Wednesday, August 28, 2013

Maadhimisho ya miaka 50 ya March in Washington

Rais Barak Obama, leo ametoa changamoto kwa kizazi kilichopo kuwaenzi mashujaa walioandamana mwaka 1963 kudai haki sawa kwa watu wa rangi zote nchini Marekani.
Mubelwa Bandio ana ripoti kamili
TUKIONI, mwanaJAMII EBOU SHATRY wa Swahilivilla Blog alihudhuria na kunasa nyota kadhaa waliohudhuria wakiwasili

Tuliobahatika kuwanasa katika kamera ya swahilivilla muigizaji Jimmy Foxx, pale alipotolewa ndani ya gari na maofisa kuanza kupekua gari alilolipanda kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial  Washington DC.

Mwigizaji wa filamu Angelha Bassett Evelyn alipotolewa kwenye gari lake na maofisa kuanza kulipekua kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial  Washington DC

Mshangao mkubwa watu walioupata ni pale mtoto wa Rais wa zamani nchini Marekani John F. Kennedy, Caroline Kennedy alipoingia na Cab (Taxi).
Cha kuchangaza pia ni pale gari lake lilipopekuliwa bila ya kujali ukubwa au cheo alichonacho na kufata sheria ya upekuzi kama wengine magari yao yalivyopekuliwa.
Caroline ni Balozi mteule wa Marekani nchini Japan

Ni Oprah Gail Winfrey pekee ambaye hajatoka kwenye gari lake ambalo lilipekuliwa na kuruhusiwa kuondoka bila ya kutolewa ndani ya gari hilo alilokua amalipanda

Mwenyewe mwenyeweeee
Chief wa swahilivilla Abou Shatry akiwa katika 50th anniversary March on Washington DC Siku ya Jumatano 28, 2013
Kwa taswira zaidi BOFYA HAPA

Tuesday, August 27, 2013

Mjadala wa rasimu ya Katiba mpya DMV

Karibu katika sehemu mbili za mjadala uliohusisha BAADHI viongozi na wanaharakati wa siasa waishio Washington DC
Katika sehemu ya kwanza, wachangiaji walikuwa viongozi wa CHADEMA tawi la Washington DC ambao wameeleza mtazamo wao na wa chama chao kuhusu rasimu hiyo.
Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Tawi Bwn. Kaley Pandukizi, Katibu wake ambaye pia ni Afisa Habari Bwn Liberatus Mwang'ombe na Mweka Hazina wa Tawi Bwn. Ludigo Mhagama
Na katika sehemu ya pili, Mwenyekiti na Katibu wa CHADEMA DMV waliungana na mwanaharakati wa chama cha CUF ambaye pia ni mmoja wa waasisi na Katibu wa Zanzibar Diaspora USA Bwn. Shamis Abdul kujadili mambo mbalimbali katika katika
Karibu uungane nasi

Mdogo mdogo......Tunakaribia. Asante kwenu

Ndio mwendo tuaminio watufaa...Mwendo usio na kasi.
Lengo ni kuhakikisha kuwa kila TUKANYAGAPO, haturejei kukanyaga (labda iwe nje ya uwezo wetu)
 Lakini pia...
Katika mwendo huu mdogomdogo, tunajifunza mambo mengi makubwa.
Nayo ni NGUVU NDOGO YA WENGI ambayo ina NGUVU kuliko NGUVU KUBWA YA WACHACHE.
Kuweza kufika hapa tulipo, imekuwa ni ushirikiano na wengi ambao wametuwezesha katika kile walichoamini kuwa ni KIDOGO kwao.
Walioona NIA na FAIDA ya kuWEKEZA katika wale waliowekeza kwa muda KATIKA JAMII.
Tumegundua kuwa kwa pamoja tunaweza kufika mbali iwapo kila mmoja atashikilia wajibu na talanta na uwezo wake katika kulileta pamoja WAZO MOJA....JAMII
Nasi sasa tunakaribia kukamilisha lengo hilo.
Tunakaribia kuwekeza zaidi katika kile tuaminicho kuwa ni muhimu zaidi kwetu...
KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KUKOMBOA FIKRA
Karibu
KARIBU KATIKA "JIKO" LA JAMII PRODUCTION.

JAMII PRODUCTION 
"USAHIHI WA FIKRA NDIO FIKRA SAHIHI"

Edibily Lunyamila akilonga na Vijimambo

Edibily Lunyamila alipokuwa akishuhudia mazoezi ya timu ya Yanga katika makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar Es Salaam. 
Photo Credits: Bin Zubeiry
Mcheza soka nyota wa zamani wa kimataifa Edibily Lunyamila, amefanya mahojiano na Dj Luke wa blog ya Vijimambo na kueleza mambo mbalimbali ikiwemo shughuli zake baada ya kustaafu soka na hata anavyolinganisha soka la "enzi" wake na sasa.
Pia kagusia changamoto ambazo wachezaji wastaafu wanakumbana nazo na maoni yake katika kukuza soccer la Tanzania
MSIKILIZE

Kijiwe cha ughaibuni

Karibu katika kipindi kingine cha KIJIWE CHA UGHAIBUNI kinachoandaliwa na Blog ya Vijimambo.
Katika kipindi hiki, wadau hujadili mambo mbalimbali yanayoikumba jamii yetu na kujaribu kuweka mtazamo wao kuhusu namna ya kukabiliana na matatizo wayajadiliyo
Leo hii, wameanza na suala la KATIBA MPYA YA TANZANIA
KARIBU UUNGANE NAO

Scolarships kutoka Help for Underserved Communities Inc. (HUC)


