gramps, Una na Mr Mojo

Nilipofanya mahojiano na Ras Innocent Nganyagwa mwaka 2003 kuhusu hali ya Reggae nchini Tanzania, alizungumza sentensi ambayo niliitumia saana katika kipindi cha Reggae chake Seif "Dj Fax" Selemani aliyekuwa Times FM. Alisema "kuna kutoeleweka kwa suala la Rasta. Kuna watu wenye locks (Rasta) ambao hawana imani ya urasta na wapo marasta ambao hawana locks". Huo ni msemo ambao si Ras Inno tu aliyefafanua ukweli huu kwa kina, bali kundi maarufu na mahiri katika muziki wa Reggae ulimwenguni la Morgan Heritage lilifafanua hili kwa kutunga wimbo wenye ujumbe huo na kuipa albamu yao jina la wimbo huo; DON'T HAFFI DREAD.

Morgan Heritage inayoundwa na ndugu watano (Peter, Gramps, Mr Mojo, Luke na Dada yao Una) walitoa albamu yao hiyo mwaka 1999 ambayo katika kibao chao wanasema "you don't have to dread to be rasta. This is not the dreadlocks thing, it's divine conception of the heart". Katika jamii zetu kumekuwa na mkanganyiko wa uelewa wa nani ni Rasta na nani ana dreads na nini athari na ama faida za kuwa na dreads. Ni uelewa huu ambao kama ilivyo kwa mengi umekanganywa na IMANI na TAMADUNI zetu na kufanya baadhi ya mambo yaliyo ama yanayostahili kuwa ya "kiuchaguzi" kuwekwa katika kundi la DHAMBI, UHUNI na mengine mengi ambayo kwa hakika hayana ukweli ndani yake.

Tumeona "mtindo" wa wasanii wengi wa Bongo Flava kutengeneza dreads kwa misingi iliyoonekana kama ya kibiashara zaidi japo wengi wao hawana imani na wengine hata hawatambui imani hizo, lakini walisokota.

Kama alivyosema Jah Peter kwenye onesho lao la San Francisco, kuna wengi wenye Rasta wasiojua lolote kuhusu imani yake ambao "wanavaa" kwa utashi na kuna wengi walio ma-rasta halisi wasio na dreads. Kubwa ni kujua njia na maisha uishiyo na namna unavyotaka kuendesha maisha pasina kujitumbukiza katika maisha ya wengine na kuharibu mtazamo wao kwa tabia zisizoendana na pale ulipojiingiza.

Ni CHANGAMOTO YETU sote kujua maisha tuishiyo na kutambua kuheshimu kila mfumo mwema wa maisha na kuuthamini kama ambavyo mifumo yetu imekuwa ikithaminiwa na kuheshimiwa.

Remember, You don't haffi dread to be Rasta. Kujua mengi juu ya hii Royal Family of Reggae bofya www.morganheritagemusic.com.

INTRO
Yeah, yeah, yeah - ragga so ragga

CHORUS
You don't haffi dread to be rasta (don't ha fi dread)
This is not a dreadlocks thing
Divine conception of the heart, well
(repeat)

VERSE 1
Oh, it's a life of a livity
Lived by the fathers of our history
Uphold the anciency and prophecy
Trust in the power of the Trinity, yeah
Got to believe in His Majesty
Oh yes, his lineage an divinity
The first step is serenity
Knowing one self's true royalty, yeah

CHORUS
You don't haffi dread to be rasta, yeah
(don't ha fi dread)
This is not a dreadlocks thing
Divine conception of the heart, well
(repeat)

BRIDGE
Don't be afraid of Jah ever burning fire
Trust in Jah fire and you never get burn
The fire that reigns over heat, air and water
No water can put out Jah fire
Jah fire gonna lift Rasta higher

CHORUS
You don't ha fi dread to be rasta, yeah
(don't ha fi dread)
This is not a dreadlocks thing
Divine conception of the heart, well
(repeat)


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.