“Help for Underserved Communities Inc. (HUC), Inatangaza nafasi 10 za kozi za ufundi za awali zinazotolewa VETA, UDEREVA WA BODABODA/PIKIPIKI, SALUNI, UFUNDI MAGARI, UJENZI, USHONAJI NA NYINGINEZO zitakazoanza Octoba 2013.
Fomu imeambatanishwa kwenye hapa chini ama kwenye "linki" iliyowekwa hapo chini.
Ichapishe (print) kisha ijaze na uitume: (kijasti@hotmail.com au Info@myHUC.org) kabla ya tarehe 15 Septemba 2013.
Chagua moja ya kozi kama zinavyoonekana kwenye fomu ya maombi.
Tunasisitiza kuwa mwombaji awe hana uwezo kabisa wa kujilipia na tayari ameanza kujishughulisha na kazi anayotaka kuisomea. 
Pia unaweza kutuma kwa;
Help for Underserved Communities Inc, 
P. O Box 7022, 
Dar es Salaam. 

Kwa maelezo zaidi kuhusu ufadhili na HUC, ingia HAPA upakue fomu hizo (PDF)
 FOMU ZIKO HAPA CHINI
Bofya READ MORE KUZIONA

"Teaser" ya SWEET PETER JEETER THE LOVE DOKTA toka Swahili Radio

SWAHILI RADIO ni kituo cha mtandaoni kilichoanzishwa Jijini Washington DC USA na Kampuni ya "MMK MEDIA GROUP" ambao wanamiliki Swahili Radio Online, Swahili TV Online, SwahiliTV Blog, Swahili Magazine USA-AFRICA, na The Bridge Show inayoonyeshwa kwenye channel za DCTV.
Sasa wapo kwenye matangazo ya majaribio ambapo wameanza kukuletea vipindi kama vya "kutoka magazetini" na "Habari za Afrika"
Sasa wanaongeza kipindi kingine cha MAHUSIANO kitakachokuwa kikitangazwa na AJ UBAO a.k.a Sweet Peter Jeeter the Love Dokta.
AJ UBAO ama Sweet Peter Jeeter The Love Dokta
Hii ni "onjesho" la Dokta mwenyewe akikualika katika kipindi chake kitakachoanza kusikika hivi karibuni
USIKOSE KUUNGANA NAO KAMA WALIVYOELEZA HAPA CHINI


MAELEZO JINSI YA KUTUPATA KWENYE SIMU ZA MIKONONI

1. Download Tunein (Tunein ni neno moja usiache nafasi) Tunein Radio app kwa simu yako mfano; iphone, ipad,ipod,android au Blackberry

2. Baada ya ku-download , open app na nenda kwenye browser  na andika neno swahili radio kisha search.

3. Ukiona logo yao ya swahili radio bofya na sikiliza.

Monday, August 26, 2013

Mkutano wa Waziri mkuu na waTanzania...London

Urban Pulse Creative Media wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wanakuletea Ziara fupi ya Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokutana na Watanzania waishio Nchini Uingereza Agosti 2013
 

Sunday, August 25, 2013

Miaka 50 ya "March On Washington". Mahojiano Na Profesa John Innis Mtembezi

Nilipokutana na Prof John Mtembezi July 22, 2012.
Ni nusu karne sasa tangu kufanyika kwa maandamano makubwa sana ya kudai haki za watu weusi, yaliyofanyika August 28, 1963 katika jiji la Washington hapa nchini Marekani. Maandamano hayo yaliyopewa jina la MARCH ON WASHINGTON,ambayo pia yanakadiriwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya robo milioni, yanakumbukwa na wengi kwa namna nyingi, lakini yamekuwa maarufu zaidi duniani kutokana na HOTUBA iliyotolewa na mwanaharakati Martin Luther King Jr aliyoipa jina la I HAVE A DREAM.
Wiki hii, maelfu ya watu wamekusanyika jijini Washington DC, kufuata pale nyayo zilipokanyaga miaka 50 iliyopita kuelekea katika sehemu ileile yalipohitimishwa maandamano hayo.
Wengi wanaamini kuwa kuna mabadiliko yaliyotokea tangu wakati ule, lakini pia wapo wanaoamini kuwa mpaka sasa, MAPAMBANO dhidi ya ukandamizaji wa haki yapo kama ilivyokuwa wakati ule….japo yawezekana ni kwa namna tofauti kidogo
Kufahamu zaidi, Jamii Production imefanya mahojiano na Prof. John Innis Mtembezi kuhusu miaka 50 tangu kufanyika kwa maandamano hayo
Wakati huo (1963), ndio alikuwa amemaliza High School.
Ameeleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na...
Anayokumbuka kuhusu siku hiyo.
Harakati zao (WaMarekani weusi) katika kudai haki zao.
Nini hasa liliwafanya waMarekani weusi waandamane?
Nini kimebadilika?
Nini hakijabadilika?
Kuwa na Rais mweusi, Mwanasheria mkuu mweusi na hata kupata kuwa na Waziri wa Mambo ya Nje mweusi ambaye ni mwanamke ni dalili za ukombozi wa mtu mweusi Marekani?
Kisha akatoa USHAURI WAKE KWA WASIKILIZAJI WOTE POPOTE WALIPO.
KARIBU UUNGANE NASI

Thursday, August 22, 2013

MJADALA WA MAONI YA KATIBA MPYA KWA WAKAZI WA DMV


Ndugu watanzania wa Washington DC na vitongoji vyake.
Tunapenda kuwakaribisha katika mjadala wa Katiba mpya ya Tanzania utakaofanyika siku ya Jumamosi (24/8/13) kuanzia saa tisa kamili alasiri mpaka saa kumi na mbili jioni.
Mjadala huu utakaorekodiwa kwenye video utasambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari pamoja na ofisi husika.
WAHUSIKA WANAOTARAJIWA KUSHIRIKI NI:
1: Wawakilishi wa matawi ya vyama vya siasa (CCM, CUF, CHADEMA)
2: Wawakilishi wa Jumuiya na Taasisi za waTanzania 
3: Wananchi wote watakaohudhuria kuchangia na kuuliza maswali.
 Anwani ni
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740


Tafadhali....JIANDAE na Usikose kuhudhuria na kutoa mchango wako ili kufanikisha kupata katiba itakayotufaa sote.

''Bongo Views'' ya GENN Redio toka kwa waTanzania wanaoishi Kansas City

Global Entertainment and News Network (GENN) iliyopo Kansas City nchini Marekani, inatambulisha kwenu kipindi  kipya cha BONGO VIEWS kitakachokuwa kikiwajia moja kwa moja kila Jumamosi  kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya kati (12 jioni kwa Marekani ya Mashariki)
Photo
Muendesha wa kipindi cha Bongo Views Joshua Kijo Simon Madelkeka akiendelea kujadili pamoja na washiriki wake kuhusu suala la uraia wa nchi mblili na mambo mengine ndani ya Studio ya Global Entertainment and News Network (GENN)
Photo: BONGO VIEWS: ANDY MKINGA and BAVON
Wachangiaji kipindi  kushoto Mjombo Andrew Mkinga,  akiwa na Anko Bavon Mwakasungula, wakijadili Mjadala kuhusu uraia wa nchi mblili na mambo mengi kuhusu mstakabaliwa nchi yetu, wakiwa ndani ya Studia ya Global Entertainment and News Network (GENN)

Kipindi cha Bongo Views  kitawajia tena LIVE wiki hii, siku ya Jumamosi Aug 24, 2013  kuanzia Saa 11 jioni kwa Saa za Marekani ya kati.  (Saa kumi na mbili jioni kwa Saa za EST US.)
Kwa wale mtakaopenda kushiriki,  msikose kutembelea. HAPA Global Entertainment and News Network (GENN).

Mjadala utakua kuhusu tatizo la madawa ya kulevya nchini.
Ili kuchangia kwa njia ya simu, piga simu namba  (913) 662-1190

Monday, August 19, 2013

Kipengele cha TUNGO ZETU ndani ya kipindi cha NJE-NDANI

CHANGAMOTO
Karibu katika majaribio ya kipengele cha TUNGO ZETU ndani ya kipindi cha NJE-NDANI kinachotayarishwa na JAMII PRODUCTION Redio kutoka Jiji Washington DC Nchini Marekani.
Katika kipindi cha wiki hii ya Jumapili Aug 18, 2013, tulijaaliwa kuwa na Bwana Yasini Landi pamoja na mkewe Salma Moshi, msanii wa kwanza wa kike kucheza na chatu jukwaani nchini Tanzania.
Mazungumzo katika kipengele hiki yalihusu kuhusu nyimbo za zamani kidogo. Salma alizungumzia wimbo wa DUNIA IMANI IMEKWISHA uliyoimbwa na muimbaji mkongwe Marijani Rajabu, mmoja wa watunzi mahiri wa muziki nchini Tanzania.
Yasin yeye alizungumzia wimbo wa CHATU MKALI uliotungwa na Muhidin Gurumo. Kwa maoni, wasiliana nasi kwa barua pepe jamiiproduction@gmail.com
KARIBU UUNGANE NASI

Mapitio ya magazeti na Habari Afrika toka Swahili Radio

Swahilitv’s avatar
SWAHILI RADIO ni kituo kilichoanzishwa Jijini Washington DC USA na Kampuni ya "MMK MEDIA GROUP" ambao wanamiliki Swahili Radio Online,Swahili TV Online,SwahiliTV Blog, Swahili Magazine USA-AFRICA,na The Bridge Show inayoonyeshwa kwenye channel za DCTV.
Sasa wapo kwenye matangazo ya majaribio ambapo wameanza kukuletea vipindi vya "kutoka magazetini" na "Habari za Afrika"
KARIBU UUNGANE NAO

Thursday, August 15, 2013

Justine Kalikawe....Miaka 10 baada ya maziko yake

Tarehe kama ya leo, miaka 10 iliyopita, niliandika HABARI yangu ya kwanza na kuituma katika gazeti la Spoti Starehe. Ilikuwa ni siku nilipotoka kwenye maziko ya msanii maarufu wa Reggae Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Justine Kalikawe.
Habari hii haikuchapishwa gazetini, lakini nafurahi kuwa nikingali na habari hii (kama ilivyotumwa) na katika kuadhimisha miaka kumi ya maziko ya Justine, nimeona ni vema kuirejea

Na MUBELWA BANDIO. Bukoba.
15/08/2003
Safari ya mwisho ya Justine, nyumbani kwake Kitendaguro Bukoba

Maelfu ya wakazi wa mji wa Bukoba na vitongoji vyake alhamisi wiki hii walijitokeza kuusindikiza mwili wa mwanamuziki mkongwe na mahiri katika miondoko ya Reggae Afrika Mashariki Justine Kalikawe ulipokuwa ukizungushwa mjini hapa kabla ya kuelekea nyumbani kwake Kitendaguro kwa mazishi.

Wakazi hao walioonekana kujawa na huzuni, walijipanga kando ya barabara za mji wakati gari lililotangulia msafara uliobeba mwili wa marehemu Justine lilipokuwa likipiga nyimbo zake zenye hisia kali na ujumbe mzito kwa jamii hali iliyofanya wengi wao kushindwa kujizuia na kuangua vilio.