IJUMAA NJEMA

Wednesday, October 8, 2008

Filamu ya Richmond yaja: Naanza kuhisi vitakavyonikera

Denis Sweya (Dino) kushoto na Deo wa Dollwood
Picha toka www.fullshangwe.blogspot.com

Katika gazeti tando la Kaka Bukuku la Full Shangwe, kuna habari juu ya makamilisho ya filamu ya Richmond ambayo kwa mujibu wa Mtunzi wa filamu hiyo na muigizaji wa filamu Dennis Sweya (Dino), itazungumzia masuala ya unyanyasaji, dhuluma na rushwa iliyokithiri. Bofya http://fullshangwe.blogspot.com/
Ni kwa mujibu wa Dino huyohuyo, kuwa filamu hiyo itakayozinduliwa mwezi ujao imepigwa picha zake katika mikoa ya Arusha na Dar-Es Salaam. Hapa napenda kumpongeza msanii Dino kwa hatua aliyofikia ya kuweza kuandika filamu, kuitafutia washiriki ama waigizaji, kampuni ya kupiga picha hizo, uhariri na maandalizi yote yanayotakiwa mpaka kuja kuiingiza sokoni. Ni hatua moja mbele kuelekea mafanikio ya kisanii, lakini kuna mambo ambayo nahisi yataniketa katika filamu hii.
1: Najaribu kuoanisha maudhui yaliyotajwa na jina la filamu hiyo kuona kama itakuwa ikimtetea na kubainisha matatizo yamkumbayo mTanzania halisi ama itakuwa ni katika kutafuta jina litakaloweza kuuza kulingana na kashfa iliyokuwa na ambayo inafifia katika taifa letu. Hili naliona kama "kukurupuka" kwa kuwa siamini kama mtu anayetaka kuzungumzia unyanyasaji, dhuluma na rushwa iliyokithiri nchini Tanzania atatumia jina hilo. Kama hakutakuwa na ufafanuzi wa haja wa namna lilivyotumika Richmond kueleza unyanyaswaji, dhuluma na rushwa iliyokithiri katika nchi ambayo sidhani kama kuna mtaa wenye jina hilo, basi hii filamu itanikera
2:
Kama kuna kitu kinachoitwa unyanyasaji, dhuluma na rushwa iliyokithiri, basi kunahitaji uchunguzi na ufuatiliaji uliotukuka kuweza kuweka yote baya. Tukumbuke kuwa Filamu ni sehemu ya kuonesha matatizo na pia suluhisho kwa jamii inayohusika. Kama filamu hii haitaeleza matatizo yaliyochunguzwa na kuonesha namna ya kutatua basi itanikera.
3: Nilishaandika juu ya uvivu wa wasanii katika kutumia sanaa ambayo sio tu wanaimudu, lakini pia wamepata nafasi ya kuweza kuitumia kuiwakilisha jamii. Lakini wanaendelea kung'ang'ania maeneo ambayo kila mmoja anatambua mazuri na mabaya yake. Naamini wapo (na namaanisha wengi) wanaofahamu unyanyasaji, dhuluma na rushwa zilizopo Arusha na Dar kuliko zitakazooneshwa katika filamu hiyo. Kuna wengi walio vijijini (kuanzia Nanjilinji mpaka Rubafu) ambao wanadhulumiwa, kunyanyaswa na kutopata huduma zozote bila kutoa rushwa. Kama filamu hii haitagusa matatizo waliyonayo kinamama vijijini ambapo wanapoteza maisha kwa kukosa pesa ya kutoa rushwa, wanapigwa bila ya kuwa na mtetezi na wanakodhulumiwa pamoja na watoto wao na pia watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali, filamu hii itanikera.
Huu ni mtazamo wangu na changamoto kwa wote wajiandaao kutengeneza filamu kuonesha matatizo ya waTanzania. Msipoenda vijijini ambako ndipo yalipo mtakuwa mnaonesha tunachokifahamu na itaonesha kuwa mnasaka pesa kuliko kujitahidi kutatua yale mnayoeleza kuwa ndio nia yenu kuu.

Kama jina la blog lilivyo (NAMNA UONAVYO TATIZO NDILO TATIZO) yawezekana nionavyo mimi ndilo tatizo japo naamini tatizo ni namna uonavyo nionavyo.
Blessings
See you "next Ijayo"

Happy Birthday Brother Fortunatus Mugisha

Ni siku nyingine inayokamilisha mwaka kamili wa maisha yako Kaka. Nakutakia kila la kheri katika kila jema upangalo na utendalo na naamini kwa imani, juhudi na maarifa uliyonayo utaweza kufanikiwa katika kila jema utendalo.
Happy Birthday Brother Fortunatus