Kalikawe aliyefariki dunia jumatano ya wiki hii katika hospitali ya mkoa wa Kagera mjini Bukoba alipopelekwa baada ya hali yake kugeuka ghafla usiku wa jumanne alizaliwa tarehe 28.08 1967 nyumbani kwao Kitendaguro nje kidogo ya mji wa Bukoba akiwa mtoto wa 7 kuzaliwa kati ya 8 wa familia yao na alipata elimu yake ya msingi darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kibeta mwaka 1974-1977 na kuendelea darasa la tano hadi la saba katika shule ya msingi Muhimbili jijini Dar-es-salaam alikohitimu mwaka 1980. Mwaka 1981 alichaguliwa kujiunga na shule ya Sekondari Tambaza ambako alihitimu kidato cha nne mwaka 1984 na kubahatika kuwa mmoja kati ya vijana 4 waliochaguliwa kujiunga kufanya kazi katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha TIPER cha jijini DSM, kazi aliyoianza mwaka 1985 kabla ya kuiacha kwa hiari yake mwaka 1986 na kujitosa rasmi katika fani ya muziki.

Mwanamuziki huyo ambaye alikwishatoa albamu 8 za audio na 3 za video katika miaka 16 aliyodumu katika muziki wa Reggae, amekuwa kielelezo kizuri cha muziki na utamaduni wa mkoa wa Kagera kwani baadhi ya albamu zake aliziimba katika lugha ya kihaya hali iliyomfanya ajikusanyie mashabiki wengi katika ukanda unaozunguka Ziwa Viktoria, na wakati mauti yakimkuta alikuwa katika maandalizi ya kuzindua albamu yake mpya aliyoirekodi hivi karibuni.

Alifanya ziara za kimuziki katika nchi za Zambia (1988) na Denmark mwaka huu.

Justine aliyelelewa na mama yake Ephrazia Kashebo (71) baada ya baba yake mzazi kufariki akiwa na umri wa miaka (1971) ameacha mke Georgia na watoto wawili wa kike Abayo (7) na niwe(4) na alizikwa nyumbani kwake Kitengule Alhamisi saa 10 jioni kwa taratibu za madhehebu ya Orthodox.

Kifo chake ni pigo jingine katika sanaa ya muziki hapa nchini na ndani ya familia yao baada ya kaka yake aliyekuwa mpiga disko mashuhuri hapa nchini Dj Kalikali aliyefariki mwaka 1991.

Atakumbukwa kama mtetezi wa wanyonge na mpigania haki, amani na utulivu katika jamii, na msanii aliyekuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya UKIMWI na zaidi atakumbukwa kwa vibao vyake kama Roho ya Korosho, Wamachinga, Watu, Maisha na vingine vingi vilivyotamba.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU JUSTINE KALIKAWE MAHALA PEMA
*************
Niliporejea Dar nikakuta HARAKATI za kuandaa Tamasha la Kumuenzi Justine Kalikawe.
Tukiwa Idara ya Habari Maelezo (2003) na Ras Pompidou, Jah Kimbuteh, Ras Inno, Bi Georgia (Mjane wa Justine) na meneja wake wa zamani Allen Mbaga kuzungumzia Tamasha la HAKUNA lililomuenzi Justine
Nikaungana na FAMILIA ya wanaReggae maarufu Tanzania katika kutengeneza video ya wimbo HAKUNA (ambayo haikutoka / sikubahatika kuiona)
Nikiwa na baadhi ya wasanii walioshiriki wimbo ulioitwa HAKUNA (urejee hapa)Hapa ni ndani ya (iliyokuwa) Bacyard Studio tulipokuwa tumekwenda kurekodi Video ya wimbo huo uliokuwa maalum kumuenzi Justin Kalikawe
Unaweza kuusikiliza hapa chini


Moja ya kazi za Justine Kalikawe nilizokuwa nazipenda (na bado nazipenda) ni ile aliyoiimba kwa lugha na midundo ya nyumbani Bukoba.
Wimbo unaitwa NOIJUKA ambao unazungumzia maisha ya utoto (ama niseme ya zamani) na namna ambavyo kama waHaya tuliishi kabla ya kuingia kwa "u-sasa" ulioondoa utamaduni wetu
Ni MAISHA YETU YA KIJIJINIIIIIIIIII
"Ego ninyijuka amakir'Ago"

Wednesday, August 14, 2013

Kijiwe cha Ughaibuni


Karibu katika kipindi kingine cha KIJIWE CHA UGHAIBUNI kinachoandaliwa na Blog ya Vijimambo.
Katika kipindi hiki, wadau hujadili mambo mbalimbali yanayoikumba jamii yetu na kujaribu kuweka mtazamo wao kuhusu namna ya kukabiliana na matatizo wayajadiliyo
KARIBU UUNGANE NAO

Tuesday, August 13, 2013

Swahili Radio kuanza "kupasua anga" Washington DC hivi karibuni

Kampuni mpya ya habari ya MMK Media Group LLC ya hapa Washington DC ambayo inamiliki Swahili Tv, sasa inakamilisha harakati za kuanzisha matangazo ya radio kupitia kituo chao cha Swahili Radio.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopo mtandaoni mwao, kituo hiki cha radio kipo tayari kuanza kurusha matangazo muda mfupi kuanzia sasa.
Kama inavyoonekana hapa chini, Mkurugenzi wa Swahili Radio Bwn. Dickson Mkama (DMK) akiwa katika majaribio ya mwisho mwisho kabla hawajaanza matangazo rasmi.
Kwa taswira zaidi za maandalizi ya kituo hiki, unagana nao hapa

SwahiliVilla blog katika tamasha la FestAfrica 2013 MD USA


Miongoni mwa waliolonga na SwahiliVilla Blog (SVB) ni mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya FestAfrica, mTanzania Nenelwa, kutoka Baltimore Maryland. Ungana na Abou Shatry katika mahojiano haya

Monday, August 12, 2013

Tanzania yangu.....Yenye wasanii walio makini "kupanda chini"

Photo Credits: Reverbnation.com
Nikiwa mwanachuo katika Kituo cha Mafunzo ya Ufundi na Huduma (VTSC) chini ya VETA mjini Dodoma, tulikuwa na somo la UJASIRIAMALI.
Na licha ya kwamba miongoni mwetu hatukuonekana kuvutiwa ama kulipenda na / hata kutilia maanani yaliyofunzwa katika kipindi hicho, kuna jambo ambalo tangu lilipotambulishwa kichwani mwangu na Mwalimu wangu Mr. Lawrence Mashindano, limeendelea kuwa MSINGI wa maamuzi mengi nitendayo.
Na ni jambo ambalo sio tu limeonekana kufaa kwenye UJASIRIAMALI, bali katika mfumo mzima wa maisha. Kuanzia mahusiano mpaka maongezi.
Ni kama vile lolote linalohusisha KUFANYA MAAMUZI limehusisha jambo hili.
Nalo ni HATUA TANO katika ujasiriamali (mimi ntaita hatua tano za maamuzi) ambazo ni O.I.G.I.R
Observe the environment
Identify opportunities
Gather necessary resources
Implement activities
Rip rewards.
Kwangu, hatua hizi tano nimezitumia hata katika kuamua lile la kusema na kuandika pia.
Sasa..........
Nirejee kwenye POST yangu ya leo.
Nimekuwa nikifuatilia mahojiano ya wasanii mbalimbali wa Tanzania na nimeishia kuwaza kama nao wanachukulia kazi yao kama UJASIRIAMALI na kama ndivyo, nawaza kama wanaijua hata hadhira yao.
Yaani kuna wakati (katika hali ya kushangaza kabisa) unasikia msanii ambaye anajua fika kuwa HANA HADHIRA YA KIMATAIFA, anawasiliana na hadhira yake kwa lugha ambayo wengi wa wamsikilizao hawaielewi kwa ufasaha ama hawaitumii kila wakati.
Lakini pia, achilia mbali kuelewa na kuitumia lugha hiyo kwa hadhira yake, bado kuna jambo jingine la msanii mwenyewe kutoimudu lugha hiyo.
Limekuwa kama WIMBI la mahojiano kuhusisha majibu mengi ya kiingereza hata pale msanii anapoulizwa kwa kiSwahili, na hili limenifanya niwaze iwapo MTAZAMO wa wasanii hawa ni kuwa "kwa kujibu kwa kiingereza wanakuwa wamedhihirisha ubora ama ukomavu fulani maishani"?
Kibaya zaidi ni pale wanaposhindwa kueleweka kwa wanaojua kiingereza, wakashindwa kueleweka hata kwa wale wateja halisi wao (ambao si wote wanaielewa lugha hiyo)
Karika ukurasa wangu wa Facebook nilipata kuuliza kuwa ni msanii gani ambaye anapohijiwa kwa kiswahili hujibu kwa kiSwahili bila kuchanganya na kiingereza?
Wengi (wa walioona na kujibu) wakamtaja Diamond.
Sina hakika na uhusiano wa hili na UMAARUFU WAKE, lakini kuna ukweli kuwa ASILIMIA KUBWA YA WASANII WETU WENGI HAWAJULIKANI AMA KUTAMBULIKA KWA KILE WANACHOSEMA (kwa kuwa hawana mafunzo ya kuzungumza), BALI KWA HABARI ZA UDAKU NA KASHFA MBALIMBALI
KUMBUKA....NIMESEMA WENGI. SI WOTE
Wapo wachache ambao wanaendeleza utamaduni wa kuwasiliana vema na hadhira yao, kwa lugha ielewekayo kwao na kufikisha ujumbe wao kwa wadau wao.
Na kwa kufanya hivyo, wanajikuta waki"connect" vema na hadhira yao

Kumbuka.....Mzee Nelson Mandela alipata kusema kuwa "If you talk to a man in a language he understands, that goes to his head. If you talk to him in his language, that goes to his heart."
Kwa tafsiri isiyo rasmi anasema, ukiongea na mtu kwa lugha anayoielewa, yale usemayo yatamkaa kichwani. Ukiongea naye kwa lugha yake, yale usemayo yataelekea moyoni mwake
Ina maana....wasanii wetu waongee na wadau wao kwa LUGHA YA KWAO, ili yale wayanenayo, yawakae mioyoni na sio vichwani.
Wale wanaojitahidi kuwasiliana na wananchi kwa namna inayowa"boa", hawana tofauti na yule anayejitahidi "kukwea chini"


Ni mtazamo wangu tu kwa namna nionavyo tatizo.
Labda namna nionavyo tatizo ndilo tatizo 

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA
Tuonane "Next Ijayo"

Ana kwa Ana ya SwahiliTv na Mfanyabiashara Davis Mosha

Wadau wenzetu wa habari SwahiliTv, walipata nafasi ya kuongea na mmoja wa wafanyabiashara maarufu toka nchini Tanzania Bwn. Davis Mosha alipokuwa katika ziara nchini Marekani.
Ungana na mtangazaji Alex Kassuwi wa Swahili Tv katika mahojiano haya

Friday, August 9, 2013

Ni mwaka mwingine kwangu....Kila mtu na kitu ni shule

FLASHBACK YA MAISHA.......(Japo kwa ufupi)
"you gotta live to learn, you gotta crash and burn,
you gotta make some stances and take some chances,
you gotta live and love and take all life has to give
you gotta live and learn so you can learn to live"
Darius Rucker