Monday, October 6, 2008

Inapotafutwa maana mpya ya kifo kukidhi mahitaji ya afya


Madaktari wanatafuta maana mpya ya kifo ama hali ya mtu kutambulika kuwa amekufa itakayowawezesha kusaidia kuokoa maisha mengi kutokana na kutumia baadhi ya viungo muhimu vya "marehemu" hao kabla "havijafa" na kuvipandikiza kwa wagonjwa wenye uhitaji. Jarida la mambo ya afya la New England Journal of Medicine limeeleza namna ambavyo madaktari waliweza kuhamisha moyo wa mtoto ndani ya sekunde 75 tangu athibitishwe kufa kwa maradhi ya moyo.
Je! Kuna uvunjaji wowote wa misingi ya kibinadamu katika hili? Yawezekana kuna ukweli lakini (na hapa naomba kunukuu ili kuweka ujumbe halisi) "......in medicine, lines move. "Dead" means irreversibly stopped, and stoppages are increasingly reversible. And when life support ends, says one bioethicist, "not using viable organs wastes precious life-saving resources" and "costs the lives of other babies." Failure to take body parts looks like lethal negligence". Whaooooooooooooooooooooo!!!!!
Bado hawajamaliza, swali jingine ni vipi tunaweza kupata viungo muhimu vya mwilini punde baada ya mgonjwa kufariki ili kuweza kuokoa maisha ya wengine wengi? (na kwa mara nyingine naomba nisipoteze maana kwa kutafsiri) wao (wataalamu wa kupandikiza viungo) wanasema "..... By redefining death. First we coined "brain death," which let us take organs from people on ventilators. Then we proposed organ retrieval even if non-conscious brain functions persisted. Now we have "donation after cardiac death," the rule applied in Denver, which permits harvesting based on heart, rather than brain, stoppage.
But stoppage is complicated. There's no "moment" of death. Some transplant surgeons wait five minutes after the last heartbeat; others wait two. The Denver team waited 75 seconds, reasoning that no heart is known to have self-restarted after 60 seconds. Why push the envelope? Because every second counts. Mark Boucek, the doctor who led the Denver team, says that waiting even 75 seconds makes organs less useful."

Bofya http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2008/10/03/AR2008100301974.html uone sayansi inakotupeleka. Kama kiungo kinatolewa ndani ya sekunde 75, si ina maana hawa wataalam wanakuwa wamekutolea macho ukate roho wachukue kiungo chao waelekee nyumbani? Ama wanajuaje dakika utakayokufa ili wawahi kutoa kiungo kabla "hakijafa"?

Sijui inaleta CHANGAMOTO gani kwa Wanasayansi vs Imani vs Tamaduni.

Sunday, October 5, 2008

Mahsusi kwa "walevi wa taswira"

Haya sasa, baada ya shule kunoga kwa Kaka Michuzi, naona kaamua kutuunganisha na ka-mchepuo ketu kwa ajili ya kuwapa nafasi ya kipekee "walevi wema wa taswira. Hebu bofya www.libenekelataswira.blogspot.com uone mambo yalivyo huko.
Ni mahususi kwa akina sie tuuuu.
Blessings Michu

Milo 7 isaidiayo kurefusha maisha.


Kwa miaka nenda rudi, wanasayansi wamekuwa wakizunguka dunia kutafuta jamii ambazo zimesemekana kuwa na maisha marefu na yenye afya njema ili kuweza kufichua siri ziwafanyazo waishi maisha muda mrefu namna hiyo. Katika miongo michache iliyopita wameweza kupata machache yenye kutia moyo juu ya hilo. Kwa mujibu wa jarida la Eating Well, wachunguzi wanasema kutumia Olive Oil kumewasaidia Wagiriki kupambana na maradhi ya moyo wakati vyakula vyenye kiasi kikubwa cha samaki kimesaidia wazawa wa Alaska kupambana na matatizo ya mishipa ya moyo. Pia siri ya maisha marefu katika visiwa vya San Blas ufukweni mwa Panama imetambulika kuwa ni matumizi ya chocolate ambayo imeonekana kusaidia kuweka mishipa ya damu katika hali ya afya njema. Huko kusini mwa Japan katika kisiwa cha Okinawa ambapo wakazi wake wanaotimiza miaka 100 wanabashiriwa kuwa mara tano ya nchi zilizoendelea ( watu 50 kati ya 100,000 wana zaidi ya miaka 100 ukilinganisha na 10 walioko Marekani na nchi zilizoendelea) na siri ya kuishi kwao maisha marefu ya afya ni Viazi vitamu, matunda yajulikanayo kama Bitter Lemon na Chai ya Sanpin (ambayo ni mchanganyiko wa green tea na maua ya Jasmine) na vyote vitatu kwa pamoja vina virutubisho vinavyosaidia kuziua kulika kwa cell za mwili.
Unaweza kujua zaidi juu ya milo 7 inayoweza kusaidia kurefusha maisha kwa kubofya http://www.eatingwell.com/recipes/collections/7_foods_to_keep_young.html