Nilipozaliwa tu nikaanza kuwaza. Na mpaka sasa ninawaza. Japo sasa nawaza kwa sauti zaidi. 
Ni kweli kuwa leo ni mwaka mpya kwangu. Tarehe kama hii zaidi ya miongo 3 iliyopita katika hospitali ya Brackenridge, ndipo nilizaliwa. Nikiwa mtoto wa tatu wa familia ya watano wa Mr na Mrs S. Bandio.
Maishani nimebarikiwa kupitia ngazi nyingi. Za kulazimika na hiari. Zenye kuona mambo na kuoneshwa na namshukuru Mungu kuwa katika hayo yote, bado kulikuwa na nafasi ya pili ya kuweza kuyarejea yale niliyokosea na pia kurekebisha na kuboresha niliyotenda vema.
Nikiwa "bwa'mdogo", nilikuwa napenda vitu vingi na nilikuwa na ndoto nyingi. Lakini kama wengi tujuavyo, mazingira ya maisha ya nyumbani (na hasa zaidi ya miaka 10 ama 15 nyuma) hayakutoa nafasi kubwa kwa wengi wetu kutambua na kuendeleza kile tulichopenda. Ilikuwa ni kusoma na kusomeshwa (labda niseme kukaririshwa) kisha utaambiwa ni nini kinakufaa kulingana na matokeo yanayotokana na mitihani ambayo ufaulu wake ungetokana na ufundishaji uliopata na pengine mazingira uliyokulia.
Hivi hujajiuliza kuwa "kama kweli uhandisi ama udaktari ama fani yoyote ya 'kisasa' si kitu cha kuzaliwa nacho, kwanini ndugu zangu wa Rubafu ama Nangurukulu ama Kasulu ya ndani ama Nanjilinji hawafiki huko?"
MAZINGIRA.
Anyway!!!!!!!
Ina maana kuna wengi walioangukia ualimu kwa kuwa "combi" za O-level ziligoma nawengine kuelekea "A-Level" kwa kufuata uchaguzi waliofanyiwa kutokana na walivyofunzwa.
Well!! Wacha nirejee kwenye "topiki"
Nilijikuta nikiwa mpeenzi sana wa kazi mbili zisizokuwa na uhusiano (kwa mtazamo wa wakati huo) ambazo ni UFUNDI na UTANGAZAJI. Nikiwa mdogo nilikuwa sikosi kusikiliza na kuchanganua walichosema watangazaji.
Na bado nakumbuka kuwa shabiki mkubwa (mpaka sasa) wa Uncle Charles Hilary. Nilipenda kusikiliza alichosema na alivyosema. Matumizi ya lugha na mengine mengi. Pia kulikuwa na Uncle J Nyaisangah ambaye alikuwa akinifanya nihisi jengo la utangazaji ni kuuubwa kiasi kwamba bendi zoote zinakaa pale na akiita bendi fulani huanza kupiga muziki. Nilipenda kazi ya kuwa na uwezo wa kuziona bendi zote na kisha ukaamua ni ipi itumbuize wimbo gani na pengine kwa muda gani (kulingana na uamuzo wako na fundi mitambo).
Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa
Lakini pia nilipenda "kuchokonoa". Nilipenda saana kuona kitu kikitengenezwa na kutoka katika ubovu mpaka utendaji kazi. Ni hali hii hii niliyoiona kwa madaktari wanapotibu lakini utabibu haukuwahi kutekenya mfumo wa maamuzi ya tamaa za kazi.
Nikirejea nyumbani, nili/ nimebahatika ama NIMEBARIKIWA kuwa na familia tengefu. IMETENGEMAA kiasi ambacho kwa namna nyingine iliniathiri na kuamini kuwa HAKUNA MIGONGANO KWENYE FAMILIA. Niliamini kilicho kigumu kwenye familia ni kulea maana niliona namna nilivyokuwa "changamoto" kwa wazazi na walezi wangu.
Lakini mara zote walionesha na kuwa mfano wa nini familia yaweza kufanya na kurekebisha mtu kwa upendo hata kama uliambatana na bakora.
NAWASHUKURU KWA HILO.
Maisha yangu ya shule yalianza mapema saana. Nilipojitambua kuwa ni kiumbe, nilikuwa naenda shule. Wazazi wangu walinizoesha ama kunianzisha shule nikiwa mdogo na nilikua nikitambua mfumo wa kuamka kwenda shule na kurejea nyumbani kuendelea na kazi za nyumbani
Malezi ya nyumbani nayo. Hahahahahaaaaaaaaaa. Kwa akili za wakati huo sikuona kama yanafaa. Sasa hivi wala siwezi kubadilisha kwa lolote. Nyumbani tulifunzwa kila kazi iendanayo na umri wako. Ungejua kufua muda ukifika, kupika na kusafisha, kupanga na kupangua. Yaani tulijikuta tukitambua namna ambavyo vitu vyawa vilivyo na hilo lilinifanya kuthamini kila "kidogo" kitendwacho" maana nilijua "shughuli yake".
Baada ya miaka 18 na wazazi, nikaachana nao na kuanza maisha ya ndugu, jamaa na marafiki. Nikiwa na Dada zangu na walezi kama Mama na Baba wadogo, Shangazi na Wajomba, Shemeji na Kaka na Dada na wengineo.
Hapa napo si padogo. Niliendelea KUJIFUNZA maisha ya kuwa mbali na wazazi (ambao kwa namna fulani wana wajibu wa lazima wa malezi kwako) na kuanza kukua na kutambua kuwa naishi na walio na wajibu wab hiari maishani mwangu
Nikaenda chuo ambako nako nikakutana na wenzangu ambao nao wakajenga sehemu kuu ya maisha. Na baada ya chuo nikarejea kusaka maisha na kisha KAZI.
Huko nako nikakutana na watu wa tofauti, wenye makuzi, mila, desturi na mitazamo tofauti.Nako nikafunzwa.
Lakini maisha hayajawahi kuwa na mwisho na wala hayaonekani kuwa na mwisho wa kujifunza. Nimekuwa nikikutana na watu wa aina mbalimbali, katika mazingira mbalimbali na kwa namna mbalimbali. Nimeonana na kuwasiliana na watu na pia nimetambulishwa na kutambulisha watu. JAMBO MOJA NINALOMSHUKURU MUNGU ni kuwa katika kila nikutanaye naye, NAJIFUNZA
Kila mtu kwa namna ambavyo amekuwa mbele yangu amekuwa DARASA tosha kutambua ambalo sikulijua.
Kila kitu ambacho nimetenda ama kutendewa kimekuwa darasa tosha kwa maisha niliyopo na yajayo.
Nikisema nianze kutaja kila aliyenibariki katika miongo hii mitatu iliyopita, sitaweza lakini hii haimaanishi kuwa sitataja wachache kwa majina na wengi kwa mjumuisho.
Wazazi wangu wapendwa, Kaka na Dada zangu. Natambua kuwa ninyi ndio mliojenga MSINGI wa maisha yangu.
Walezi wangu ambao niliachwa nao wazazi walipokuwa kazini na wale walionilea nilipotoka kwa wazazi, ninyi mlipalilia pando la wazazi.
Marafiki na wale wajihesabio kuwa maadui. Ninyi mmenifunza kwa njia iliyonifaa na nawashukuru mno.
Kipekee napenda kumshukuru Da mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye bado namtafuta na naendelea kuomba msaada wa waungwana kuniwezesha kuniunganisha naye.
Kwa sasa.............
Sina budi kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mke wangu mpenzi Esther na binti zetu Paulina na Annalisa 
Ninyi mmekuwa kama STRESS-BUSTERS wa maisha haya magumu. Mmekuwa yeyusho la kero na hasira za wengine juu yangu na kuwa msingi na mhimili wa pale nitelezapo.
NAWAPENDA NA KUWAHESHIMU MNO
Kwa yeyote na chochote nilichokutana nacho maishani kwangu, na ambacho kimekuwa shule na makuzo yangu.
NAWAPENDA SAAAANA
Ni mwaka mwingine maishani mwangu, na kila mtu niliyekutana naye na kila kitu nilichokutana nacho NIMEJIFUNZA, na kwa kila nitakayekutana naye na kila nitakachokutana nacho, NITAENDELEA KUJIFUNZA.
Baraka kwenu nyote

Ni siku mpya kwangu. Mwaka mpya kwangu. Ni siku yangu. Asante kwako

Siku zinasonga na kwa hakika licha ya ugumu tupitiao, tukiangalia nyuma twaona kama jana tuu tulipokuwa tukicheza kama watoto.

Nami sasa nimetulia kuangalia maisha yangu yaliyopita katika siku hii ninayokumbuka kuzaliwa kwangu. Na ninajifunza mengi kwa kukumbuka mengi. Najua maisha yangu yasingekuwa yalivyo kama nisingezungukwa na watu niliozungukwa nao. Labda ningekuwa na watu tofauti ingekuwa zaidi ya hapa ama pungufu yake, lakini kwa sasa sina la kulaumu bali NASHUKURU KUWA NILIVYO.
Kwa hakika kuna wengi waliogusa maisha yangu ambao kwa namna moja ama nyingine wamebadili maisha yangu. Huwa nawafikiria saaana na mara kwa mara nimekuwa nikijaribu kuandika chini watu hao ili niweze kuwashukuru kwa pamoja lakini nimeshindwa. Tarehe 7 Aprili nilijaribu kwa mara ya mwisho kuwashukuru wote lakini nikashindwa na ndio chanzo cha kuandika kuwa HUWEZI KUWAHUKURU WOTE, WAOMBEE TUUU (Bofya hapa kusoma).
Kila mmoja ana nafasi ya pekee kwangu.
Kwa wanafamilia yangu sina la kusema. Wakubwa mmekuwa mkinionesha njia kwa upendo na unyenyekevu na mara zote kunisaidia pale niangukapo na wale wadogo kwangu mmekuwa mkinitia moyo pale nilipoonekana kukosa wa kuwa upande wangu.
Shukrani kwenu.
Kwa wale tuliocheza wote, furaha tuliyokuwa nayo wakati huo ndio chanzo cha fikra za sasa. Tuliosoma wote, bila ninyi nisingeweza songa mbele kwani mlisaidia kwa namna kubwa saaana.
Wale niliofanya nao kazi na hawa tunaoendelea kufanya kazi ya kuielimisha jamii na zaidi wale wasomao hapa kusaidia kunielewa, NAWAPENDA SAAAANA.
Wale MARAFIKI ZANGU ambao tumekutana kwa namna mbalimbali na bado tunajaliana na kusaidiana....NAWATHAMINI SANA
Labda nitoe upendeleo kwa watu wanne.
Mmoja ambaye licha ya kuthamini mchango wake kwangu na kumuombea kila leo, bado nahitaji msaaada wa kuwasilaiana naye. Si mwingine bali ni Dada mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye niliandika habari ya kumtafuta HAPA (bofya kuisoma) na bado naendelea kusubiri mawasiliano naye.
Nirejee wa wanangu wapenzi....Paulina na Annalisa. Hawa wamekuwa stress busters kwangu.
Wamekuwa zaidi ya faraja pale nichokapo na pengine ni TASWIRA ya nini kinatakiwa kuendelea.
Mara kadhaa nilipofanya / kufanya UPUUZI, nawakumbuka ama kukumbushwa kuhusu hawa na hilo hurejesha fikra kuwa SIKO DUNIANI KWA AJILI YANGU TU.
Wazazi na walezi (wema) mwalielewa hili.
MWISHO NI SALAMU ZA UPENDO KWA WANGU Esther.
NAKUPENDA SAAANA, NAKUHESHIMU, NAKUTHAMINI NA NAPENDA UTAMBUE KUWA UWEPO NA USHIRIKIANO WAKO MAISHANI NI KATI YA VITU VYEMA NINAVYOJIVUNIA KATIKA MAISHA.
SINA LA ZIADA NINALOWEZA KUMUOMBA MUUMBA
Ni mwaka mpya Kwangu, Ni siku yangu na ASANTE KWAKO
THANK YOU LORD

Tamasha kubwa la muziki wa Injili kufanyika Washington DC kesho

Waimbaji wanaofanya vema kwenye muziki wa Injili Afrika Mashariki, Upendo Kilahiro na Christina Shusho, watatumbuiza katika Tamasha kubwa la Injili litakalofanyika Jumamosi hii jijini Washington DC
Kama walivyoongea kwenye VIDEO HII, waimbaji hao wamekamilisha maandalizi ya tamasha hilo ambalo pia litashirikisha waimbaji wenyeji wa hapa Marekani.
Tamasha hilo kubwa lililo sehemu ya Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries litafanyika siku ya Jumamosi kuanzia saa kumi kamili mpaka saa tatu usiku (6:00pm - 9:00pm) na kiingilio kwenye tamasha hilo kitakuwa ni dola kumi ($10) kwa watu wazima, bure kwa watoto.
Anwani ambapo litapofanyika tamasha hilo ni
The Way of the Cross Gospel Ministries 
(at University United Methodist Church) 
3621 Campus Drive 
College Park, MD 20740 
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na
Mch. Ferdnand Shideko +1 240 476 6718 ama
Ms Flora Mnkande +1 240 217 6335
Waimbaji hawa wote watatumbuiza nyimbo zao za zamani na mpya na wanawaalika watu wote kujumuika nao na waimbaji wenyeji kuweza kupata BARAKA kwa njia hii ya uimbaji

Balozi Mulamula na Balozi Nyang'anyi washiriki sherehe za Idd na waTanzana wa DC



Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mustafa Nyang'anyi (kulia) akiwasili kwenye park ya Wheaton, Maryland kwenye sherehe ya Eid El Fitr iliyoadhimishwa Alhamisi Aug 8, 2013 baada ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani kuisha. Sherehe hii iliyoandaliwa na jumuiya ya Waislam waishio DMV, TAMCO pia ilihudhuriwa na Balozi wa sasa wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

Balozi mpya wa Tanzani nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akilakiwa na  Afisa Ubalozi Suleiman Saleh wakati anawasili kwenye sherehe za Idd El Fitr.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Mustafa Nyang'anyi, viongozi wa TAMCO na wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
Picha zote kwa hisani ya VIJIMAMBO BLOG

KWA PICHA ZAIDI, BOFYA READ MORE

Thursday, August 8, 2013

Eid Mubarak


Twapenda kuwatakia ndugu zetu waamini wa dini ya kiIslam siku njema na mwanzo mwema wa maisha mema waliyojifunza ama kuyaanza wakati wa mwezi mwema wa Ramadhani.
Tunawaombea muweze kuendeleza uvumilivu, kujitoa na kujali ambako mmeonesha wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa hakika mwezi umekuwa mwema miongoni mwetu kwa kuwa tumeishi maisha yampendezayo Mungu, na naamini kwa kuendeleza yale mema tuliyoyaishi katika mwezi huu, tunaweza kuufanya mwaka na miaka yote kuwa na wema kama ilivyokuwa kwenye mwezi huu.
IDD NJEMA

Wednesday, August 7, 2013

Shusho, Kilahiro kuhudumu Washington DC wikiendi hii

Watumishi wa Mungu Christina Shusho na Upendo Kilahiro, mwishoni mwa wiki hii watahudumu katika jiji la Washington DC na Vitongoji vyake (DMV).
Shusho na Kilahiro ambao ni miongoni mwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, wameshawasili Washington DC tayari kwa huduma hiyo ambayo ni sehemu siku tatu za  Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way Of The Cross Gospel Ministries.
Maadhimisho haya yataanza siku ya Ijumaa na kumalizika Jumapili
Maadhimisho haya yatafanyika
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa watumishi hawa kuhudumu pamoja kanisani hapo katika kipindi cha miaka miwili, ambapo mwaka 2011waliungana na Upendo Nkone kuhudumu katika Mkutano mkubwa wa Injili ulilofanyika kanisani hapo.
 Watazame na kuwasikiliza wanavyoelezea siku hizo
 
            USIKOSE!!!!!
Na hizi ni baadhi ya nyimbo zao mpya
NI KWA NEEMA wake Christina Shusho (hit as always)

Na huu...NKIZA
Moja ya nyimbo mpya za Upendo Kilahiro kutoka katika albamu yake mpya aliyoimba kwa lugha ya kiRundi ya SINZOGIT'ICO NTIYA
IMAGINE
Hawa wote katika JUKWAA MOJA wikiendi hii

Tuesday, August 6, 2013

Kijiwe cha Ughaibuni


Karibu katika kipindi kingine cha Kijiwe cha Ughaibuni kinacholetwa kwenu na Blog ya Vijimambo.